Jamaa wamejitengenezea sheria za ajabu sana yaani kifupi wapo juu ya sheria. Wamekuwa ni jeshi, sasa sijui watakuwa wanavaa sare ??? Sielewi. Hawaripoti popote zaidi ya kwa Rais tu, yaani wao bosi wao ni Rais tu na sio kinyangarakata yoyote inshort wao ni zaidi ya JWTZ kwa mfumo huu. Wamekuwa na hadhi ya jeshi alafu wana kinga ya kutoshtakiwa patam hapo [emoji1787][emoji1787]
Yaani Tanzania tunazidi kupotea wenzetu intelligency organs zao wanazipanga kisasa zaidi kwa ajili ya kiuchumi na teknolojia sisi tunazitengeneza kulinda dola zaidi kwa ajili ya siasa. Hivi wakishakuwa jeshi so what? Wanataka kupambana na nani kwa kutumia nguvu? Tutakuwa na majeshi mangapi? Lakini kwasehemu kuhusu "kinga" nimewaelewa kwanini wameomba, huwezi kunituma nikafanye kitu kitakachoniingiza matatani wakati wewe mwenzangu una kinga alafu mimi sina kinga, lazima na mimi unipe kinga ndo twende sawa. Mindonilivyoelewa kwa mawazo yangu, na hapo kama kiongozi unajijua unanitumaga na unataka kuendelea kunituma lazima utanipa tu kinga.
Ila all in all Tanzania tunapokwenda sio kuzuri tutafika sehemu Katiba mpya haitawezekana tena na kuna watu hawatataka kutoka madarakani hata wakishindwa na wananchi hawawataki kwasababu watakuwa wameshaharibu vya kutosha hivyo watahofia wakiingia wengine watakuwa katika hali mbaya. Chanzo cha kuharibu ni kuanza upitishwaji wa mambo kama haya, safari moja huanzisha nyingine. Mtu aliyejiwekea kinga ni nadra sana kujali haki ya mtu mwingine zaidi ataangalia maslahi yake kwanza. Haki ikitoweka amani pia hutoweka, ndo chanzo cha machafuko.
Minilidhani sasa hivi TISS wangejitengeneza kisasa zaidi kwa ajili ya kusaidia Taifa letu, pamoja na kulinda usalama kupitia intelligence na sio kupitia force; wahakikishe tunapata teknolojia muhimu kwa ajili ya nchi yetu. Kusaidia wafanyabiashara kupata dili kubwa nje ya nchi na kulinda rasilimali zao zilizopo nje. Kulinda rasilimali zetu against mabeberu na matepeli papa, haya yote yanafanyika kupitia ukusanyaji uchambuaji na uchakataji wa taarifa na kutengeneza mikakati then kuwapata watu sahihi wa kutekeleza. Haya hayapatikani eti kwakuwa Jeshi hapana ni kuwa wa kisasa zaidi tena kuwa underground zaidi. Minilichoona katika huu muswada ni kama wanataka misifa tu ambayo kama nchi haitusaidii chochote. Ndomana siku hizi kijana akiwa huko atafanya kila kituko ili tu umtambue yeye ni nani[emoji1787][emoji1787]