Kama mnamuona Rais Samia ameshindwa kusimamia Katiba na kulinda rasilimali zenu muwaombe Wabunge wamuondoe kwa Ibara ya 46A ya Katiba

Kama mnamuona Rais Samia ameshindwa kusimamia Katiba na kulinda rasilimali zenu muwaombe Wabunge wamuondoe kwa Ibara ya 46A ya Katiba

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kila kona mnalalama, eti mafuta yanapatikana kwa bei juu, Chakula bei juu, umeme umekuwa unakatika masaa 24, rushwa na uonevu kila kona hii ni ishara mbaya.

Mkuu wa nchi yetu anapoapa ili atuongoze huwa anaapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT.

Sasa kama Katiba ilitungwa ili Watanzania tusikwame kwa kila kitu tunapoishi hapa nchini, halafu sasa kila kitu hovyo. Maana yake Mkuu wa nchi amekwama kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT.

Watanzania kila jimbo tuwatume Wabunge wetu waungane ili wapitishe Azimio la kumuondoa Rais Samia ili tusiteseke kama sasa.
 
Kila kona mnalalama , eti mafuta yanapatikana kwa bei juu, Chakula bei juu, umeme umekuwa unakatika masaa 24, rushwa na uonevu kila kona hii ni ishara mbaya.

Mkuu wa nchi yetu anapoapa ili atuongoze huwa anaapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT.

Sasa kama katiba ilitungwa ili Watanzania tusikwame kwa kila kitu tunapoishi hapa nchini, alafu sasa kila kitu hovyo. Maana yake mkuu wa nchi amekwama kuilinda na kuitetea katiba ya JMT.

Watanzania kila jimbo tuwatume Wabunge wetu waungane ili wapitishe azimio la kumuondoa rais Samia ili tusiteseke kama sasa.
Wabunge wapi hao!? Hawa wa ccm waliowekwa na Magufuli!? Hawana ubavu huo ni waoga kama kunguru na njaa kama zote. Hawana uzalendo kwa nchi yao kabisa. Wananchi tumewaona hawafai kabisa baada ya kuridhia utopolo wa DP World.
 
Sasa mbona wananchi wanalia? Umeme hakuna, maji ya mgao, ufisadi na mikataba mibovu ...
Umeme na maji kukosekana ni tangu awamu ya kwanza ya Tanzania, ufisadi upo kila awamu watu wanaiba kila mahali.

Mikataba mibovu ni uelewa wetu wa kijamii kuwa mdogo na hulka ya kupenda kuongea ambavyo mtu hata haelewi anaongea kitu gani.
 
Hapa ndipo unafanya Watanzania kumkumbuka hayati JPM. Bora ukae kimya puuzi wewe
 
Mpuuzi ni wewe unayemuona hayati JPM kuwa ni sawa na malaika. Alijawa ukabila mwingi na aliwakera wengi tu.

Wewe kuwa ndugu yake haimaanishi kwamba alikuwa msafi sawa na malaika.
Alipokuwepo umeme ulikatika? Bandari zilibinafishwa? Mimi naongelea ukweli sio ushabiki
 
Back
Top Bottom