Kama nchi tunajipangaje na huu uwezekano mkubwa wa WW3 ambao utakuwa na athari kubwa duniani?

Kama nchi tunajipangaje na huu uwezekano mkubwa wa WW3 ambao utakuwa na athari kubwa duniani?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Kwa mashambulizi ya jana na usiku huu waliyofanya Iran kwa Israel tutegemee Israel kujibu. Tishio ni kubwa kiasi kwamba "Doomsday Plane" ya Israel imeonekana ikipaa ikidhaniwa ni viongozi wanahama nchi. Ni kubwa kiasi kwamba inasemekana Netanyahu amehama Ikulu na kukimbilia kwenye jumba kubwa la bilionea mmoja Yerusalem lenye handaki kabambe yeye na familia yake.

Iran imesema wazi mwarabu yeyote atakayeingilia kati, atampiga. Putin amesema US wakiingilia kati na yeye ataiunga mkono Iran.

Kwa kuzingatia tetesi nzito na fukuto la vita kunauwezekano middle east ikafungwa kwa Muda, kuna uwezekano safari za meli zikafungwa kukatiza mitaa hiyo. Hivyo kutakuwa na athali kubwa kwetu.
Nashauri serikali na wadau kufuatilia kwa karibu na kutupa update nini cha kufanya badala ya kusubiri matokeo yake yatukutilize.

Binafsi kama mtumishi naombe taifa, letu na vita hivyo vikome ili amani iwepo tutangaze neno na Yesu aje tuhamie dunia mpya na nchi mpya ambayo hakuna vita, vikohozi wala taabu.
 
Bahati mbaya Mtumishi viongozi wa Nchi Yako wanatafutana huko nani anamtukana mwenzie mitandaoni.Wanahitaji maombi walau wawe na akili.Nafikiri yanayoendelea mashariki ya kati tamekuja wakati Nchi yetu ipo katika mapendekezo ya bajeti tunatarajia Kwa udharura Waziri wa fedha Dr Mwigulu kupunguza Kodi Kwa kiwango kikubwa vifaa vya mifumo ya gesi kwenye magari,nishati nao watenge fedha za kusapoti uanzishwaji wa vituo vingi vya kuwekea gesi na kuharakishwa utoaji wa vibali vya kufungua vituo,Bashe nae aje na mkakati wa Serikali kwenye kilimo kuna hofu ya njaa huko mbeleni.
NB:Bei ya mafuta haitaelezeka,tutegemee njaa Kali sana,pia naona Wazungu wengi wakikimbilia Africa kama kutakuwa na upenyo.
TUSISAHAU KUWAOMBEA VIONGOZI WETU WALAU MWAKA HUU WAWE NA AKILI.
 
Hivi kuna watu angali bado wanapiga magoti kuombea viongozi wa kiafrika?
 
Cha msingi ni kuwa na akiba ya chakula mvua zilizopo zitumike kulima sana na maghala ya chakula yaboreshwe
Chakula kisiende nje ya nchi
Wakati wa vita pesa huhitajika kidogo ila chakula na madawa ni sna
Acha ije si wanaitaka hao ambao siku zote wamejiita wastaraabu na watatua migogoro naona huu unawashinda
 
Back
Top Bottom