Maelezo ya kutokea kwa mwanadamu yapo hivi.
Kwa uwezo wangu wa kufikiri bila kusoma popote, mm naamini mwanadamu ni zao litokanalo na dunia kwasababu kila ninachokiona sasa ni zao la dunia. Mfano miti, mawe, umeme, magari, ndege, wanyama, wadudu na kila kitu kinachotengenezwa na wanadamu na kisichotengenezwa ni material yatokanayo na hii sayari dunia.
Pili kila kitu kina exist na ku survive kutokana na support ya mazingira. Yaani kama mazingira hayaruhusu, basi kitu cha namna hiyo hakiwezi ku exist. Mfano samaki wa maji baridi huwezi kumkuta kwenye maji ya chumvi. Hata wanyama wa sehemu zenye asili ya baridi kuwezi kuwakuta kwenye joto. Hata mimea pia inayoota na kukua kwenye maji, haiwezi kuishi pakame.
Hayo yote ni kwa uwezo wangu kufikiri. Ila na wewe jiongeze utapata majibu kamili