Kama mtu akifa anaenda mbinguni kwanini watu wanaogopa kifo, kwanini wanalia, je kwenda mbinguni ni jambo baya sana ?

Jambo la kulia ni uhamuzi wa wa mtu.
Japo kulia kunatokana na yule mtu mlikuwa naye vipi?
 
Wewe kama kuoga maji kunafanya uwe safi, kwanini unaona shida kuoga maji baridi ukiwa Njombe?
 
Wengi huogopa kwasababu ya hofu wasioijua, hofu ya kupoteza na kutokuwa na uhakika wa kuona na kutenda vile alivyozoea kuona au kutenda...
 
Nani kakuambia mtu akifa anaenda mbinguni ? .....labda useme wachamungu watakatifu ndiyo wameelezwa kuwa watakwenda mbinguni kwa wakati uliokubalika....pia vilio vipo vya sababu mbali mbali ...nabii elisha alilia alipo muona nabii elia akichukuliwa kwenda mbinguni.
 
Hujawai kusikia watu wenye imani za mtu akifa anaenda mbinguni?
 
Uelewa wako wa masuala ya kiroho ni finyu. Mtu ana sehemu tatu. Roho, Nafsi na Mwili. Sasa mtazamo wako ni wa kimwili tu.
 
Hujawai kusikia watu wenye imani za mtu akifa anaenda mbinguni?
Imani zilizo potoshwa hizo ni sawa na wakristo wanavyo potosha kuwa yesu alienda kuzimu baada ya kufa na kutoka kuzimu siku ya 3 kwa kufufukq ...huu ni uongo hakuna kitu kama hicho kwenye injili ....tatizo wakristo awajui kuzimu ni wapi?
 
Ushawahi kufiwa?
 
Uelewa wako wa masuala ya kiroho ni finyu. Mtu ana sehemu tatu. Roho, Nafsi na Mwili. Sasa mtazamo wako ni wa kimwili tu.
kwahiyo mtu akifa anaenda mbinguni? mfano wangu wakimwili wakati nimegusia vitabu vya kidini tayari hivyo vitabu vya kidini sio vitabu vya kiroho ? inasikitisha sana mbumbumbu anamuita mwelevu hajui pengine hujui unachotaka kukijenga niongelee masuala ya kidini alafu nisiwe nimegusa mambo ya kiimani kweli?
 
Baada ya kifo maisha huendelea tunacho badilika ni maumbile tu. Hushangai mtu akifa mwili huoza na kutoa wadudu (viumbe hai) hao wadudu ni wewe, tena ni chakula cha viumbe wengine, ni mzunguko kama mchezo wa kombolela-we are not perish
 
duuh, asante sana kwa mchango wako inamaana mwanadamu akifa anabadilika anakuwa wadudu ?
 
Kuzaliwa ni kuletwa duniani na kufa ni kuondoka duniani .

Au hilo pia linahitaji maombi kujuwa?
unaweza kuletwa duniani wakati tayari mavumbi yaliyokuunda yapo ??

unawezaje kuondoa duniani ikiwa mwili wako upo kaburini ?

Kisayansi na hata kidini hakuna kitu kama hicho hata kidini wanasema binadamu ni sehemu ya mavumbi ya ardhi, kwahiyo kufa nikuondoka duniani au kupoteza uhai ? kazi kweli kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…