Mleta mada,
Ukitaka ujue ubora na udhaifu wa JPM na Mamá Samia basi ingekupasa urejee changamoto tulizokuwa nazo toka awamu ya Kikwete.
**Rejea zile kelele za wananchi tukiongozwa na Chadema juu ya ufisadi wa Serikali ya JK ( skendo za EPA, Richmond, Escrow, ufisadi nssf) matumizi mabovu ya kodi za wananchi (safari za nje ya nchi za viongozi mbalimbali, semina na warsha zenye posho nono nono etc)
, rushwa kila kona, madawa ya kulevya, ujambazi na uporaji silaha kwenye vituo vya polisi, ugaidi wa kibiti mkuranga, ukwepaji kodi bandarini na kwenye biashara, watumishi hewa, huduma mbovu sekta ya afya, ubovu miundombinu ya barabara reli,na mengine kadha wa kadha
Kisha angalia alivyoingia Magufuli madarakani ameweza kushughulikia kwa kiwango gani hizo kero na changamoto zilizokuwa zinaikabili nchi yetu, ndipo utajua Magufuli alipiga kazi au alikuja kuuza sura
Sio unaleta vitu dhaifu dhaifu vya kumlinganisha Magufuli na Mamá Samia eti huruma, hana dharau, hana visasi, anapenda watu,,,, shabaaashhh....!!!
Magufuli hakuja kuuza sura, alikuja kuchapa kazi na kazi imeonekana.