Wait! , katika kipindi hicho cha manabii, mtu angeandika mawazo yake (mfano waandishi wa Quran, na vitabu vingine), kisha wakasema ni maono toka kwa Mungu, nini kingeamua kipi cha kukipokea kama ‘uteremsho’ na kipi sio ‘uteremsho’ , ilihali wote wamedai ni maono?
Halafu kuwa mstaarabu, sijaja hapa kuchat na ChatGPT. Ukileta jibu lisilo na mantiki toka ChatGPT kama ambavyo unafanya, mjadala utaishia hapa.
Hujajibu swali mkuuTofauti ipo
👉 Ujumbe haujafungwa kwenye lugha moja.
- Hakuna ibada inayolazimisha lugha ya awali (unaweza kusali kwa Kiswahili)
Wait! , katika kipindi hicho cha manabii, mtu angeandika mawazo yake (mfano waandishi wa Quran, na vitabu vingine), kisha wakasema ni maono toka kwa Mungu, nini kingeamua kipi cha kukipokea kama ‘uteremsho’ na kipi sio ‘uteremsho’ , ilihali wote wamedai ni maono?Kitu gani ambacho hakina mantiki , Mbona mnaogopa Chartgtp imewakosea nini ?? Unahakika gani kuwa nimechukuwa ChartGtp ?? hata kama nimechukuwa kwani wewe unalo jibu tayari ?? Mimi nakuruhusu utafute maswali huko chartgtop au website ya kanisa lolote , utajibiwa tu
Wait! , katika kipindi hicho cha manabii, mtu angeandika mawazo yake (mfano waandishi wa Quran, na vitabu vingine), kisha wakasema ni maono toka kwa Mungu, nini kingeamua kipi cha kukipokea kama ‘uteremsho’ na kipi sio ‘uteremsho’ , ilihali wote wamedai ni maono?
Unafunuaje (kuteremsha)kile ambacho kimeshafunuliwa? , na kurekebisha sio kukosoa ambacho kilishafunuliwa (kuteremshwa)?Moja ya vigezo muhimu zaidi kutumia ni kuangalia Je, ujumbe huu unalingana na kile ambacho Mungu tayari amekwisha kufunua?
Katika Biblia
Nabii aliyepingana na Taurati alikataliwa (Kumbukumbu la Torati 13).
Katika Uislamu:
Qur’ani inajitambulisha wazi kuwa inathibitisha ufunuo uliotangulia huku ikirekebisha upotoshaji (Qur’ani 2:97, 5:48).
Hii ina maana kwamba:
Ufunuo ulipimwa kulingana na mfumo wa imani wa kiteolojia uliokuwepo tayari
Unafunuaje (kuteremsha)kile ambacho kimeshafunuliwa? , na kurekebisha sio kukosoa ambacho kilishafunuliwa (kuteremshwa)?
Na je, hicho kilichoteremshwa awali, kilichaguliwa vipi kwamba ndio kimeteremshwa kati ya vingi vilivyodaiwa kuteremshwa
tunafafanua na kufikisha ujumbe wa ufunuo uleule.
🤣Wanasema hicho ni kibri cha allah yeye ndio anaamua afanye nini
hicho kilichoteremshwa awali, kilichaguliwa vipi kwamba ndio kimeteremshwa kati ya vingi vilivyodaiwa kuteremshwa kwa wakati huo?Katika Uislamu, hakuna kufunua upya kile ambacho tayari kimefunuliwa kikamilifu.
Ufunuo (wahyi) ni tendo la Mungu peke yake, si la mwanadamu.
Kinachofanywa na wanadamu ni:
Hivyo basi, hatusemi “tunateremsha tena ufunuo”, bali:
- Kukisoma kilichoteremshwa
- Kukielewa
- Kukifafanua (tafsiri) kulingana na lugha na muktadha
- Kukifundisha na kukitekeleza
hicho kilichoteremshwa awali, kilichaguliwa vipi kwamba ndio kimeteremshwa kati ya vingi vilivyodaiwa kuteremshwa kwa wakati huo?
“Hakika Sisi ndio tulioteremsha Ukumbusho, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda.”
(Qur’ani 15:9)
“Leteni sura moja mfano wake ikiwa mnasema kweli.”
(Qur’ani 2:23)
Hata sasa, wapo akina Gwajima ambao hawaji na Mungu mpya, hawajaleta maadili mapya yasiyo na mizizi, wanadhibitisha uwajibikaji uleule wa Nuhu, Ibrahimu, Musa na Isa.Katika Uislamu, hakukuwa na mchakato wa wanadamu kuchagua kati ya “mafunuo mengi yanayodaiwa”.
Kilichoteremshwa (Qur’ani) kilijithibitisha chenyewe kwa sifa zake, na Mungu Mwenyewe akahakikisha ulinzi wake:
Hii ina maana: uthibitisho haukuachiwa wanadamu.
wakati wa Mtume Muhammad ﷺ kulikuwa na:
- washairi waliodai kupata ilhamu
- makuhani (kahin)
- watu waliodai kuwasiliana na majini
- watu waliodai unabii wa uongo (kama Musaylimah)
Lakini Qur’ani ilijitofautisha wazi na hayo kwa:
Lugha na muundo usiofananishwa
Waarabu bingwa wa lugha walitambua mara moja:
- si ushairi
- si maneno ya kuhani
- si hotuba ya kawaida
Ndiyo maana Qur’ani ilitoa changamoto:
Changamoto hii haikujibiwa, licha ya uadui mkali.
Kilichoteremshwa:
- kilimkosoa Mtume mwenyewe ﷺ
- kilimwekea majukumu mazito, si manufaa binafsi
- kilipingana na desturi, maslahi na mamlaka ya makabila
Huu si mtindo wa “maandishi ya kujitunga”.
Tukiiangalia Qur’ani Tunaona
- haikuja na Mungu mpya
- haikuleta maadili mapya yasiyo na mizizi
- ilithibitisha tauhidi, maadili, na uwajibikaji uleule wa Nuhu, Ibrahimu, Musa na Isa (amani iwe juu yao)
Lakini pia ikasahihisha upotovu uliokuwa umeingia katika simulizi zao.
Kwani lini Gwajima alisema maneno yake yameshushwa? Gwajima huyu mlaji wa maboga ya kondoo wake, mpaka video zimo mitandaoni? 😝😝😝Hata sasa, wapo akina Gwajima ambao hawaji na Mungu mpya, hawajaleta maadili mapya yasiyo na mizizi, wanadhibitisha uwajibikaji uleule wa Nuhu, Ibrahimu, Musa na Isa.
Je, maneno ya Gwajima yameshushwa?