Kama mtu anakopa benki 5 tofauti za Tanzania na akaweza kukimbia nchi bila kugundulika ni ishara kwamba TISS na vyombo vingine vimelala

Mkuu, kusema wamelala ni lugha inomaanisha kuwa wawe tayari masaa 24.

Ni kweli vyombo vyetu vimekuwa macho masaa 24 hilo halina ubishi kabisa.

Lakini kauli ya raisi yamaanisha kwamba huyo mwizi hayupo nchini.

Na kama hayupo nchini amepitapita vipi hadi kutoroka?
 
Nimereply juu. Ume establish taarifa kwa vyombo vya usalama zilitolewa muda gani baada ya huyo bilionea kukopa na kuondoka nchini? Taarifa zingetolewa mapema asingefika hata Vingunguti pepsi angetiwa mbaroni. Mabenki ndani ipo syndicate ya baadhi ya wahalifu. 🙏🙏🙏
 
Mkuu, kauli ya raisi kwamba mwizi kakopa benki tano au sita tofauti kwa kutumia fake documents na kakimbia nje weye waielewaje?

Mimi nimezungumzia kauli ya raisi na ndo msingi wa mada yangu kwamba ikiwa raisi kakiri kuwa huyo mwizi amekimbia nchi hilo ni tatizo.

Auweye umemwelewavipi raisi Samia?
 
Amna hiyo ina security ya serikal ndo maana analalamika
 
Huyo kaja kaa mwekezaji
 
Mimi sitaki kuilaumu Tiss nawalaumu watawala je Tiss imewezeswa kwa kiasi gani?
Je Tiss ni idara ya nani ikiwa Rais anaweza pangua na kuweka mtu wake? What If akiweka mtu wakupiga naye nani atatoa hiyo taarifa?
Sheria zetu zipoje maana tusilaumu chombo tukasahau Kuna mfumo unao ruhusu haya.
Tiss yetu hakuna asie jua ina hitaji a big reforming iwe idara isio ingiliwa na siasa na ndipo tutaona maajabu.
 
Hivyo vyombo unavovishangaa ni vya kabatani ama?
Kama ni vile vya ulinzi na Usalama TZ asee... Vipo kwa ajili ya kuthibiti upinzani! Huyo mkopaji angekuwa upinzani wangemdaka kabla hata ajakopa benki ya kwanza!
 
Sikiliza bhana, mimi siwezi kutaja taja mamlaka ya Mhe. Rais naiheshimu kwa kiwango cha juu. Nimekueleza naona unataja taja tu mamlaka kuu ya nchi. Nimekuuliza ni wapi Mhe. Rais alizotaja hizo taasisi? Mhe. Rais kazungumzia benki kumkopesha mtu kwa docs fake na akawatoro hao benki. Huo ni udhaifu wa kibenki siyo vyombo vya usalama. Usiviingize na kutaja taja mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu. Msikilize vizuri utaelewa. 🙏🙏🙏
 
Mkuu, please stop being condescending, yaani kuwa na tabia ya kuonyesha ubabe au kutoa vitisho hiyo naamini huna.

Na hii tabia mara nyingi sisi waafrika ndiyo tabia yetu sisi.

Nimemsikiliza uzuri tu na nimerudia hiyo sehemu (dak ya 33) nimechambua na nimeweka analysis yangu.

Nawe una uwezo huo kutumia akili yako kuchambua hotuba ya mheshimiwa raisi Samia na kuja na hitimisho lako, hivyo ndivyo mambo huwa.

Na katika mada utangulizi wangu umeanza uzuri kwa kumtaja kwa heshima raisi wetu.

Pia kutajwa mamlaka ya juu ni kitu cha kawaida sana kisikutishe.

Mradi mtu havunji sheria.

Kama waona washindwa kuweka "counter argument" kimantiki basi wacha na pita, huja haja ya kuzogoa.
 
Serikali itawakamata tu maana ina mkono mrefu, hivyo namna ya kuwafuatilia itafuatwa na kukamatwa warudishe hela wazokopa na waliowasaidia nao washughulikiwe.
 
Serikali itawakamata tu maana ina mkono mrefu, hivyo namna ya kuwafuatilia itafuatwa na kukamatwa warudishe hela wazokopa na waliowasaidia nao washughulikiwe.
Na wakikamatwa watangazwe kwa watanzania ili tuelewe kwamba vyombo vyetu vimefanya kazi yao.
 
Wewe huwezi kuwa na kuhakikishia. Usitishie watu ubwana shamba wako eti wewe Tiss. Labda ungekuwa chizi flan hivi.
Kwani kuwa TISS ndiyo nini? Mbona una inferiority complex mbaya sana? Nyie ndiye matapeli wanawatishia kuwa wao ni TISS mnaishia kuwapa fedha. Hao ni binadamu kama wengine tu na hawana cha ziada.
 
Kwani kuwa TISS ndiyo nini? Mbona una inferiority complex mbaya sana? Nyie ndiye matapeli wanawatishia kuwa wao ni TISS mnaishia kuwapa fedha. Hao ni binadamu kama wengine tu na hawana cha ziada.
Wewe siyo TISS. Tulia wewee
 
Sijui kigezo ya teuzi au ni shule gani wanaopitia!!
Wanadhani kazi yao kubwa ni kuandamana na Rais kuweka Usalama na Kwa Marais wanaokuja tu! KaI ya Hawa watu ni pana Kwa Taifa wanaotakiwa kujiongeza sana kila kona ya nchi.
Uhamiaji pale Kurasini Kuna kila namba ya Rushwa na ucheleweshaji wa huduma nyingi zinafanyika kwenye zile maduka na migahawa iliyopo mbele ya zile ofisi.
Ni Kwa Nini pakawekwa maduka pale mahali muhimu vile.

Ni wakati muafaka Serikali na Jiji Biashara kuhakikisha hakuna kuweka biashara kwenye maeneo muhimu ya ofisi za Serikali na uwe kama Ilivyo eneo la Uwanja wa ndege.
Sivyo basi na waweke biashara pale kwenye Kituo cha Polisi.
Biashara kwenye malls, Kariakoo mlimani city nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…