Kama mtu anakopa benki 5 tofauti za Tanzania na akaweza kukimbia nchi bila kugundulika ni ishara kwamba TISS na vyombo vingine vimelala

Jana, raisi wa Jamhuri ya ya Muungano na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama Tanzania kaeleza kwamba kuna mtu amekopa benk 5 au 6 tofauti za Tanzania na hajulikani alipo, yaani amekimbia na kutoka nchini.

Sasa huu ni mtihani kwa TISS, vyombo vya fedha, uhamiaji na wizara ya mambo ya ndani kwa ujumla.

Haiwezekani mtu mmoja akafanya jambo hilo zito na asepe kilaini hivyo hiyo ni ishara tosha kwamba idara yetu ya usalama na vyombo vingine vimelala au vimejiruhusu kupwaya kupita kiasi.

Lakini mimi ntaikosoa zaidi idara ya usalama kwani yenyewe ndio yaweza kuchagiza shughuli zote za ulinzi na usalama wa nchi.

Natambua idara hii ina uwezo mkubwa tu ina maofisa mahiri tu ambao wamepata mafunzo ndani na nje ya nchi hivyo wana ueledi, umahiri, uerevu na kila aina ya mbinu za kimkakati na kimedani kuhakikisha nchi yetu ipo salama.

Leo hii shirika la ujasusi wa ndani la Russia la FSB limetangaza kumshikilia mwandishi wa jarida la Wall Street Journal kwa madai ya kujihusisha na ujasusi wa ndani yaani kwa kiingereza twasema "Espionage".

Hiyo ni kazi ya majasusi wa ndani ya Russia yaani "Counter Espionage Agents" ambao wapo macho masaa 24 kulinda nchi, mali zake au "Assets" na miundombinu yake na wananchi kwa ujumla.

Sasa ni wakati wa idara yetu ya usalama wa Taifa kujipambanua kumtafuta huyu mwizi wa fedha zetu ambazo zimehifadhiwa kwenye mabenki zikiwa ni akaunti za watu na mitaji pia. Ni wakati wa kushirikiana na vyombo ya ulinzi na usalama vya nchi jirani na pia ni wakati wa kumtambua mtu huyo ambae ni wazi atakuwa alikuwa na pasi ya kusafiria, makabrasha mbalimbali yanoonyesha anuani zake na kadhalika hata kama ni "fake documents".

Kuhusu mabenki yetu nina imani kwa wana taratibu zote kali ambazo ni lazima mkopaji azifuate na kwenye hili ni lazima iwe ni "inside job" wafanyakazi walohusika ni lazima wapatikane kabla ya Jumaa.

Niliwahi kutoa mapendekezo huko nyuma kuhusu kuifanyia mabadiliko idara ya usalama wa taifa Mapendekezo: Serikali ipitie upya Sheria ya Usalama wa Taifa na TISS iundwe upya kwa maslahi ya taifa na nikzaeleza kwa upana wake.

Pia niliwahi kueleza kwamba wapo watu watembea na wallet tu Mtu anaesafiri kwenda nje kila siku lakini anabeba wallet na passport tu, utamfikiriaje? na hawa huenda ni wale ambao huenda sehemu kufanya machafuko kama uporaji fedha katika taasisi za fedha bila kugundulika na hii ni hatari kwa taifa.

Na pia nikawahi kutoa wazo kama nchi yetu ipo tayari kwa vita vya kijasusi wa uchumi katika mada hii Ujasusi wa Kiuchumi na Kiteknolojia unakuwa kwa kasi, Je Tanzania iko tayari ambapo yawezekana kabisa huyu mtu aliefanya wizi huu wa kughushi ni wale akina Carlos Jackal ambae alikuwa na uwezo wa kuingia katika nchi yoyote na kumaliza kazi kisha kujiondokea asijulikane.

Carlos alikuwa ni jasusi ambae alifunzwa kulelewa na kuwa alipwa ujira na idara ya kijasusi ya Russia ya wakati huo KGB na kazi zake hazikuwa na mfano.

Lakini mtu huyu ambae amehusika na wizi wa mabilioni ya shilingi si wa aina ya Carlos Jackal lakini aweza kuwa ni mhalifu wa kimataifa na huenda akarudi tena.

Hivyo Idara yetu ya TISS iamke isijisahau kwani majukumu yake si ya kisiasa bali ni ulinzi madhubuti wa nchi yetu vikiwemo vyombo vyetu vya fedha ambavyo kwa kushirikiana na vyombo vingine kama Uhamaji na hata huko nje Interpol tayari mtu huyu angekuwa yupo kwenye "Wanted List".
Ni kwamba regulator wa mabenki, BOT, hana uwezo wa ku-monitor loans hizo? Mtu akikopa, au kabla ya kukopa basi jina lake lisomeke moja kwa moja BOT, akitaka kukopa benki nyingine tena BOT watoe alert kwa hiyo Benki nyingine, kwa Siri. Pia iwe na idara ya kuchunguza loans na dhamana zake.
 
Na hapo ndipo tunakosea.

Regulator hutakiwa kuwa huru yaani masuala yote ya kibenki ikiwemo BOT wanakuwa wako chini ya uangalizi wa Independent Financial Regulator ambae akigundua umefanya upuuzi akuchapa faini.

Hivyo benki zilizokwapuliwa hizo fedha zinawajibika kwa kutoa maelezo IFR na kisha kuangalia wapi wamekosea na hupigwa faini, ili wasirudie makosa kama hayo.
 
Mkuu, weye puuzia tu hakuna haja ya kutoa vitisho, "after all" huu ni mjadala tu aukuumuzi weye wala yule ila una faida na wengine hapa wapata kitu fulani.

Kuna mambpo yafanyika katika nchi yanaudhi hivyo tegemea response yoyote ile.

Ndiyo huru huo wa kuongea - We dare to talk openly.
Issue sio mimi,bali kauli za kuitukana TISS waga zina matokeo yake.ID fake haikufichi usijulikane.
 
Sasa huko ni kutishana ingawa mimi wakija hao TISS hapa Kibaigwa watafahamu waongea na nani na ntawapa chai ya mkandaa au kahawa na kashata na ntawapa somo kuhusu J. Edgar Hoover aliwezaje kuunda FBI na yataisha.
 
Sasa huko ni kutishana ingawa mimi wakija hao TISS hapa Kibaigwa watafahamu wanongea na nani na ntawapa chai ya mkandaa au kahawa na kashata na ntawapa somo kuhusu J. Edgar Hoover aliwezaje kuunda FBI na yataisha.
Ok mkuu mwambie aendelee kutukana taasisi za serikali.
 
Waanze na CEOs wa hizo Bank, huwezi kumkopa mtu mabilioni na hujui utazipataje au kuwa na risk management ya kuzuia uhuni kama huu, hizi ni Bank private inabidi shareholders watambae na wakurugenzi waliowakabidhi kuziendesha, uhamiaji au TISS wanaweza kusaidia lakini wenye Bank lazima wafanye kazi yao pia kuzuia huu uhuni wa mchana
 
Litakuwa ni jambo la uzuri sana benki hizi zikijulikana.
 
loan-image.jpg

Jana, raisi wa Jamhuri ya Muungano na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania kaeleza kwamba kuna mtu amekopa benki 5 au 6 tofauti za Tanzania na hajulikani alipo, yaani amekimbia na kutoka nchini.

Sasa huu ni mtihani kwa TISS, vyombo vya fedha, uhamiaji na wizara ya mambo ya ndani kwa ujumla.

Haiwezekani mtu mmoja akafanya jambo hilo zito na asepe kilaini hivyo hiyo ni ishara tosha kwamba idara yetu ya usalama na vyombo vingine vimelala au vimejiruhusu kupwaya kupita kiasi.

Lakini mimi ntaikosoa zaidi idara ya usalama kwani yenyewe ndio yaweza kuchagiza shughuli zote za ulinzi na usalama wa nchi.

Natambua idara hii ina uwezo mkubwa tu ina maofisa mahiri tu ambao wamepata mafunzo ndani na nje ya nchi hivyo wana ueledi, umahiri, uerevu na kila aina ya mbinu za kimkakati na kimedani kuhakikisha nchi yetu ipo salama.

Leo hii shirika la ujasusi wa ndani la Russia la FSB limetangaza kumshikilia mwandishi wa jarida la Wall Street Journal kwa madai ya kujihusisha na ujasusi wa ndani yaani kwa kiingereza twasema "Espionage".

Hiyo ni kazi ya majasusi wa ndani ya Russia yaani "Counter Espionage Agents" ambao wapo macho masaa 24 kulinda nchi, mali zake au "Assets" na miundombinu yake na wananchi kwa ujumla.

Sasa ni wakati wa idara yetu ya usalama wa Taifa kujipambanua kumtafuta huyu mwizi wa fedha zetu ambazo zimehifadhiwa kwenye mabenki zikiwa ni akaunti za watu na mitaji pia. Ni wakati wa kushirikiana na vyombo ya ulinzi na usalama vya nchi jirani na pia ni wakati wa kumtambua mtu huyo ambae ni wazi atakuwa alikuwa na pasi ya kusafiria, makabrasha mbalimbali yanoonyesha anuani zake na kadhalika hata kama ni "fake documents".

Kuhusu mabenki yetu nina imani kwa wana taratibu zote kali ambazo ni lazima mkopaji azifuate na kwenye hili ni lazima iwe ni "inside job" wafanyakazi walohusika ni lazima wapatikane kabla ya Jumaa.

Niliwahi kutoa mapendekezo huko nyuma kuhusu kuifanyia mabadiliko idara ya usalama wa taifa Mapendekezo: Serikali ipitie upya Sheria ya Usalama wa Taifa na TISS iundwe upya kwa maslahi ya taifa na nikzaeleza kwa upana wake.

Pia niliwahi kueleza kwamba wapo watu watembea na wallet tu Mtu anaesafiri kwenda nje kila siku lakini anabeba wallet na passport tu, utamfikiriaje? na hawa huenda ni wale ambao huenda sehemu kufanya machafuko kama uporaji fedha katika taasisi za fedha bila kugundulika na hii ni hatari kwa taifa.

Na pia nikawahi kutoa wazo kama nchi yetu ipo tayari kwa vita vya kijasusi wa uchumi katika mada hii Ujasusi wa Kiuchumi na Kiteknolojia unakuwa kwa kasi, Je Tanzania iko tayari ambapo yawezekana kabisa huyu mtu aliefanya wizi huu wa kughushi ni wale akina Carlos Jackal ambae alikuwa na uwezo wa kuingia katika nchi yoyote na kumaliza kazi kisha kujiondokea asijulikane.

Carlos alikuwa ni jasusi ambae alifunzwa kulelewa na kuwa alipwa ujira na idara ya kijasusi ya Russia ya wakati huo KGB na kazi zake hazikuwa na mfano.

Lakini mtu huyu ambae amehusika na wizi wa mabilioni ya shilingi si wa aina ya Carlos Jackal lakini aweza kuwa ni mhalifu wa kimataifa na huenda akarudi tena.

Hivyo Idara yetu ya TISS iamke isijisahau kwani majukumu yake si ya kisiasa bali ni ulinzi madhubuti wa nchi yetu vikiwemo vyombo vyetu vya fedha ambavyo kwa kushirikiana na vyombo vingine kama Uhamaji na hata huko nje Interpol tayari mtu huyu angekuwa yupo kwenye "Wanted List".
Nilishasema Hakuna TISS TZ kuna waganga njaa tu watu mkabisha
 
Hiyo ya mikopo mitano mikubwa ya mabillions itakuwa ni syndicate hatari mno. Siyo ya kitoto hiyo na itakuwa ilipangwa. Ukizingatia wapo pia watu wanaojiandaa na uchaguzi mwaka 2025.
 
Back
Top Bottom