Kama misikiti inaweza kujengwa mitaani kwa uhuru, kwanini kujengwa kwa makanisa kuwe kero Zanzibar?

Kama misikiti inaweza kujengwa mitaani kwa uhuru, kwanini kujengwa kwa makanisa kuwe kero Zanzibar?

Ndio wanachokofanya huko moshi, kuna sehemu ukitaka kujenga msikiti wakikubaini tu biashara imeishia hapo
Unataka kubalance story sehemu gani Moshi wanakataa kujenga misikiti?
Machame 98% ni christians lakini misikiti ipo c chini ya 4 na msikitini mwingine unajengwa nkweshoo,mbona hakuna hizo chokochoko za kubomoa misikiti?
Kinachowasumbua huvumilivu kwenu ni 0 ,na mkienda ugenini mnataka wenyeji waifate Imani yenu kilazima watake wasitake lakini watu wapo cool tu
 
Wavunje tu hata hapa mtaani Kuna kanisa linapiga sana kelele usiku kucha kila ikifika ijumaa had jumapili watu hatulali hili nitalivunja mwenyewe

Shubaaaastard
 
Nimeshuhudia taarifa na video mtandaoni ikionyesha kanisa dogo la TAG maeneo ya Zanzibar likivunjwa na greda kwa amri ya wakuu fulani wa serikali wa Zanzibar.

Sababu za kimsingi za hayo kutokea ni kukosekana kwa uvumilivu wa kidini kwa baadhi ya wakazi wa Zanzibar dhidi ya imani zingine, jambo ambalo linalindwa na watawala wa Zanzibar kwa miongo yote. Japokuwa wakuu wa serikali huko Zanzibar wamekuja na sababu nyingine duni na kijinga (wanadai wamevunja kanisa hilo kwa sababu za taarifa za kitisho cha hali ya hewa kuhusu mvua inayoweza kuleta mafuriko maeneo hayo!)

Tunapaswa kutambua haya.
1. Karibu mitaa yote ya Zanzibar kuna misikiti mikubwa au midogo.

2. Karibu misikiti yote ya Zanzibar ina vipaza sauti (horn speaker) zinazopiga adhana kila siku kutwa mara tano.

3. Karibu misikiti yote ya Zanzibar imejengwa kwenye makazi ya watu au jirani kabisa na makazi ya watu.

4. Mpaka sasa Zanzibar haina maeneo rasmi ya wazi yaliyotengwa mahususi kujenga nyumba za Ibada tu na kujulikana kwa watu wote.

5. Serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanzania kikatiba zote hazina dini na hazipaswi kufuata mlengo wa imani yoyote ya kidini zaidi ya kuheshimu na kulinda uhuru wa imani zote.

MAMBO MUHIMU YA KUTAFAKARI
-Kwanini kuwe na shida kila mara dhidi ya taasisi za kikristo zinapotaka kujenga makanisa, kuabudu kwa uhuru au kueneza imani yao maeneo ya Zanzibar?

-Kwanini Serikali ya mapinduzi Zanzibar na serikali ya muungano zinashindwa kulinda uhuru wa kuabudu kwa wakristo waliopo Zanzibar?

-Kwanini jamii za imani ya kikristo zionekane kama ni wavamizi, wapitaji na wageni waliokosa mwenyeji kila mara huko Zanzibar?

TAFAKARI

makanisa ya walokole ni kero. Yavunjwe tu​

 
Unataka kubalance story sehemu gani Moshi wanakataa kujenga misikiti?
Machame 98% ni christians lakini misikiti ipo c chini ya 4 na msikitini mwingine unajengwa nkweshoo,mbona hakuna hizo chokochoko za kubomoa misikiti?
Kinachowasumbua huvumilivu kwenu ni 0 ,na mkienda ugenini mnataka wenyeji waifate Imani yenu kilazima watake wasitake
Misikiti 5 tu wakati wakati Zenji Kuna makanisa yasiopungua 30

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Sasa ngoja nikupe shule kidogo bwanamdogo. Tanzania inaundwa na nchi 2 zilizo huru kabisa. Zanzibar na Tangayika . Katika muungano yapo masuala ya muungano na yasiyo ya muungano katika uendeshaji wa serikali ( Nenda kayatafute uyasome). Suala la Tanganyika kuvaa koti la muungano siyo ticket ya kuingia zanzibar na kuharibu mila na desturi za watu wa Zanzibar. Kwanini tusijivunie utanganyika wetu kama wazanzibari wanaojivunia uzanzibari wao? Mila zetu sisi ni mchanganyiko kula kiti moto, makanisa mengi ya kina mfalme zumaridi n.k, uislam pia upo tanganyika. Lakini kwa zanzibar ni tofauti na hawataki sasa kwanini kulazimishana?
Ruka ruka unavyojua ila fahamu Zanzibar kuwa na katiba yake na Tanganyika kutokuwa na katiba yake hakuipi Zanzibar upenyo wowote wa kujifanyia mambo Kinyume na Katiba ya Jamuhuri. Katiba ya Jamuhuri ni moja na hiyo ndio kuu (supreme) kwa sasa.
 
Nafikiri wanafanya tathmini kwa haya makanisa ya kilokole ya miujiza na unabii wa kuunga na superglue watoaji shuhuda wengi ni Waislamu, fanya tathmini kwa kwa Mwamposa

Niliandika tena kwenye uzi mwingine, hata sisi wakristo tuna ushamba huo kwenye ngome zetu wala tusikimbilie kulaumu waislam tu

Nimetoa mfano wa eneo nililozaliwa na kukulia, Kibosho Moshi, huko kujenga misikiti au kanisa lisilo RC ni mbinde, Vita yake utachemka maana inapigwa na padre, waumini, na serikali za mitaa ambao wote hao ni Wahafidhina RC.

Kumbe kama taifa Tunahitaji kustaarabika na kuishi kwa kuchukuliana na kuheshimiana.
Kuwe na mipaka na utaratibu wa uendeshaji ibada maana makanisa ya kilokole yamezidi kusumbua usiku kucha.
 
Na hili ndiyo nalolikemea.
Mimi bado lawama zangu ni kwa serikali.
Mambo hayako regulated, sijui wanaogopa nini hasa?
Maadam wameshindwa kupangilia makazi ya watu na nyumba za ibada, basi waangalie nukta ya noise pollution bila kuogopa imani za watu. Binafsi, sipingi nyumba za ibada kuwa kwenye makazi ya watu, nachopinga ni makelele maana kwangu mimi hizi ndiyo hasa usumbufu wenyewe.
Ningekua na mamlaka, ningedhibiti loudspeakers misikitini na makanisa ya kilokole. Period!
Ilipaswa ikae hivyo, wewe kweli ni GT halisi.
 
Ruka ruka unavyojua ila fahamu Zanzibar kuwa na katiba yake na Tanganyika kutokuwa na katiba yake hakuipi Zanzibar upenyo wowote wa kujifanyia mambo Kinyume na Katiba ya Jamuhuri. Katiba ya Jamuhuri ni moja na hiyo ndio kuu (supreme) kwa sasa.
Mbumbumbu kumbe nimepoteza muda wangu bado hujaelimika.
 
Ndio maana lukuvi alisema waislamu ni magaidi ndio maana tanganyika inaidhibiti zanzibar
 
hawa wazanzibar ni wapuuzi Sana, 2010 niliwahi kushushwa kwenye gari zao za chai maharage bila sababu yoyote kisa tuu nimemuongelesha msichana aliyekuwa ameketi kando yangu kumuulizia kitu ninachoenda kushukia.


pia sokoni hapo darajani lijamaa limoja lilikataa kuniuzia mashine ya kukamua juisi ya miwa, mpaka nilitafuta mzanzibar akanisaidia kununua Kwa niaba yangu.
...na wewe ukaubali kushushwa kwenye gari kwa sababu hiyo..?
 
S

Hatuogopi competition ya imani, hatutaki kupotoshwa na hatutaki kupoteshewa watoto wetu. Ikiwa unasema kuwa tunaogopa kupotoshwa, then yes sawa na wala hatuoni aibu kwa hilo tunaogopa kupoteshewa familia zetu, tunaogopa adhabu ya Mola wetu siku tukirudi kwake.
Sio hamtaki kupotoshwa ila mnataka nyie na watoto na vizazi vyenu visiione pepo kwa mafundisho ya uongo na ya chuki..... Eti ukijilipua unaenda peponi huyo allah wenu bana aisee....
 
Wazanzibari wameukataa huu uhayawani wa makanisa haya feki.
Inashangaza huku Bara mtaa mmoja kuna makanisa matano!
Makanisa ni mengi kuliko waumini,matokeo yake ni makelele tu mitaani.
Kingine majority ya Wazanzibari ni waislam na huu ni ukweli ulio wazi.Hatuwezi kulazimisha Wazanzibari waishi kinyume na Utamaduni wao.

Jambo linalonishangaza Zanzibar,Sheria hizi na tofauti za Utamaduni haziwabani WAZUNGU kufanya watakavyo.
Mwezi mtukufu ukiwa na Ngozi nyeusi huwezi kula mahala popote Zanzibar,hata hoteli za nyota tatu au nne nilizowahi kutembelea nilinyimwa hata kuuziwa soda tu!
Lakini wazungu wanapata ulabu bila wasiwasi!.This is tantamount to slavery!

Tupo kwenye “Nchi” yetu lakini unabaguliwa na Mzungu wanamtukuza!
Beach wazungu wanakaa uchi lakini mtaani Mwanamke aliyeumbika akivaa nguo wao wanayoiona sio sahihi wanampiga na kumdhalilisha!
Sielewi mantiki yake!!.
Wazanzibari wana mambo ya ajabu sana,inahitaji moyo kuishi nao vizuri,unahitaji kuwa zaidi ya bwege ili uende nao sawa.
Ni ngumu kujifanya bwege kama wewe sio bwege,hasa ukiwa katikati ya mabwege.Bora uwe bwege kwa wenye akili.
Cha msingi tuwaache na Maisha yao.
....ni Wajingaz. Period.
 
Hilo kanisa la kihistoria ni kivutio kikubwa cha utalii na linahifadhi historia muhimu ya Zanzibar hivyo huwezi kulibomoa labda uwe na matatizo ya akili.
Kwa sasa hivi ndio haiwezekani... Lakini wangeamua kufanya hivyo baada ya mapinduzi wangeweza
 
Back
Top Bottom