Kama mwanamichezo umegundua nini mechi ya Simba na Yanga

Kweli marefa wanatuhujumu sana hata mechi ya Ruvu shooting ili takiwa tushinde ila klabu bingwa kule tutapita coz hamna marefa wa bongo
Wanaoongoza kwa malalamiko
1. Trump
2. Act & Chadema
3. Simba
 
Yanga ilitakiwa kumaliza mechi first half,Mbinu za Cedric second half kuwaacha wale mababu kupumua ndiyo imetumaliza Yanga.

Si mbaya, matokeo ya sare kwa Yanga ni faida kuliko mikia
Hivi kuna sehemu Cedric alisema alibadili mbinu kipindi cha Pili??Mimi nadhani Simba ndio Walibadilika, Simba walibadilika kuanzia kipindi cha Kwanza Dk ya 33 uwanja ulishainama mpaka half time, kipindi cha pili chote uwanja uliendelea kuinama , baada ya kusawazisha Yanga walikuwa ktk dk 5 ngumu sana ukiondoa shuti LA Fei Toto.

Kama MTU atataka kuja kunishawishi kuwa Kaze alibadili mbinu aniambie alibadili kuanzia Dk ya 33 kipindi cha kwanza.Rejea marudio ya game uone
 
Yanga ndio utamaduni wao, hata wakicheza na team nyingine ushindi wao ndio huo wa goli moja, ni culture ya club ya Yanga kuamini Goli moja linatosha kuleta points 3!!

Hilo LA Pili lipo sehemu zote duniani katika fani na taaluma mbalimbali wageni kuwa bora kuliko wenyeji, mgeni mzembe hawezi kutoka nje ya mipaka yake, akitoka lazima awe competent.Ni kawaida
 
unalazimisha timu kucheza unavyotaka wewe shabiki... kupaki basi ni mbinu ya mchezo pia
Kwanini mnadhani Yanga ndio imeamua kupaki basi na sio Simba ilibadilika na kuanza kupeleka Mashambulizi mfululizo??Uwanjani mpira uko mmoja tu, mwenzio akiumiliki wewe huna jinsi zaidi ya kuzuia
 
Hao wachawi wana uwezo?hawapendi hela?kama wana Uwezo si waende BOT wakabebe hela kimiujiza na mabegi wakawe matajiri??
 
Hao wanaosema hivyo ni upotolo wanatafuta sababu
 
Simba walibadili mbinu kutoka formation ipi kwenda ipi? Au kutoka katika aina ipi ya mchezo kwenda kwenye aina ipi?
 
Yanga wanahitaji kocha wa mazoezi ya viungo haraka iwezekanavyo. Simba hawana mbinu za maana za kimpira kulinganisha timu yeyote ya ligi kuu.
Ila Simba wapo juu sana kwenye stamina. Simba wana pumzi na inaonyesha wanafanya sana mazoezi ya viungo.

Simba karibu asilimia 75 ya ushindi wao ni kutokana na kumiliki kipindi cha pili. Pasi zao fupi pia ni mbinu nzuri ya kuhifadhi pumzi tofauti na timu nyingi za VPL ambazo hukimbiza mpira. Yaani unapewa pande refu la juu, halafu winger anakimbizana nalo na kumimina majalo.

Yanga, pamoja na kuwa na wings zenye mbio na mapafu ya mbwa, strikers wao hawapo hivyo.

Ningekuwa kocha wa kikosi kama cha Yanga, Nchimbi angekuwa striker, ningemfunza ku-strike yeye pamoja na Waziri junior.

Na midfield ningeweka Watano, wawili nyuma, Mukoko na Makapu.

Watatu mbele, Tuisila, Feisal na Haruna. Na wings wa kushoto ningemtengeneza boxer na Farid.

Ila VPL ina bahati yanga wamemkosa "Sure Boy".

Sarpong na Yacouba ... hapana.

Carlinhos naona bado ni mchezaji wa Instagram tu, kama Morrisson.
 
siku zote 'uoga' au 'over confidence' vina impact kubwa sana kwenye matokeo ya soka………...
 
Ukiifunga kila timu goli moja, unachukua ubingwa. No matter what!
 
Tatizo ni tafsiri wala siyo VAR.
Hata VAR ikiwapo tafsiri ya mwamuzi ni muhimu. Maana VAR inaweza kuonesha jinsi tukio lilivyotokea lakini mwamuzi akaona hamna sababu. Akapeta!
Kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…