Kama mtu anakopa benki 5 tofauti za Tanzania na akaweza kukimbia nchi bila kugundulika ni ishara kwamba TISS na vyombo vingine vimelala

Umempa elimu nzuri. Hapa tatizo liko benki alizokopa. Mbona sisi watu wa kawaida kukopa benki ni mlolongo wenye vielelezo vingi sana mpaka size ya sehemu nyeti wanakuuliza?
 
Ingekuwa kuwafuatilia CHADEMA hapo ndo ungeona maajabu ya TISD
 
Watanzania tusiwe mazuzu hivyo kila kinachosemwa tunameza bila tafakari. Kuna Interpol ambayo mwalifu atarudishwa kujibu mashtaka popote alipo kati ya nchi 194 zilizo wanachama!!
Wewe ndo zuzu. Kukopa hela ni uhalifu? Interpol wanaendaje kumkamata mtu kisa mnamdai mtu hela ambayo mlimpa kwa makubaliano? Tafuteni njia mmalizane nae.
 
I'm with you uko right.

Kwahiyo (kwa mfano wako wa Singasinga) ndo maana nasema huenda sasa imelala, hivyo mambo kama hilo la mtu kutokomea kusikojulikana ni ishara hizo kuwa wamelala.

Wakati wa yule mzee, walikuwa wamekumbushwa wajibu wapo na wakawa macho na mambo mengi yakawa yavumbuliwa.

Hata mimi nina mfano hai, kuna siku nilitua TZ (wakati wa utawala wa JPM) na hapohapo nikaona jamaa amebanwa aeleze amepataje pasi ya kusafiria ya TZ aliyo nayo ilhali yeye ni Mnigeria.

Hiyo yaonyesha jamaa wa uhamiaji aliwaita mazee washughulike na jamaa ili wapate kutambua kama kuna gorgery au la.

Jamaa walikuwa wapo macho na wanafanya kazi pale ambayo ni moja ya kazi muhimu sana kuangalia mgeni anaeingia nchini.

Kwahiyo ni kuwakumbusha tu kwamba kulala kwaweza kuleta maafa mengine makubwa kuliko hayo ya mamikopo.
 
Waache walale tu wTu walambe 🍯🍯🍯
 
Kabisa mkuu

Wa juu akiwa lege lege, tutavilaumu taasisi nyingine zimefeli kumbe kiongozi wa juu.

Mfano mwingine Mwakyembe ana majina ya wakurugenzi wa mashoga, unataka kusema serikali nimeshindwa kutambua hadi atambue Mwakyembe?
 
Kama ni hivyo kwanini mkuu wa nchi aliongelee ikiwa kila kitu chajulikana?

Atupa faida gani?
Ngoja nikupe mfano, aliyewahi Kuwa DG TISS Dr. H.K aliwahi danganya kuwa mkewe anaumwa uingereza na bill zikawa zinakwenda lakini jasusi junior BCM akia ikulu akang'amua kuwa mke wa bosi wake Si mgonjwa bali yupo Canada anapiga buku kipindi hicho balozi wa tz huko alikuwa BWM hivyo Hela zinazotumwa huko zinaliwa, BCM akamtonya Rais kipind hicho mwl JK Nyerere.

Sasa mwl Akala bati mara muda mfupi DG TISS Dr. HK akanunua Benz new model ndipo Nyerere akamwita na kumhoji mwisho akamfuta kazi baadae Dr HK akamfuata BCM na kumwambia wewe ndo umechomoa betri hivyo ama zako ama ZANGU dogo BCM akarudi Kwa Rais na kumwambia Kuwa katishiwa na mbobezi JK akamwita Dr. HK na kumwambia ole Wako nisikie KIJANA kang'atwa na nyigu nitakunyonga hadharani ndipo Hali ikatulia hivyo Rais kudanganywa na Hawa wajomba hasa usalama ni kawaida sana
 
Na walipatana baadae maana walikuwa wakinywa moja moto moja baridi pale Palm Beach Hotel na BWM alipapenda sana pale.

Kazi kwelikweli.
 
Wenye power ndo wanafanya hayo.
 
Hilo genge la huyo Khan ni kubwa sana na limetapakaa Afrika nzima.
 
Ni kwasababu Putin ni mtaalam wa "Counter Espionage" hivyo ni lazima mifano iwe dhahiri.

Wanafunzi wake hawawezi kukosea hata kidogo wakikudaka huwa ni asilimia 101 una kosa.

Au vipi mkuu 🙂🙂
Wewe umejuaje mkuu????? Kwa kusoma kwenye mitandao????????? Mbona hawakumdaka Boriss yelstin na mpunga aliokomba benki kuu ya urusi miaka ile??
 
Dogo umeongea kwa dhiaka kuhusu TISS ila be wise,usitukane mamba wakati mto ungalipo..Be wise hii platform ya JF ni ya mpito na kuna leo na kesho.
 
Wewe umejuaje mkuu????? Kwa kusoma kwenye mitandao????????? Mbona hawakumdaka Boriss yelstin na mpunga aliokomba benki kuu ya urusi miaka ile??
Mimi nimesoma vyuo mbalimbali sio mitandaoni.

Nimefanya case studies na dissertation ya mambo hayahaya.

Hivyo nafahamu nnachokiongea.
 
Ila hujaingia frontline kudhibitisha ubora wao.
No kufanya analysis kwatosha kusaidia shughuli zozote muhimu kwa taifa.

Wachambuzi huwa hawaingii frontline wapo nyuma wakisaidia kwa info, data na uchambuzi wa adui amekaaje, ana nini yuko vipi kivifaa anajeshi kiasi gani, atumia mbinu zipi na kadhalika.

Ila ni kazi very risky.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…