Kama mipakani COVID19 iko hivi, Tanzania yenyewe hali iko vipi?


MKuu tuongeze dua tu.
 

ndugu wacheni ujinga,
Hizo nchi zote zisha kontrol huu ugonjwa, na wanajua wapi upo na wapi hakuna, nani anao na nani hana, kwasasa maambukizi ni machache na ndio maana wanafikira kufungua badhi ya sehemu.

huku kwetu hakuna takwimu na hakuna anayejua status ya maambukizi ikoje kama inashuka au inapanda.

kifupi tumekwisha.
 
Hali ni mbaya - majaliwa
DAR watu wanapukutika - Makonda
 
Juzi usiku saa 6 naangalia news mpaka sasa USA watu wasio na ajila ni 15% kabla ya corona saiz ni 33% mambo yanazidi kuwa magumu tu sasa kama taifa kubwa tu USA wanateseka sisi ni nani tufunge mipaka au tuake ndani?

kuna watu wanaona kinachofanyika ni upumbavu lakini hawajui chochote kuhusu ugonjwa ambao dawa yake ni chanjo na ni muda gani chanjo huchukua kukamilika na kuanza kutumika huchukua nawaona tu wanabwabwaja tu ila saiz kila mtu ataelewa tu vizuri ukweli wa mambo.

maana hakuna chanjo ya mwaka mmoja hizi taarifa tunazopata niza matumaini tu lakini chanjo huchukua miaka 10 kukamilika huko lakini kama hii itakamilika ndani ya muda mfupi basi itakuwa ndio chanjo ya kwanza kukamilika kwa muda mfupi toka dunia ianze kuumbwa lakini pia kumbuka chanjo ya Indonesia ile ya muda mfupi ilivyo uwa watoto na ndio maana watu weupe hawataki vaccines.
 
Ubaya ni uhaba wa taarifa lakini ubaya zaidi ni dhana tunazozitengeza kutokana na taarifa haba.
 
Kwa hiyo unataka tufanye Nini Ndugu??
 
Hivi chadema walishakulia nini? Kila anayetoa taarifa humu wewe unawaza chadema du! Na unawachukia kweli. Utakuwa unaumia sana juu ya chadema. Si uwe una nyamaza tu. Eti hali mitaani ni kawaida, ndiyo ni kawaida kwakuwa wakubwa wamezuiliwa kupima, lamini wakipima wagonjwa ni zaidi ya elfu 10
Mkuu mtaani maisha ni Yale yale mtaani kwangu sijashudia mgonjwa wa corona

Ila nikiingia Twitter na jamii forum Ndio Chadema wanaeneza sana uwongo kuhusu corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha upumbavu. Mtaani kwangu wamekufa wawili na zaidi ya watu watano walikua wanaumwa wamepona. Na pia kuna rafiki yangu arusha amekufa kwa corona. Acheni uchawi wa kuwaambia watu hamna ugonjwa na upo. Semeni ukweli kwa kumuogopa Mungu hata kama unauma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana control nini? Watu acheni masihara.... Labda ungeniambia wanajaribu.
 
Karibu mtaani halafu baadae uje kupost ulichokiona,huku maisha bado yanaendlea kama kawaida ingawa taarifa za maambukizi hatuzipati lakini maisha ya kawaida yanaendelea mjini kazi kama akawaida ingawa wale watu wa utalii imekula kwetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…