Uchaguzi 2020 Kama ni kweli basi Kamati ya Roho Mbaya ya CCM hasa Jimbo la Kigamboni mkimaliza Kumlima Mtu mnione

Mkuu GENTAMYCINE isije ukatafuta jinsi ya kumeza haya uliyoandika. Mimi huwa siamini matamshi ya wanasiasa hata siku moja. Yaani wanageuka kama lorry la Bedford. Ila ikiwa kweli ni safi sana sanaili akajifunze adabu na nidhamu.

Hivi ni kwanini Watanzania ( Waswahili ) ni Wagumu Kuelewa Jambo? Hivi nimesema nina uhakika nalo au nimesema kama ni kweli? Mnanikera!!!!
 
Yahusu tuhuma za vyeti feeeeeeeki zinazomkabili huyo Bashiteeee a.k.a migulu baja
aupate tu huo ubunge kelele zipungue mjini bhana
 

Angekua kweli ni mtu wa shukurani hasingethubutu kusimama hadharani na kumpakazia Rizwani kikwete kashfa ya kuuza madawa ya kulevya Huku akiwa hana ushaidi wa kutosha

Ikumbukwe Ridhwani ndio aliemuokota Makonda anatanga tanga UVCMM wakampa cheo

Sana sana akipita tusubili majigambo na mipasho
 
Hivi ni kwanini Watanzania ( Waswahili ) ni Wagumu Kuelewa Jambo? Hivi nimesema nina uhakika nalo au nimesema kama ni kweli? Mnanikera!!!!
Nami mwishoni nimesema kama ni kweli nitafurahi. Au hujanielewa?
 
Mie simuamini kbs jiwe, Bashite mwanakujipendekeza hawezi kutia nia Kigamboni bila kumshirikisha God Father!.

kifupi wanatuchezea shere, lao ni moja!.

itoshe tu kusema Bashite ni Mbunge MTEULE wa kigamboni!!!.
Na huu ndio ukweli mchungu na msema kweli siku zote ni mpenzi wa mungu!
 
Yaani huyo mtu alienda ugombea kigamboni atashinda kwa kishindo hamtaamini kama yanga ambavyo hawakuamini kupigwa goli nne na simba wiki jana
 
Hii kali
 
Hata tabir zako za Simba kuifunga Yanga tareh 8 zilikuwa hivi hivi.Tangu pale sikuamin kabsa na mambo unayosema huwa ni vice versa.
 
Kaka duwa za kuku hazimpati Mwewe. Mlezi wa Wcb haepukiki tutake tusitake tupende tusipende lazima aingie bungeni. Ikitokea amechujwa njoo pm nikupe vocha ya buku
 
[emoji1666]
Mie simuamini kbs jiwe, Bashite mwanakujipendekeza hawezi kutia nia Kigamboni bila kumshirikisha God Father!.

kifupi wanatuchezea shere, lao ni moja!.

itoshe tu kusema Bashite ni Mbunge MTEULE wa kigamboni!!!.
 
Kaka gent kwa hili Sina imani nalo kabisa,..nnachoamini mpka Sasa Kaka mkubwa atalinyakua Jimbo..lile mapema Sana..na atakuwepo kwenye baraza la mawaziri msimu ujao..na hata Kama hatopita Basi anaweza akateuliwa..
✓isipokuwa hivyo,.nidai elfu kumi
 
Kiukweli kutoka ndani ya vilindi vya Moyo wangu nafarijika Sana kuona makonda anenda kuwa mbunge wangu na spika mpya wa bunge la Tz.
 
Kama mtu anapewa uongozi wa mkoa tuu anakuwa na kauli za aina hii nawe bado ukampenda, basi tatizo sio yeye ila utakuwa wewe ambaye huchukizwi na ujinga, majivuno na kebehi.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…