Kama mtu akifa anaenda mbinguni kwanini watu wanaogopa kifo, kwanini wanalia, je kwenda mbinguni ni jambo baya sana ?

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
3,558
Reaction score
7,935
Naomba niwape elimu, nini maana ya kifo?

Kifo maana yake ni kutokuwepo kwa maisha kwa mtu na tukisema kuzaliwa maana yake ni kuwepo kwa maisha kwa mtu, hivyo kwasababu hakuwepo akazaliwa yani akapata maisha akifa inamaana ameyapoteza maisha hayo sasa ni vipi mtu huyo aende mbinguni?

Kumekuwa na dhana kuwa mtu akifa anaenda mbinguni, hakuna uthibitisho wa hilo suala, kitu tunachokijua ni kwamba kuna kupata maisha "kuzaliwa" na kupoteza maisha "kufa" hakuna kitu kingine dhana hii inaushahidi hata tukienda kufukua makaburi miili ya walio kufa bado ipo kaburini na imeharibika.

Inamaana mda wote mtu akifa anabaki kaburini akiharibika na sio anaenda mbinguni huwezi kwenda mbinguni ikiwa hauna "uhai" hauna "maisha" kwani mbinguni ni sehemu ya wafu au walio hai ? jibu ni kwa walio hai.

Vitabu vya dini Quran na biblia vinathibitisha kuwa mungu atakuja duniani na atafufua watu wake kwanza ndio aendenao mbinguni wakiwa hai, atawafufua na miili yao iliyo haribika na kurudi kuwa wazima tena hato chukua maiti. sasa jiulize huku kufa kwa maiti kisha iende mbinguni inamaana mbinguni ni wafu, ni vipi utaenda mbinguni wakati umekufa ?

Je kuna kunyakuliwa kiroho bila mwili mtu akifa kwenda mbinguni? hili ni swali la msingi sana.

Kwanza tuangalie vitabu vya dini maarufu vinasemaje kuhusu hili, vitabu vya dini vikubwa kama Quran na biblia vinasema mungu atakuja kufufua wafu kisha watenda mbinguni inamaana hiii dhana ya kunyakuwa mtu kiroho akifa sio ya kweli labda naomba nifafanue.

Wanadamu au binadamu maana yake ni viumbe vilivyoumbwa duniani na wanasifa za kuwa na mwili wa nyama hii inaushahidi wa kiuhalisia katika uhalisia mwanadamu ni mwili bila mwili yeye hawezi kuishi, ndio maana vitabu vya dini vinasema wafu watafufuliwa yani watarudishwa miili yao kwanza.

Kwahiyo hatuwezi kusema mtu atoke kiroho aende mbinguni alafu tuseme yeye bado ni mwanadamu, hapana mwanadamu ni kiumbe wa mwili na nyama, hivyo ni kitu kisichowezekana au kueleweka wala hakina ushahidi wowote.

Mfano uislam wanasema mtu akifa anaenda mbinguni ingali mwili wake bado upo kaburini na wanasema anaenda mbinguni kupewa bikra sabini na mbili sasa atapewaje bikra sabini na mbili wakati hana mwili hana mikono hana sehemu za siri, hana mishipa ya hisia mwili wake upo duniani kaburini bado na amesha kufa wala hayupo hai tena.

Na kuna baadhi ya dini za kikristo pia yanadai mtu akifa anenda mbinguni huwezi kwenda mbinguni ikiwa umekufa, mfano yesu alikufa lakini hakuenda mbinguni akiwa amekufa bali alifufuka kwanza na kwenda mbinguni, huu ni ushahidi wenye nguvu kuwa huwezi kwenda mbinguni ukiwa umekufa au huwezi kwenda mbinguni ikiwa mwili wako bado upo kaburini unaharibika na kuoza, ili mtu aende mbinguni lazima hawe hai kwanza.

Asante sana!
 
Naomba niwape elimu, nini maana ya kifo?

Kifo maana yake ni kutokuwepo kwa maisha kwa mtu na tukisema kuzaliwa maana yake ni kuwepo kwa maisha kwa mtu, hivyo kwasababu hakuwepo akazaliwa yani akapata maisha akifa inamaana ameyapoteza maisha hayo sasa ni vipi mtu huyo aende mbinguni?

Kumekuwa na dhana kuwa mtu akifa anaenda mbinguni, hakuna uthibitisho wa hilo suala, kitu tunachokijua ni kwamba kuna kupata maisha "kuzaliwa" na kupoteza maisha "kufa" hakuna kitu kingine dhana hii inaushahidi hata tukienda kufukua makaburi miili ya walio kufa bado ipo kaburini na imeharibika.

Inamaana mda wote mtu akifa anabaki kaburini akiharibika na sio anaenda mbinguni huwezi kwenda mbinguni ikiwa hauna "uhai" hauna "maisha" kwani mbinguni ni sehemu ya wafu au walio hai ? jibu ni kwa walio hai.

Vitabu vya dini Quran na biblia vinathibitisha kuwa mungu atakuja duniani na atafufua watu wake kwanza ndio aendenao mbinguni wakiwa hai, atawafufua na miili yao iliyo haribika na kurudi kuwa wazima tena hato chukua maiti. sasa jiulize huku kufa kwa maiti kisha iende mbinguni inamaana mbinguni ni wafu, ni vipi utaenda mbinguni wakati umekufa ?

Je kuna kunyakuliwa kiroho bila mwili mtu akifa kwenda mbinguni? hili ni swali la msingi sana.

Kwanza tuangalie vitabu vya dini maarufu vinasemaje kuhusu hili, vitabu vya dini vikubwa kama Quran na biblia vinasema mungu atakuja kufufua wafu kisha watenda mbinguni inamaana hiii dhana ya kunyakuwa mtu kiroho akifa sio ya kweli labda naomba nifafanue.

Wanadamu au binadamu maana yake ni viumbe vilivyoumbwa duniani na wanasifa za kuwa na mwili wa nyama hii inaushahidi wa kiuhalisia katika uhalisia mwanadamu ni mwili bila mwili yeye hawezi kuishi, ndio maana vitabu vya dini vinasema wafu watafufuliwa yani watarudishwa miili yao kwanza.

Kwahiyo hatuwezi kusema mtu atoke kiroho aende mbinguni alafu tuseme yeye bado ni mwanadamu, hapana mwanadamu ni kiumbe wa mwili na nyama, hivyo ni kitu kisichowezekana au kueleweka wala hakina ushahidi wowote.

Mfano uislam wanasema mtu akifa anaenda mbinguni ingali mwili wake bado upo kaburini na wanasema anaenda mbinguni kupewa bikra sabini na mbili sasa atapewaje bikra sabini na mbili wakati hata mwili hana mikono mwili wake upo duniani kaburini bado na amesha kufa wala hayupo hai tena.

Na kuna baadhi ya dini za kikristo pia yanadai mtu akifa anenda mbinguni huwezi kwenda mbinguni ikiwa umekufa, mfano yesu alikufa lakini hakuenda mbinguni akiwa amekufa bali alifufuka kwanza na kwenda mbinguni, huu ni ushahidi wenye nguvu kuwa huwezi kwenda mbinguni ukiwa umekufa au huwezi kwenda mbinguni ikiwa mwili wako bado upo kaburini unaharibika na kuoza, ili mtu aende mbinguni lazima hawe hai kwanza.

Asante sana!
Wafia dini ni mbumbumbu, sijui kama watakuelewa.
 
Kuna makabila yanaogopa kutahiriwa kwa hofu ya maumivu itakuwa kufa?

Halafu tunaoogopa ni sisi wenye makando kando mengi, unaogopa hivi ninakoenda nitasalimika kweli? Kwanini Mafwele asiogope? Ila wale wanaoishi maisha safi mbona huwa wanakufa huku wakitabasamu? Tushawaona sana.
 
suala la namna ya kufa au maumivu yake inategemea na aina ya kifo chako kama ukipigwa shoka au panga nazani unajua maumivu yake ni nini
 
Kinachokufa ni mwili, sio roho. According to Bible miili hii ya duniani itaishia duniani then mbinguni Kuna miili mingine.
Hayo maneno sio ya biblia nime toa mifano kwanini yesu hakuacha mwili alifufuka kwanza kisha akaenda mbinguni unataka kuniambia kama mbinguni kuna mwili mwengine inamaana yesu watakuwa wawili mbinguni hebu fungua akili kidogo.

hayo maneno kwenye biblia hakuna mimi biblia naijua vizuri ni uongo, hebu pia nikuongezee mfano wa yesu kurudi mara ya pili kwenye ufunuo wa yohana anasema atafufua watu, kwanza kisha watavikwa mavazi meupe kisha ndio safari mbinguni.

jiulize kama kuna mwili mwengine mbinguni yesu anakuja kufufua watu wa kazi gani ?
 
Tukubali tuu hatujui, wafia dini wake take advantage ya kutokuelewa kwetu, maana issue zao zote ni mbingu, moto, ahera etc yaani vitu ambavyo hata wao hawajui
 
Kumekuwa na dhana kuwa mtu akifa anaenda mbinguni, hakuna uthibitisho wa hilo suala, kitu tunachokijua ni kwamba kuna
Kwa sababu hakuna uthibitisho kuwa wakifa wataenda mbinguni, Mbona unauliza swali na jibu unatoa mwenyewe?
 
Kazi kweli kweli, nimesema hakuna uthibitisho wa mtu akifa kwenda mbinguni na sio sina uthibitisho mtu akifa haendi mbinguni nimetoa mifano ya mabaki ya maiti kwenye makaburi umeelewa?
 
Anaye ogopa kifo na asiye ogopa mwisho wote watakufa tu.

Kuhusu kwenda mbinguni, wote tutaenda ila huko zipo pande mbili na kila mmoja atakwenda upande anao stahili kutokana na matendo yake hapa duniani.
 
Kufa si safari ya harusi,, ni kuachana na familia, ndoto, na maisha. Even believers cry not because they doubt heaven, but because love hurts when it’s left behind.
 
Back
Top Bottom