Kama Saudi Arabia na Vatican wameweza kufanya ibada majumbani sisi tuliopokea dini toka kwao tunashindwa nini?

Masikini huficha ujinga na uzembe wake kwenye dini? Eti viongozi wanaotuhumiwa kufuja Mali zetu,kuteka na kuua watu wasio na hatia eti ndo hao hao Leo wanajifanya wacha Mungu
 
Serikali inataka huruma baada ya kufanya uzembe wa kiwango cha SGR
 
Tuliupokea kutoka wapi? Wao waliouleta wanakusanyika?
 
Viongozi wa dini wamewatoa kafara kondoo wa bwana.
 
Kama serikali imeweza kufunga shule na vyuo hadi vya hayo makanisa na misikiti,inashindwaje kupiga stop hizo ibada?
 
Asante kwa kuweka kumbukumbu sawa! Ccm na serikali yake wanahisi wakitekeleza ushauri watawapa credit "wapinzani" na kuonekana wamekosa maarifa na kwahiyo waanaendeshwa kwa "remote controller".
 
Ukimpa mtoto wako madafu ampelekee kitukuu chako bado ni sahihi kusema Uledi amepokea madafu kutoka kwa nyanya yake.
Dhana ya kupokea kitu ni pana sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatuongelei madafu, hapa tunaongelea elimu ya dini. Ndiyo maana tuna masomo ya historia ya dini. Sijawahi kuona historia ya madafu.
 
Vipi kuhusu sadaka?..
 
Ndugu yangu kwanza ninakupongeza sana kwa andiko zuri. Ni Serikali pekee ndiyo inayoweza kuepusha wananchi na hili janga. Sihitaji kurudia

Sihitaji kurudia andiko zuri uliloandika na majibu mazuri kabisa ya wanajamii forum. Ni serikali pekee ndiyo itaweza kuepusha wananchi na hili janga kwa kutoa uamuzi sahihi kama ulivyosema. Mungu wetu anaabudiwa katika Roho na Kweli. Siyo majengo! Viongozi wa dini kamwe hawatasema ibada zisifanyike kwenye majengo kwa sababu zao. Na shetani hupenda kuanza na viongozi kwanza na siyo waumini wa kawaida kusambaratisha makanisa.
 
Nimekuelewa!
 
Hapa napata elimu, ahsante mkuu!
 
Serikali za Saudi Arabia na Italia zimetoa amri za kufungwa misikiti na Makanisa.
Kwa nini serikali yako haitoi amri hiyo?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…