Kwa bahati mbaya sikuona mapema comment yako ila kama utaruhusu tuingie kwenye mjadala juu unachokijua nami ninachokikua kuhusu Ngorongoro na Loliondo basi tuingie kwenye mjadala.
Ila wakati tunaingia kwenye mjadala naomba ujue kuwa Waziri alitoa GN Nom 421 mwaka 2022 ya kuongeza ukubwa wa pori tengefu la Loliondo, tangazo ili lilisababisha majeraha makubwa ikiwemo wakazi wa maeneo hayo kupigwa Risasi na kufa na wanyama wao kuuliwa! Serikali ikaenda kuweka bikon kwa mtutu wa bunduki.
View attachment 2758799
Wananchi walijipanga wakaenda kufungua kesi juu ya tangazo ilo la Waziri, J3 Ruling imetoka imesema tangazo la Waziri lilikiuka sheria na hivo batili.
View attachment 2758798
Pia naomba nikukumbushe kuwa katika eneo ilo sheria ya uhifadhi inawatambua wamasai kuwepo katika eneo la Loliondo na inatambua vijiji vilivyopo! Pia tambua kuwa Ardhi ni kiumma na iko mikononi mwa Rais kama mdhamini na sio mmiliki.
Tukisema tuende kisheria Serikali ina makosa sana juu ya kinachoendelea Loliondo na Ngorongoro na hatusemi hivi sababu ya Samia tu ila haya yalianza tangia enzi za Mwinyi na ndiyo maana mzee Mwinyi katika kitabu chake kiitwacho "Safari ya Maisha Yangu" Rais mstaafu Mzee Mwinyi alikiri kuwa alifanya makosa kuuza eneo la pori tengefu la Loliondo! Na hiki ndicho kimesabisha kutesa Wamasai mpaka leo.