Kama nchi tunajipangaje na huu uwezekano mkubwa wa WW3 ambao utakuwa na athari kubwa duniani?

Kama nchi tunajipangaje na huu uwezekano mkubwa wa WW3 ambao utakuwa na athari kubwa duniani?

Kwa mashambulizi ya jana na usiku huu waliyofanya Iran kwa Israel tutegemee Israel kujibu. Tishio ni kubwa kiasi kwamba "Doomsday Plane" ya Israel imeonekana ikipaa ikidhaniwa ni viongozi wanahama nchi. Ni kubwa kiasi kwamba inasemekana Netanyahu amehama Ikulu na kukimbilia kwenye jumba kubwa la bilionea mmoja Yerusalem lenye handaki kabambe yeye na familia yake.


Iran imesema wazi mwarabu yeyote atakayeingilia kati, atampiga. Putin amesema US wakiingilia kati na yeye ataiunga mkono Iran.

Kwa kuzingatia tetesi nzito na fukuto la vita kunauwezekano middle east ikafungwa kwa Muda, kuna uwezekano safari za meli zikafungwa kukatiza mitaa hiyo. Hivyo kutakuwa na athali kubwa kwetu.
Nashauri serikali na wadau kufuatilia kwa karibu na kutupa update nini cha kufanya badala ya kusubiri matokeo yake yatukutilize.

Binafsi kama mtumishi naombe taifa, letu na vita hivyo vikome ili amani iwepo tutangaze neno na Yesu aje tuhamie dunia mpya na nchi mpya ambayo hakuna vita, vikohozi wala taabu.
kuna watu wanajifanya wababe sana wengine wanajifanya wateule wa Mungu kumbe mashoga tu...wacha kipigwe ili tuheshimiane siku za mbeleni huko
 
Mathayo24:3-14
Omba kwa ajili yako na kwa ajili ya Kanisa la Mungu ulimwenguni.
 
Wazungu wakuda sana,Vita zinazowahusu wao hua lazima wazibatize jina la 'Vita ya dunia'.

Wapigane tu.
Wako sahihi.uko kwao ndo dunia ilipo.uku kwetu ni uvunguni mwa dunia.Kama afrika ata nuclea moja hakuna watasemaje sasa.Vita vyetu bado nivyafimbo.Wao wakiparurana impact inafika hadi uku uvunguni.
 
Hi vita ndio itakuwa mbaya kwetu sidhani kama tuna akiba ya mafuta ya kutosha
 
Kama una pesa nsssf,psssf bank kachukue Mapema utakuja kunishukuru serikali hua Inazuia pesa zote ikitokea ww3 .....
 
Back
Top Bottom