Kama mipakani COVID19 iko hivi, Tanzania yenyewe hali iko vipi?

Kama mipakani COVID19 iko hivi, Tanzania yenyewe hali iko vipi?

Madereva wa masafa ni njia kuu ya kusambaza ugonjwa wowote ule... UKIMWI, Malaria, Covid-19, n.k
Wana hulka ya kuwa na watoto wadogo hadi wakubwa maeneo mbali mbali...!!
 
Mkuu mtaani maisha ni Yale yale mtaani kwangu sijashudia mgonjwa wa corona

Ila nikiingia Twitter na jamii forum Ndio Chadema wanaeneza sana uwongo kuhusu corona
Jiulize, Rais wetu yuko wapi wiki ya tisa sasa? Tafakari ndugu!
 
Uwezekano ni kwamba walokwishaambukizwa ni wengi sana ila lwakuwa kinga zao za mwili zinafanya kazi ndipo idadi ya wanaougua haiwi kubwa, kama hao madereva wangekuwa wanaugua hakika wasingeshika usukani kuendesha gari tena umbali mrefu.

Kumbuka hali ya upimaji nchini haiko kwa kasi. Watu wa afya wanapaswa kufanya uchunguzi mpya dhidi ya huu ugonjwa kwani visa vya wabaosemekana kufa nao ni vya ghafla sana.

Jihadhari ugonjwa upo
 
Mkuu unauhakika gani idadi ya waonaugua sio kubwa? Hivi kunaupimaji Tz? Acha kuumauma maneno, people are dying. Au mnataka malaika aje apashe habar???
Upimaji upo Mimi ni mhanga nilikuwa suspect na nikapimwa.
Kuhusu kuugua au kutougua taarifa za ugonjwa na dalili zinaelezwa daily.
Hakuna kuuma wala kutafuna hao wanaokufa daily wanafia mitaani nasi tunaishi mitaani, hizo maiti zinazozagaa mnaziona wenyewe tu? Achani ramli pata picha mitaani kwa ndugu na jamaa pia
 
Mkuu unauhakika gani idadi ya waonaugua sio kubwa? Hivi kunaupimaji Tz? Acha kuumauma maneno, people are dying. Au mnataka malaika aje apashe habar???

Kwani kuugua kunafichika mazee?
MTU mgonjwa anaweza toa Lori dar kuelekea Kenya? Mgonjwa kabisa?
Nazungumzia kuwa na maambukizi ni tofauto na kuwa mgonjwa.
Ulimsikia rc wa Kilimanjaro akisema amepima lakini hana hata dalili yu mgonjwa, unafuatilia reports za WHO kuwa MTU aweza kufa ghafla akiwa na maambukizi lakini haluonyesha ugonjwa.
Kwa mantiki hiyo, waloambukizwa waweza kuwa wengi ila wagonjwa kwa kuonesha dalili mpaka kufa si wengi na yamkini wengine wanapona bila kujijua kutokana na hali ya upimaji sio kubwa kwa RAIA lakini kiukweli maradhi mpaka kifo hakifichiki, kama kungekuwa na massive death tungeshuhudia bila kuhadithiwa..
 
Nahisi tumeipotezea
maana huko Tandika naendaga almost daily tunabanana tena sikuizi hata barakoa watu hawavai.. mbagala push za kugombea daladala zinazidi maradufu ni kama ugonjwa haupo vile.
Na mimi ni miongoni mwa ambao tumejitoa mhanga liwalo na liwe
 
Ni Hivyo yaaani[emoji41][emoji41]
20200513_073531.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Wakuu,

Hali ya maambukizi ya corona hapa nchini kwa sasa haifahamiki zaidi ya sintofahamu tu huku watu wakiendelea kufanya shughuli zao kama kawaida

Watanzania tuko njia panda sasa tusielewe hali ya nchi hii kwa vita ya covid19 mpaka kujiuliza maswali kama hali ya mipaka ya nchi iko hivi, Tanzania yenyewe hali hali ikoje? I mean huko Dar es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na kwingineko kwingi maambukizi yakoje

Kwa sasa tunashuhudia mipaka ikifungwa na nchi zote jirani kututenga Rwanda, Uganda, Kenya, Zambia zote zimetutenga kwa sababu watanzania tunasambaza corona katika nchi hizo

Tuendelee kujiuliza yaani dereva wa lori ambaye anafika bandari tu kupakia mzigo huku akiwa ajajichanganya sana huko mitaani anapata corona je wale kutwa wanapambana na usafiri wa daladala, mishe za kariakoo, dereva bodaboda watakuwa na hali gani?

Tanzania tuna hali gani ikiwa wasafiri wa malori tu wasio na mizunguko na mchanganyiko mkubwa wa watu wanaathirika vibaya dhidi ya corona?
Mbona una bwaja bwaja kama demu, mbona hujasema mpaka fulani idadi ni hii, mpaka fulani idadi ni hii n.k .
Na hii ya mipaka kufungwa kawaulize wenye nchi zao idadi yao ipoje, Sasa kama jirani wana matatizo yao ndio tuyabebe??
 
Mbona una bwaja bwaja kama demu, mbona hujasema mpaka fulani idadi ni hii, mpaka fulani idadi ni hii n.k .
Na hii ya mipaka kufungwa kawaulize wenye nchi zao idadi yao ipoje, Sasa kama jirani wana matatizo yao ndio tuyabebe??
Sawa mke wa meko nimekuelewa
 
Back
Top Bottom