Kila kona mnalalama, eti mafuta yanapatikana kwa bei juu, Chakula bei juu, umeme umekuwa unakatika masaa 24, rushwa na uonevu kila kona hii ni ishara mbaya.
Mkuu wa nchi yetu anapoapa ili atuongoze huwa anaapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT.
Sasa kama Katiba ilitungwa ili Watanzania tusikwame kwa kila kitu tunapoishi hapa nchini, halafu sasa kila kitu hovyo. Maana yake Mkuu wa nchi amekwama kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT.
Watanzania kila jimbo tuwatume Wabunge wetu waungane ili wapitishe Azimio la kumuondoa Rais Samia ili tusiteseke kama sasa.