Kwa mujibu wa Prof Kabudi P.A.M '' Rais ni symbol ya Taifa. Wapambe ni wake ni Wanajeshi wakionyesha huyu ndiye''.
Sikumbuki Picha ya Rais mwingine ndani ya Ikulu zenye utata kama ya Tipwatipwa.
Watanzania hawamchukii Tipwatipwa, wanachukizwa na picha zenye ''symbol ya Taifa'' kuwa kama zinavyoonekana
Sikumbuki picha za Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Ngosha Magu zinazoonyesha mtu au watu wakiJInafasi mbele ya bendera za Taifa na Rais. Wanaofika Ikulu huelezwa protocol ! Tipwatipwa anajiachia kama yupo kwake ! too low
Idara ya Usalama, Mawasiliano Ikulu na Habari zipo wapi? Kipi JF imekifanya cha kuangushiwa zigo la siku 90!!
Ikiwa picha ni mbaya, Idara ya uslama ilikuwa wapi kuzuia mapema! kumuonya Tipwtipwa etc!
Madai ya Bentley, Ferrari, RR, Bugatti n.k. yanayohitaji kujibiwa na wahusika. Kununua hizo lazima mtu na source nyingine si mshahara wa serikali au Familia ya Kiongozi.
Viongozi husika watoke kueleza ni njia zipi zinazowapa kipato cha ziada cha kununua gari hizo, wasipofanya hivyo siku wakiambiwa wanamiliki Boeing na Chopper hawatakuwa na uhalali wa kutoa ufafanuzi.
Wakisema hawamiliki Boeing au Chopper, wataulizwa Bugatii, Bentley, Ferrari ! je! hii habari haitazimika
Kwamba Ngosha alikuwa clean ni jambo ''debatable'' . Kila mmoja abebe mzigo wake, hatuwezi kusema kashfa za ngosha zinahalalisha manunuzi ya Bugatti. Lakini pia hatuwezi kusema Ngosha alikuwa clean!
Kuna pesa za bargaining, kuna Bilioni 70 zilizopelekwa Mwanza, kuna 1.5 T haijulikani etc hakuna aliyefanya naye kazi aliyetolea ufafanuzi au kukanusha!
JokaKuu