Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,072
HIARI YASHINDA UTUMWA ni moja ya msemo wa Kiswahili wenye hekima kubwa sana unaoonesha umuhimu wa personal integrity.
Ukiwa muadilifu, utakuwa na nidhamu ya kutekeleza wajibu wako bila kusukumwa wala kulazimishwa.
Kwa bahati mbaya sana, Watanzania kwa asilimia kubwa hatujalelewa kuwa waadilifu na kujisimamia. Tukiaminiwa tunafanya hiyana.
Kimsingi, tumekuzwa kuogopa wakubwa zetu (wazazi/walezi) na mambo mengi tulitekeleza kwa hofu ya kuchapwa au kunyimwa chakula. Kinyume na hapo HATUFANYI.
Hii kansa imesambaa hadi kwenye maeneo ya kazi, biashara na sehemu za utoaji huduma. Mashirika mengi yanayoongozwa na wageni hawapendelei kuajiri watanzania kwa sababu ya uzembe, ukosefu wa uaminifu, uadilifu, kutowajibika na kutojisimamia.
Tumeona hata serikalini, watumishi wa umma walitekeleza majukumu yao ipasavyo kupitia 'nidhamu ya uoga' na mambo yakaenda.
Hivyo, kama nidhamu ya uoga ilisaidia watu kupata huduma nzuri, basi inatufaa sana kutokana na tulivyokuwa programmed tangu utotoni.
Kinyume na hapo ifanyike kazi kubwa ya kubadili tabia (behavioural change) kwa taifa zima. Mchakato ambao utahitaji muda na nia thabiti.