Kiukweli wengi wetu leo, hatukuwa tunajitambua wakati wa utawala wa Mwinyi.
Mzee Mwinyi anaonekana ni mtu asiyejali kuhusu wananchi wengine, as long as yeye kapata.
Huyu Mzee haheshimu wala haoni umuhimu wowote kuhusu sheria wala katiba ilimradi ziko upande wake.
Kina Warioba ingawa hawajazeeka sana lakini at least wanaweza kusimamia wanachosema.
1- Wakati wa utawala wa Magu alishawishi zaidi ya mara mbili kuhusu katiba ivunjwe ili Magu aendelee na madaraka.
Binafsi nilidhani ni kwasababu ya uzee, ila baada kuandika kwenye kitabu chake kujutia kuliachis uhuru bunge kuhusu kundi la G55 nimegundua ni hulka yake
2- Mzee Mwinyi rafiki yake ni yule mwenye nacho, mwenye uwezo wa kumpa anachotaka.
Hapa naweza kusema hana tofauti na Sheikh wa Mkoa wa Dar. Mwinyi alimkana kabisa January Makamba baada ya January na familia yake kukosana na Jiwe.
Kwa mantiki hii, sioni ni kwa namna gani tungesalimika kama Mwinyi angekuwa na maamuzi enzi hizo. Maana anaonekana siyo mzee mwenye kuridhika kabisa.