Kama mtu anakopa benki 5 tofauti za Tanzania na akaweza kukimbia nchi bila kugundulika ni ishara kwamba TISS na vyombo vingine vimelala

Mnakuja na theorise za kiajabuajabu wakati mama kaweka very clear, kuwa game ni ya wafanyakazi wa mabenki. Nini ambacho hamjakielewa kwenye kukopa?
 
Ila uyu kaishayakanyaga izo pesa atazilipa
 
Tiss wajishughulishe na mikopo? Hili mbona ni kosa la benki? Benki inakopeshaje mtu ambaye haimjui? Dhamana anazoweka kwanini hawazihakiki? Huu ni mchongo wa benki na TISS unawaonea bure. Hujui hata inavyofanya kazi pengine.
Mkuu labda humjui mleta mada. Jamaa ni Tiss tena wa muda mrefu.
 
Hao wanaopaswa kufanya maamuzi ndio wanapaswa wajikague tena.
 
TISS kwani wapo tena? sio kwamba nao walifutwa baada ya kuonekana hawana tija kwa Taifa?
Wangekuwepo haya ya ushoga yasingekuwawepo kwa kaisi hiki na pia uteuzi wa viongozi hadi wenye matatizo ya akili!
 
Tatizo na changamoto kubwa ni TISS kutumika kisiasa za ndani tu badala pia ya kiuchumi na kiutamaduni dhidi ya mataifa ya kigeni kwa maslahi mapana ya kitaifa.
Mabadiliko ya fikra, kutoka kwenye mapambano ya ndani kwenda kimataifa yanahitajika .
 
Mkuu huyo Nolle Prosequl ni mke alipewa?
Hapana mkuuπŸ™‚

Hilo ni neno la kilatini (likimaanisha kutokuwa tayari kuendelea na mashtaka) la kisheria ni ile "notice" ambayo mwendesha mashitaka hutoa kufuta mashitaka dhidi ya mshtakiwa ama yote au sehemu yake.
 
Mnakuja na theorise za kiajabuajabu wakati mama kaweka very clear, kuwa game ni ya wafanyakazi wa mabenki. Nini ambacho hamjakielewa kwenye kukopa?
Hao wafanyakazi wapo nchi gani si hapahapa
 
Kuna mambo mengine tunayajadili kiujumla sana na kuvitwisha mzigo vyombo vya usalama bila mantiki. Mtu kakopa huko benki na kakutana na Meneja mikopo na DG wa benki kaidhinisha, TISS, Polisi au FIU wanahusikaje?

Hivyo vyombo vya usalama vinahusika na mikopo benki? Nilidhani hoja ingekuwa ma CEO wa benki husika wakamatwe na chain yote iliyoidhinisha mikopo. Pili, Interpol kama walipewa taarifa ya jinai walipaswa kutuma warrant mtuhumiwa arejeshwe.

Kukiwa na hoja lazima tufikiri kabla ya kunyooshea vidole taasisi zetu pendwa. Mimi na wewe na wageni wanafurahia nchi yenye usalama wa hali ya juu ni TISS. Uhuru na mipaka yetu iko salama ni JWTZ. Usalama wa raia uko juu ni Polisi. πŸ™πŸ™πŸ™
 
Mkuu, raisi Samia kasema mwizi kakopa pesa benki kwa kutumia dhamana za kughushi na kakimbia nchi, hIyo ni kauli ya raisi mwenyewe na ipo tafuta uisikilize.

Sasa raisi akija na kauli kama hiyo yamaanisha nini?

Yaani benki zilipogundua mtu kachukua mkopo benki 5 au 6 tofauti na kasepa na pengine polisi wamejulishwa, uhamiaji pale uwanja wa ndege na idara zingine wewe wafikiriaje?

Kitendo cha raisi kuja na kauli kama hiyo yaonyesha wazi kuna tatizo katika mfumo mzima kuanzia benki kwenyewe hadi kwa wale ambao wana wajibu wa kuhakikisha mtu anakamatwa.

Mbona huko nyuma watu wamekamatwa JNIA wakitaka kupanda ndege?
 
Usisingiz TISS kwenye mambo ya mkopo , Hizo ni terms tuu za mkopeshaji ndio zinamapungufu
 
Yaani taarifa yoyote inayotoka kwa Mhe. Rais wala haihojiwi. Ni sahihi kwa asilimia 100. Rais ni mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu. Ila hakuna sehemu Mhe. Rais amekisema hiki kilichoandikwa hapa kutuhumu TISS na Polisi.

Nikasema; hii mikopo ni taratibu za kibenki. Mikopo mikubwa kama hii naamini hadi bodi zinajua. Sasa kusema kila mkopo taasisi za usalama zijue huko ni kuwaonea. Kuhusu hoja mtuhumiwa alipitaje airport au border yoyote ya nchi inategemea taarifa zilitolewa muda gani?

Kama tukio hadi kabaini CAG usikute ma CEO wa benki walikuwa wanapambana kimya kimya. Naamini kabisa kutoka rohoni vyombo vya usalama visingeshindwa kuzuia hata ndege kama ilianza kupaa.

Nina imani kubwa mno na vyombo vyetu pendwa vya usalama. Nchi hii iko vizuri jamanii. Hapa ni watu wa benki wanapaswa kukamatwa tu. Benki kuna michezo mingi ya money loundering. πŸ™πŸ™πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…