Kama Mohammad Mwenyewe Alisema Kuwa Alitokewa na Shetani au Jini Pangoni, Kwa Nini Watu Wengine Walimlazimisha Aamini Alikutana na Malaika?

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Simulizi la awali la Muhammad kwa mkewe lilikiwa kwamba alipokuwa pangoni Hira, alitokewa na kiumbe wa ajabu ambaye aliamini alikuwa shetani au jini, huyo kiumbe alimwambia asome, akasema yeye hajui kusoma, yule kiumbe akaanza kumbana na kumwachia, akirudia tena na tena, akimlazimisha asome, na Muhamad akaendelea kumwambia kuwa yeye hajui kusoma.

Yule kiumbe akaendelea kumbana mpaka alipozidiwa nguvu. Alipotoka hapo akiwa na hofu, alifika kwa mkewe akamweleza yaliyomtokea pangoni, na kueleza kuwa alikuwa ametokewa na shetani au jini aliyembana na kumlazimisha kusoma. Muhamad alikuwa na hofu kubwa kiasi cha kutaka kujiua. Ndipo mkewe akampeleka Muhamad kwa binamu yake, aliyeitwa Waraqah, ambaye alikuwa mwanafunzi wa ukristo.

Huyo binamu yake aliyekuwa mwanafunzi wa Ukristo, alimwambia kuwa huyo aliyembana huko pangoni atakuwa alikuwa ni malaika, sawa na yule aliyemtokea Musa, hapo kale. Maelezo hayo yalimpooza Muhammad ambaye kabla yake, kutokana na hilo tukio, alifikia hatua ya kutaka kujiua. Baada ya maneno ya kumfariji, Muhammad akatoka hapo akisema ametokewa na malaika Jibril.

Lakini wataalam wa mambo ya kiimani wanaeleza kuwa tokeo la malaika huambatana na ujumbe wa faraja na siyo tishio, na pia malaika hajawahi kutokea kwa kumtesa mtu kama Muhamad alivyobanwa na huyo aliyemtokea, mpaka kiasi cha kuishiwa nguvu na kuingiwa na hofu kuwa alikuwa amepagawa na mapepo, hata akatamani kujiua.

Jambo la kujiuliza, kama mhusika mwenyewe alisema alikutana na jini au shetani, au alikuwa amepagawa na mapepo hivyo kuona vitu ambavyo havikuwepo, huyu binadamu yake ambaye hakuwepo huko pangoni, alikuwa na uhakika gani Muhammad alitokewa na Malaika Jibril, na siyo kama shuhuda alivyoamini kuwa alikuwa ametokewa na kubanwa na shetani au jini? Je, haiwezekani kuwa Waraqah alitafuta maneno ya kumpoza Muhamad asijiue kutokana na hofu aliyokuwa nayo, lakini hakumaanisha hicho alichomwambia? Kama huyo Allah angekuwa ni Mungu au angekuwa ni malaika, kwa nini huyo malaika asijitambulishe, mpaka aende akaambiwe na mtu ambaye hakuwa shuhuda wa tukio lenyewe?

'Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"

Fuatilia:

In Islamic tradition, the account of Muhammad in the Cave of Hira describes his first revelation from the Angel Gabriel (Jibril). However, some critical or external viewpoints interpret the intense, terrifying nature of this initial encounter as a possible demonic possession or deception by Satan.
Mohammad was told to read. Muhammad replied, "I cannot read." He was pressed tightly, and released, repeating this command and action three times until Muhammad felt exhausted.
then revealed the first verses of the Qur'an (Surah Al-'Alaq 96:1-5).

Muhammad was terrified by this experience, left the cave, and feared he might be possessed by a spirit or jinn. He told his wife Khadija to "cover him" and confessed his fear of being haunted.

Khadija consoled him and took him to her cousin, Waraqah ibn Nawfal, a Christian scholar who identified the entity as "Namus" (Gabriel), the same angel who visited Moses.
Some, particularly in non-Islamic or critical analyses, argue that the event fits descriptions of satanic influence rather than angelic visitation. These viewpoints are generally based on the following interpretations:
  • Fear and Distress: Critics argue that biblical angelic encounters usually begin with a calming message ("Fear not"), whereas this encounter left Muhammad in extreme terror and distress, which they argue is characteristic of a demonic, rather than angelic, experience.
  • Physical Coercion: The violent squeezing is cited by critics as evidence that the entity was not a divine messenger but a demon or jinn, which in Islamic tradition can sometimes take on deceptive forms.
  • Initial Doubts: The fact that Muhammad initially feared he was possessed or that the experience was from a devil is, for critics, evidence of the true nature of the event.
  • Suicidal Thoughts: Some narratives suggest that after the initial encounter, when the revelations ceased for a period, Muhammad was so distressed that he contemplated suicide before being reassured.
 
Kwani jini si ndio malaika huyo huy kiasili?
 
Dini, moja ya uraibu mbaya sana ukiuendekeza.
 
Sasa Jibril kumbe akikutokea anakutia kabali kwanza. Huyu Jibril siyo yule aliemtokea Maria mama wa Yesu kumpa ujumbe juu ya kuchaguliwa kwake kumzaa Masiah? Kama ndo yeye vipi hakumtia kabali Maria au ndo sababu alikuwa mwanamke😁😁😁Ila Yaan Jibril anajua kabisa jamaa (Muddy) hajui kusoma wala kuandika sasa kwanini amtie mwenzie roba kumlazimisha kusoma?! Ona sasa alitaka asababishe mchizi kujiua, angekaa kimya bila kusema kwa mke wake usikute wangemkuta kajitia kitanzi kama Yuda Eskariot😁😁😁😁Dini hizi bhana, yaan mtu unapewa ujumbe mzito kwa watu na bado wanatumia nguvu kwa kukukaba roba hadi unazima😅
 
Alaf akatohoa jina la malaika waliokuwa wanamuita Waesrael, yeye miaka 600 mbele akajidai alimtokea pia. Kwa kutag ubavu wa mjomba wake Waraq.

Pengine wanamsingizia Waraq.

Yaan bila Waraq kusingekuwa na ujinga huu.
 
😁😁😁,
Uislam unawashuhulisha kuliko dini yenu yenye maajabu tele ambayo mungeanza kutafakari kwenu kwanza
1. Mungu kazaa mtoto.
2. Balada ya kuabudu na kumsifu MUNGU mnamuabudu mtoto wake.
3. Mungu Yesu anaadhibiwa na viumbe wake na kupigwa misumari bila huruma.
Etc 😁😁😁😁😁
 
Muhamadi alipokutana na Mkewe Hadija baada ya kutoka kule Pangoni na kuulizwa na mkewe kuwa;
"Nini kimekutokea kule Pangoni"?
Muhamadi alijibu hivi;
"Nahisi kuzugwa na mashetani na kunichezea akili yangu"
(Maisha ya Mtume na wakeze, by Shehe Farsy)

Muhamadi kwa kinywa chake alikiri kuwa alitokewa na mashetani kule Pangoni:

Hiyo habari ya Waraga Bin Naufari (alikuwa Padre Mkatoriki mpiga ramli, yaani mganga wa kienyeji wa kuagua akitumia majini)
haina mantiki kwakuwa hakuwepo kule Pangoni:
Leo hii kuna miji wakisikia sauti ya Allahu Akbarii wanatimua mbio kuokoa maisha yao:
Aya hizi hapa
1)
4:79 - Jema lilio kufikia limetokana na Mwenyezi Mungu. Na ovu lilio kusibu linatokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha.
2)
2:97 - Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

ndio maana mwisho wa siku Majini wenye dini yao wakajitokeza na kusema wao ni Waislamu (Sura ya Majini 72,) na ndio waliomtokea na kumkaba kule Pangoni:

Je, tuamini maneno ya Muhamadi au ya Walaga?
 
Back
Top Bottom