Kama nikiulizwa kuwa nimeridhika na Utawala wa Rais Samia au ninamkumbuka Hayati Magufuli

Nakwambia hata wapinzani sasa hivi wanajua hakuna rais kama jpm, sijui alichelewa wapi kuwa rais hata kama asante mungu kutuonesha kuwa kuna watu wenye uwezo wa kipekee kama jpm
Yaani acha tu...
 
Watu wa instagram ,facebook n.k.wanamlilia sana JPM na kumkumbuka,ila humu sijui mnakuwa mmetumwa? ...[emoji2][emoji2]
Twitter na JF huwez AMINI kama nao ni watanzania. Huko FB na Ista ktk comment 1000,hazifiki 20 za kumponda Magufuli. Maoni sahihi na ya watanzania wengi huwez yapata Twitter au JF
 
Reactions: tyc
😂😂😂😂😂😂😂🙀🙀🙀🙀🙀🙀🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Twitter na JF huwez AMINI kama nao ni watanzania. Huko FB na Ista ktk comment 1000,hazifiki 20 za kumponda Magufuli. Maoni sahihi na ya watanzania wengi huwez yapata Twitter au JF
Wa JF walisema Lissu atashinda kwa zaidi ya asilimia themanini,hawakujua Watanzania waliowengi hawajawahi kusikia hata JF Nini,kilichooza nafikiri alimusimulia Bibi yake Ikungi.

UN kumuenzi JPM kuliwaumbua, Watanzania kukanyagana wakimuaga lilikuwa pigo jingine.
 
Dikteta alikuwa anatutia hofu wafanyakazi na wafanyabiashara
 
Samia ana hofu ya Mungu,huwezi kumfananisha na dikteta mwendazake
 
Mzee alikuwa na roho chafu mnoo
 
Na kwa upande mwingine linganisha Uongozi wa Kikwete aliajiri walimu wote tena bila application kila mwaka
Alipandisha mishahara ya watumishi na madaraja kila mwaka.
Aliunganisha barabara za lami mikoa yote.
Alijenga hospitali kubwa za kitaifa.
Alijenga chuo kikuu kikubwa Africa Mashariki.
Aliruhusu democrasia.
No.
Hapo sasa na umlinganishe na Ngosha
 
atafungwa kulingana na nguvu ya ushahidi au kuachiwa kutokana na udhaifu wa ushahidi.
nchi yetu inaongozwa na utawala wa sheria, ndio maana yupo mahakamani.
 
Hivi huwa mnazungumzia huu Uchaguzi uliopita au mnatania.
Kwa taarifa yako huo Uchaguzi ilikua ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu.
Na inawezekana Mungu aliamua kufanya yake baada ya kuona uonevu katika Uchaguzi huo.
 

Kikwete amefanya mengi sana ambayo ni mazuri pia

Lakini mada inahusu ulinganisho wa JPM na Samia,
labda ufungue uzi mpya wa JK vs JPM
 
Kweli kabisa ,pamoja na ufisadi lakini aliweza kufanya yote hayo,jamaa yangu yeye kazi aliyofanya ni Kujenga vipandevipande vya barabara kwa kutumia mishahara ya wafanyakazi ambayo hakupandisha miaka 5.

Alijenga barabara kwa misaada ya maafa waliyostahili kusaidiwa wahanga wa majanga.

Alijenga barabara kwa misaada ya fedha za corona..
Nchi ilipoteza mahusiano ya kimataifa.
 
Mzee alikuwa na roho chafu mnoo
Yaani badala ya kuiunganisha nchi yeye akaanza kuigawa.
Kwamba Hawa msiwabomolee kwa sababu waliomchagua.
Wale waliobomolewa ni wale ambao hawakumchagua.
Aisee hiyo roho ya ajabu sana.
Uchaguzi sio chuki.
Uchaguzi ni njia ya kupata viongozi tu.
Hebu fikiria wagombea wa Upinzani qakieudiaha fomu eti wanawekewa pingamizi kwa kukosea herufi tu halafu nchi mzima.
Au wanatekwa njiani wanachelewa halafu fomu zao zinakataliwa.
 
Samia ana hofu ya Mungu,huwezi kumfananisha na dikteta mwendazake
Vyovyote Samia atakavyokua lakini hawezi kuwa na roho kama ya Jiwe.
Jiwe hakua binadamu aisee.Tungeendelea nae miaka mingine mitano watu wangekoma Sana .
 
Ni kweli alikuwa wa kipekee kwa kujigia promo kubwaaaa kwenye mambo ya kawaida kabisa
Kweli kabisa mambo yanayostahili kufanywa na serikali yoyote yeye aliyafanya yaonekane ni yeye kafanya,wakati watu wanalipa kodi na hata maraisi wengine walishayafanya tena zaidi yake.
Alivitisha vyombo vya habari vikawa vinaimba nyimbo zake tu.
 
Kikwete amefanya mengi sana ambayo ni mazuri pia

Lakini mada inahusu ulinganisho wa JPM na Samia,
labda ufungue uzi mpya wa JK vs JPM
Aloanzisha ulinganisho wa JK na JPM kwenye mada hii sio mimi.
Mbona hukumjibu huyo kwanza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…