Kama nchi tunajipangaje na huu uwezekano mkubwa wa WW3 ambao utakuwa na athari kubwa duniani?

Kama nchi tunajipangaje na huu uwezekano mkubwa wa WW3 ambao utakuwa na athari kubwa duniani?

Kwani umeshajipangaje kwanza na mafuriko ya Rufiji na kwingineko yanayoua na kuhamisha watu?
Hayo tunayo siku zote. Pia watu wahamishiwe mbali na njia za maji maana Pwani bado kunaeneo kubwa bikra.
 
Hadi Sasa tupo milion 61, ikifika 2040 tutakuwa million 90 au 97 hadi Sasa hakuna kiongozi anayewaza athari za idadi kubwa ya watu ,hatuna mipango yoyote zaidi ya uchaguzi kila mwaka ,SEMBUSE VITA!!!!!
 
Ewe iran nakuamuru uache mara moja kushambulia taifa teule la Israel.

Muisraeli kutoka nanjilinji.
Uteule ulikuwa kwenye agano la kale sio Sasa.
Wa Sasa ni mazayuni yaani ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu
 
Hadi Sasa tupo milion 61, ikifika 2040 tutakuwa million 90 au 97 hadi Sasa hakuna kiongozi anayewaza athari za idadi kubwa ya watu ,hatuna mipango yoyote zaidi ya uchaguzi kila mwaka ,SEMBUSE VITA!!!!!
Mapori yamejaa anzia TU kibaha uone.
Usiitazame Dar ukidhani ndo nchi nzima imejaa hivi.
Population sio kizuizi Cha maendeleo
 
Nashauri serikali na wadau kufuatilia kwa karibu na kutupa update nini cha kufanya badala ya kusubiri matokeo yake yatukutilize.

Kwenye serikali ya bongo hakuna political analyists wala ushuzi wa analyists kwenye kada nyingine...

Kama wangekuwepo tusingekuwa hivi tulivyo kiuchumi, kisiasa na mambo mengine...

Sisi tunaenda kwa kudra...
 
Kwa mashambulizi ya jana na usiku huu waliyofanya Iran kwa Israel tutegemee Israel kujibu. Tishio ni kubwa kiasi kwamba "Doomsday Plane" ya Israel imeonekana ikipaa ikidhaniwa ni viongozi wanahama nchi. Ni kubwa kiasi kwamba inasemekana Netanyahu amehama Ikulu na kukimbilia kwenye jumba kubwa la bilionea mmoja Yerusalem lenye handaki kabambe yeye na familia yake.

Iran imesema wazi mwarabu yeyote atakayeingilia kati, atampiga. Putin amesema US wakiingilia kati na yeye ataiunga mkono Iran.

Kwa kuzingatia tetesi nzito na fukuto la vita kunauwezekano middle east ikafungwa kwa Muda, kuna uwezekano safari za meli zikafungwa kukatiza mitaa hiyo. Hivyo kutakuwa na athali kubwa kwetu.
Nashauri serikali na wadau kufuatilia kwa karibu na kutupa update nini cha kufanya badala ya kusubiri matokeo yake yatukutilize.

Binafsi kama mtumishi naombe taifa, letu na vita hivyo vikome ili amani iwepo tutangaze neno na Yesu aje tuhamie dunia mpya na nchi mpya ambayo hakuna vita, vikohozi wala taabu.
Pumbavu Yani umeongea vizuri mwanzo ila hapo umeanza kutema mafundisho feki ya wazungu eti yesu awaijie akawapeleke kwenye Dunia mpya 😂😂😂 Bado sana tena sana waafrika ngozi nyeusi kuja kujitambua wewe unawaza yeshu mfu aje akuokoe wakati wenye dini yao wapo wanaoambana kule
 
Ukisoma humu utaishia kucheka tu ! 😂😂😂 Israel haiwezi kujibu chochote kwa Iran itaishia kuonya onya tu na hii ndio itakuwa mwisho wa vita hata kule gaza. Msione Kuna nchi kama turkey, Pakistan,qatar,Kuwait zimetulia mkidhani haziwezi isaidia Iran ,subiri huyo Israel ayatimbe ndio aone
 
Kwenye serikali ya bongo hakuna political analyists wala ushuzi wa analyists kwenye kada nyingine...

Kama wangekuwepo tusingekuwa hivi tulivyo kiuchumi, kisiasa na mambo mengine...

Sisi tunaenda kwa kudra...
Development za mashambulizi ya Iran zimechukua wiki nzima, lakini hakuna influencer yeyote alikuwa anaandika hata twitter, wanadandia matokeo.
Pumbavu Yani umeongea vizuri mwanzo ila hapo umeanza kutema mafundisho feki ya wazungu eti yesu awaijie akawapeleke kwenye Dunia mpya 😂😂😂 Bado sana tena sana waafrika ngozi nyeusi kuja kujitambua wewe unawaza yeshu mfu aje akuokoe wakati wenye dini yao wapo wanaoambana kule
Ukweli ndio huo. Unaouona kwangu upumbavu ni hekima kubwa sana hahaha
 
Development za mashambulizi ya Iran zimechukua wiki nzima, lakini hakuna influencer yeyote alikuwa anaandika hata twitter, wanadandia matokeo.

Ukweli ndio huo. Unaouona kwangu upumbavu ni hekima kubwa sana hahaha
Pumbavu kujifanya unaijua sana dini ya watu kuliko waliokuletea, tena bila aibu eti "yeshu akija atatupeleka dunia mpya"😂😂😂
 
Sisi hatuna vita vingine vikubwa zaidi ya ujinga na umaskini na hatujapata ushindi hata 1%.hivyo vita vya wengine acha vitokee tujue madhara ya kuwa wajinga.
 
Sisi hatuna vita vingine vikubwa zaidi ya ujinga na umaskini na hatujapata ushindi hata 1%.hivyo vita vya wengine acha vitokee tujue madhara
Ujinga na umasikini wa taarifa sahihi ambazo zinaweza kutusaidia kuforecast ktk mambo ya kitaiafa na kimataifa.
 
MUHURI wa nne ulishafungiliwa ( ufunuo 6:8).

Vita havitakoma, njaa, Matetemeko, mafuriko,mapinduzi na majanga ya Kila aina nknk

Muhimu tutunze chakula, 2026 Kuna ukame mkuu utaikumba Dunia nzima Kwa miaka 3 na nusu.

Neema na Nuru itaanza kuonekana Tanzania kuanzia 2030.

Muovu azidi kuwa mwovu, Mwizi azidi kuiba, mtakatifu azidi kujitakasa.

Amen
 
Wiki mbili zilizopita Israel alirusha makombora kwenda Iran yakazuiliwa Leo Iran amejibu Western news Kila Kona Iran iran , congo Kila siku vita huoni western news zikiripoti Kwa ukubwa
 
Back
Top Bottom