Kama Ngosha angekuwepo, yule jamaa bonge Mzimbabwe angetia mguu wake kweli hapo Ikulu?

Kama Ngosha angekuwepo, yule jamaa bonge Mzimbabwe angetia mguu wake kweli hapo Ikulu?

What the helly JF massive?

Naona kama vile tunarudi nyuma kitaifa.

Hivi ni mimi tu au na nyie mnaona kama nionavyo mimi?

Endapo kama taarifa zote za kuuhusu ufisadi wa serikali iliyopo ni za kweli, ndo basi tena. Hatuna nchi.

Kilichopo ni personal fiefdom ya Samia and Co.

Mpaka kufikia 2030, chochote kidogo kilochobaki, hakitakuwepo tena.

Sikumbuki kabisa kipindi cha Magufuli kuona magari ya kifahari yanayohusishwa moja kwa moja na mtoto wa Rais na genge lake.

Sikumbuki kabisa kuwaona watoto wa Magufuli wakituhumiwa kusukuma ndinga za bei mbaya.

Kama ilitokea, basi nilipitwa. Au labda walikuwa wanaendesha kwa siri sana.

Ma RR, Ferrari, Bugatti, na kadhalika, yote hayo yanahusishwa na watu wa karibu sana na Samia!

Watu walio na makandokando ya ufisadi, Samia anawakaribisha sebuleni kwake halafu anakumbatiana nao, wanapiga na picha na kuzirusha kwenye mitandao.

Baadhi ya hizo picha zinalionyesha hilo li Zimbabwe likiwa limejiachia kwa raha utadhani lipo nyumbani kwake.

Magufuli naye alituhumiwa kwa mambo ya ufisadi, lakini mimi mpaka leo hii, sijawahi kuona ushahidi wowote ule ulio tangible.

Sijawahi kumwona Jesca Magufuli akiendesha Ferrari.

Sijawahi kumwona yule wa kiume, kaka yake na Jesca, akiendesha Bentley.

Hivi, huyu tipwatipwa wa Kizimbabwe angethubutu kweli kwenda nyumbani kwa Magufuli na kujiachia na kujitanua kama alivyofanya sebuleni kwa Samia?

Mambo kama haya kwa nini hatukuyaona wakati Magufuli akiwa Rais?

Kwa nini sasa hivi yameshamiri?

Hayo magari ya kifahari anayoyamiliki Abduli, kwa nini hatukuyaona kipindi mamake akiwa makamu wa Rais?

Kayanunua ndani ya hii miaka 4 ya mamake kuwa Rais?

Kidogo kidogo Ngosha mtamuelewa tu.

Alikuwa na mapungufu mengi.

Lakini naamini kabisa moyo wake na dhamira yake vilikuwa vimelenga pazuri.

Hii contrast iliyopo sasa hivi kati ya Samia na Magufuli, inaongea mengi sana.
Thubutu, Ngosha ni ngosha, Nkema ni nkema 😂
 
Hahahaha, JIBU kamili sidhani km utapata
Seriously, umewaona watoto wa Magufuli walivyo?

Ukiwaangalia tu unaanza kujiuliza hizo hela alizopiga baba yao ziko wapi?

Kabla Magufuli hajafa, hatukumwona Abduli akisukuma hizo RR, Bugatti, Ferrari, n.k.

Anafanya shughuli gani zinazomwingizia kipato cha kumudu kununua hizo gari?
 
Huyu jamaa [nadhani anakoneksheni na Abdul, pamoja na mtoto wa Ruto aliyeolewa na wapopo] labda alitumia huu mwanya kuangalia kama atapata vitenda hapa nyumbani.

Hajaishia kuingia ikulu ya Tanzania tu kafika hadi Kenya..... kipindi cha nyuma alishavutana na serikali ya Zimbabwe baada ya kushindwa kumaliza tender alizopewa....alishahusishwa na kutapeli watu...na kwenda jela...

Achana na hivi karibuni kuonekana kugawa pesa airport [kwao Zimbabwe anagawa magari na pesa kwa wasani] Zimbabwe kuna msanii anaitwa Jah Prayza anamtumia saana kwasababu ndiye mwenye ushawishi.

Anyway, ni kijana mpambanaji acha ajilie anavyojitafutia....
 
Imekuwa rahisi sana kumkosoa Rais Samia kutokana na kuwa mpenda demokrasia na kuheshimu uhuru wa watu kutoa maoni. Enzo za JPM hakukuwa na uhuru wa watu kutoa maoni na kukosoa. CAG aling'olewa kwa kufichua upotevu wa matrilioni ya pesa.

Mbaya zaidi kulikuwa na marafiki wa karibu wa JPM waliokuwa wanafanya mambo ya kihuni mno kwa kuwa JPM alikuwa mtu wao. Ilifikia sehemu makonda akawa kama makamu wa Rais... kina Sabaya walikuwa wakiogopeka kuliko mawaziri. Yaani uhuni mtupu. Pesa za Plea bargain watu walijipigia tu.
 
Seriously, umewaona watoto wa Magufuli walivyo?

Ukiwaangalia tu unaanza kujiuliza hizo hela alizopiga baba yao ziko wapi?

Kabla Magufuli hajafa, hatukumwona Abduli akisukuma hizo RR, Bugatti, Ferrari, n.k.

Anafanya shughuli gani zinazomwingizia kipato cha kumudu kununua hizo gari?
Duli alikuwa anauza tyre za magari kipindi cha mzee jiwe
 
Ngosha alikuwa anapigaje sasa hayo mahela?

Ana mahoteli? Ana majumba? Ana ndege? Ana meli?

Upigaji wa Ngosha ulikuwa kwenye nini? Migodi ya almasi?
Ngosha hakupiga, ila kundi lake linalomzunguka limepiga sana.

Kina Makonda, alexander Mnyeti, Doto james, walikuwa matajiri ghafla.
 
Ngosha naye alikuwa na upuuzi wake. Kama alimruhusu Musiba kuivunjia hadhi ikulu na kuifanya kuwa sawa na ukumbi wa DDC wa kukatia mauno, asingeshindwa kumkaribisha huyo ***** wa Zimbabwe.

Tangu 2015 Tanzania haijawahi kuwa na rais
Watu wa upinde tu ndio wana kumbukumbu mbaya sana kutoka kwa jpm.
 
Imekuwa rahisi sana kumkosoa Rais Samia kutokana na kuwa mpenda demokrasia na kuheshimu uhuru wa watu kutoa maoni. Enzo za JPM hakukuwa na uhuru wa watu kutoa maoni na kukosoa. CAG aling'olewa kwa kufichua upotevu wa matrilioni ya pesa.

Mbaya zaidi kulikuwa na marafiki wa karibu wa JPM waliokuwa wanafanya mambo ya kihuni mno kwa kuwa JPM alikuwa mtu wao. Ilifikia sehemu makonda akawa kama makamu wa Rais... kina Sabaya walikuwa wakiogopeka kuliko mawaziri. Yaani uhuni mtupu. Pesa za Plea bargain watu walijipigia tu.
1000358631.jpg

Jiwe huyu alietamani malaika washuke wafungie mitandao?
 
Ngosha alikuwa anapigaje sasa hayo mahela?

Ana mahoteli? Ana majumba? Ana ndege? Ana meli?

Upigaji wa Ngosha ulikuwa kwenye nini? Migodi ya almasi?
 
Back
Top Bottom