Kama Saudi Arabia na Vatican wameweza kufanya ibada majumbani sisi tuliopokea dini toka kwao tunashindwa nini?

Kama Saudi Arabia na Vatican wameweza kufanya ibada majumbani sisi tuliopokea dini toka kwao tunashindwa nini?

Unajua ukishakiri kua yesu ni bwana na mwokozi wa maisha yako unakua umetangaza vita na shetani, na shetani atajaribu kufanya kila njama za kukuporomosha hapo juu ulipo

Unajua kwamba shetani kapewa mamlaka ya kumjaribu binadamu na katika hili shetani kaamua kutumia huu ugonjwa kama jaribio ili kuwateka watu?

Unajua kukubali kusalia nyumbani kwa kuogopa maambukizi ambayo yamepangwa na shetani ni ishara kwamba shetani amekushinda nguvu na umekosa imani ya kupambana naye?

Unaelewa kwamba namna pekee ya kumshinda huyu shetani ilitakiwa yeyote yule ambaye amemkiri yesu kua bwana na mwokozi wa maisha yake ajitokeze katika wodi za wagonjwa wa corona kwa lengo la kuwafanyia sala ya toba kwa kuwashika vichwani?

Mnakumbuka kua ukiwa na yesu hakuna lishindikanalo maana amewaahidi kutengeneza njia mahala pasipo na njia?
Takataka! Ujinga mtupu! Kibwetere wewe.
 
Nyie mnaoshikilia misikiti na makanisa mnashangaza maana sababu yenu ni kwamba hiyo ni mikusanyiko isiyo ya lazima,watu wanaweza wasiswali misikitini na makanisani ila bado huku mitaani maisha yapo kama kawaida hakuna kilichobadilika. Na huku ndiyo tunachanganyika wote kuazia wanafunzi waliyozuiliwa kwenda shule,waumini mnaotakata kuzuia wasiabudu kwenye majumba ya ibada na hadi akina Kiranga pia tunakusanyika nao huku mitaani.

Kama kweli mmeona corona ni hatari na mna nia ya dhati ya kuzuia maambukizi basi yafanywe maamuzi ya kweli sio haya kutaka kuzuia wanafunzi wasisome na waumini kwenda kuabudu kwenye nyumba za ibada lakini watu hao hao wanakusanyika mitaani kama kawaida na hufanya mambo yao kama kawaida watu itakuwa ni kazi na bure tu.

Mie ndiyo maana nasema ikiwa bado hadi sasa tunatoleana mifano ya Italy na Spain kuonesha uhatari wa corona basi bado waafrika hatujaona huo uhatari wa corona hapa afrika na ndiyo maana maisha bado yanaendelea kama kawaida.
hivyo watu wanavyojaa pale Kariakoo si zaidi ya waliopo Kanisani?. Kwa nini Mungu alimwambia Suelemani amjengee hekalu? wakati yeye yuko kila mahali?
 
32829755-983D-4B74-9622-C91E2EB3F508.jpeg
 
hivyo watu wanavyojaa pale Kariakoo si zaidi ya waliopo Kanisani?. Kwa nini Mungu alimwambia Suelemani makengee hekalu? wakati yeye yuko kila mahali?
Tatizo watu ni kama wamepania vile hiyo misikiti na makanisa tena wengi hawa wasiokuwa na dini.
 
Kwani mmelazimishwa kwenda misikitini na makanisani? Ukiona kusalia nyumbani ni sawa ni bora ukafanya hivyo kuliko kubeza wanaoenda makanisani.. mbona huko marekani, Italy, Spain na kwingineko wamefunga hayo makanisa na misikiti tokea kitambo sana na bado wanadondoka kama kuku!
 
Dunia ya leo imejaa maasi, imani hazitponyi tena, kirusi kinaua hata makanisani tena kwa walokole, tumepewa hekima na Mungu tuitumie.
Kuna miaka ile, ilikua rahisi kuomba na miujiza inatokea, leo hii hao akina Gwajima video zao wakifanya porn zimezagaa kwenye internet, ndio unawategemea wakuombee.

Lakini ukiomba msamaha si unasamehewa?

Si wote mnakubali kua Mungu ni mwenye huruma na husamehe endapo utafanya toba?

Na hawa watoto wadogo wanaokufa kwa corona imekuaje waambukizwe hadi kufikia hatua wanakufa je wao wamefanya mahasi gani mbele za Mungu?

Hadi chui wanapata corona, sasa nao hawa tunawaweka katika kundi gani? Chui nao wanafanya maasi?

It's Scars
 
Mbona hamponyi corona sasa? Pamoja na kukusanyika kwa siku zote hizo idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka? Kuendelea na mikusanyiko ya ibada hali tunajua wazi ugonjwa unaambukiza sana kutokana na mikusanyiko ni kumjaribu Mungu wala haina tofauti na shetani alivyomtaka Yesu amjaribu Mungu. Majibu ya Yesu kwa jaribu kama lenu ni haya (Lugha Kiingereza na Kiswahili):-

Matthew 4:5-7
"[5]Then the devil taketh him up into the holy city, and setteth him on a pinnacle of the temple,
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,

[6]And saith unto him, If thou be the Son of God, cast thyself down: for it is written, He shall give his angels charge concerning thee: and in their hands they shall bear thee up, lest at any time thou dash thy foot against a stone.
akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

[7]Jesus said unto him, It is written again, Thou shalt not tempt the Lord thy God.
Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako."

Acheni kuwa mawakala wa shetani kwa kivuli cha Yesu.

Pia tambua kwamba Mungu yupo mahali popote na baadhi ya sifa zake ni hizi:-

1. God is omnipresent - Mungu yupo kila pahali.

2. God is omniscient - Has unlimited knowledge; Uelewa wa Mungu hauna mipaka (hakuna asichokijua).

3. God is omnipotent - God has unlimited power; Mungu ana nguvu/uweza usio na kikomo.

Ndiyo maana hata mkuu wa katoliki (Papa) anawaambia waamini wake Waungame popote pale walipo Mungu yupo na anawasikia badala ya kwenda kwa kasisi/padri kama wengi walivyozoea.

Nimekuonesha hapo kua ukiwa na imani hakuna jambo ambalo linaloshindikana

Mfano yesu alipokua anatembea juu ya maji halafu petro akamuuliza vipi nami naweza kutembea yesu akasema waweza kutembea ilimradi tu unaimani

Petro akatembea hatua kadhaa ila alipoweka hesitation kua mahali aendapo pana kina kirefu hivyo kuna uwezekano anaweza kuzama ndio imani ikamshuka na akazama

Kwaiyo hapo imani ndio "key" kupitia imani umepewa mamlaka ya kuamuru hadi milima iame

Mfano mwingine daniel alipowekwa katika tundu la simba wenye njaa kali, wale mabwana walitaka wamgeuze msosi kwa simba ila kwasababu alikua na imani simba hawakumfanya chochote

Mfano mwingine ni wale meshak shadrack na ebednego walivyowekwa katika tanuru la moto, kwakua walikia wakimtumainia Mungu wa ukweli na walikua na imani iliyothabiti moto haukiweza kuwadhuru hata kidogo

Sasa kwanini ufikiri kuwe kuna ugumu kwa hawa wanaojiita wapakwa mafuta ya bwana kujitosa hospitalini kwa kuwafanyia hudumu ya maombi kwa kuwashika vichwa haonwagonjwa wa corona na wakati wanaimani??

Hujui kwamba kipimo cha imani ni majaribu? Hujui kwamba hili gonjwa nalo ninsehemu ya majaribu ili kupima imani ya watu?

Unajua kama kosa ulishafanya pale mwanzo ulipokula kiapo kua umemkubali yesu kua bwana na mwokozi wa maisha yako, kwa maana ya kwamba ulikwisha tangaza vita na shetani?

Unaelewa kwamba formula ya kukataza watu kwenda majumba ya ibada ni sawa na formula ya mourinho kupaki basi wakati wa kandanda??



It's Scars
 
Jana nilimsikia Prof Lipumba akisema yeye ameanza kuswalia nyumbani ili kuepuka misongamano inayoweza kusababisha maambukizi ya Covid 19.

Binafsi nikawa nimemwelewa vilivyo.

Ndipo nikaanza kutafakari, kama Waislamu kule Saudia wanaswalia nyumbani Bakwata wanashindwa nini?

Kama Wakristo kule Vatican, UK na Germany wanasalia majumbani hawa Katoliki, Anglican na KKKT wanafeli wapi?

Kama Walokole huko USA wanasalia majumbani hawa kina Kakobe, Gamanywa, Gwajima, Mwingira wanashindwa nini?

Kuna wakati yatupasa kutumia busara hata kama mamlaka za juu zimewaachia hiyo fursa bado mnatakiwa kutumia hekima ya Mungu kutenda jambo sahihi.
Serikali haiwezi kuwakataza directly lakini nyie mmebarikiwa macho ya rohoni na mwilini na hata hao wagonjwa 88 waliotangazwa hadi sasa ni waumini wenu.

Hekima ya Mungu wa mbinguni na iwe juu yenu!
Waafrica tunaweka siasa hata kwenye mambo ya majanga.......wacha tupukutuke ili tutie adabu......

eti makanisa yasifungwe sababu yanaombea Corona.....yale yale ya Kibwetele.
 
Dini sio hizia au mawazo yako ujue, katika hali isiyo ya dharura katika mafundisho sahihi ya uislam mwanaume anawajibu wa kuswali jamaa msikitini na waumini wenzako, sio kwamba ukiswalia nyumbani hupati thawabu la zinakuwa ndogo na kama umefanya makusudi swala inaadhiniwa msikiti wewe unasali kwenye store yako ya mkaa unapata dhambi unless kuwe na dharura yoyote ile. Katika kipindi kama hichi mafundisho sasa ya Mtume wetu rehma na amani ilipaswa misikiti ifungwe watu wasalie nyumbani kutokana na hali iliyopo hadi hapo itakapokaa sawa. Lakini ni makosa na kama wewe muislam unasema kwenda kuswali jamaa msikitini ni unafiki nasi unapata madhambi na utubie kwa mola wako toba iliyo ya kweli. Inna Allah Ghafur-rRahiim.

Hoja yangu hiyo nimeitoa katika Mukhtaza huu wa Dharura hii ya Janga la CORONA na sijasema kuwa Watu kamwe wasiwe wanaenda huko Makanisani au Misikitini. Na usisahau hata Mimi pia ni Muumini tena mzuri tu na pengine yawezekana hata kuliko Wewe ila siungi mkono kwa sasa Watu Kukusanyika huko katika Nyumba za Ibada. Siku nyingine uwe unayaelewa Kwanza Maelezo ya Mtu vyema kabla hujaanza Kukurupuka Kumjibu Kihisia Hasi kama ulivyofanya sasa sawa?
 
Hoja yangu hiyo nimeitoa katika Mukhtaza huu wa Dharura hii ya Janga la CORONA na sijasema kuwa Watu kamwe wasiwe wanaenda huko Makanisani au Misikitini. Na usisahau hata Mimi pia ni Muumini tena mzuri tu na pengine yawezekana hata kuliko Wewe ila siungi mkono kwa sasa Watu Kukusanyika huko katika Nyumba za Ibada. Siku nyingine uwe unayaelewa Kwanza Maelezo ya Mtu vyema kabla hujaanza Kukurupuka Kumjibu Kihisia Hasi kama ulivyofanya sasa sawa?



Ninachokijua tu ni kwamba ukiwa na Imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu / Allah hata ukisalia Sebuleni au Chumbani Kwako au Bustanini Kwako au hata Stoo basi Dua yako inakubaliwa na unabarikiwa vizuri tu. Huko kwenda Makanisani na Misikitini mara nyingine huwa ni Mbwembwe tu zilizochanganyika na Unafiki mwingi ndani yake.

Kauli yako hiyo hapo, wewe mnafiki huna elimu yoyote ya dini, mwenye elimu ya dini hawezi kuandika uliyoyaandika.
 
Ninachokijua tu ni kwamba ukiwa na Imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu / Allah hata ukisalia Sebuleni au Chumbani Kwako au Bustanini Kwako au hata Stoo basi Dua yako inakubaliwa na unabarikiwa vizuri tu. Huko kwenda Makanisani na Misikitini mara nyingine huwa ni Mbwembwe tu zilizochanganyika na Unafiki mwingi ndani yake.

Kauli yako hiyo hapo, wewe mnafiki huna elimu yoyote ya dini, mwenye elimu ya dini hawezi kuandika uliyoyaandika.

Kuna tofauti na Mimi kutokuwa na Elimu hiyo ya Kidini na Wewe kuwa nayo lakini bado haijakusaidia na umebakia kuwa Juha Kiimani.
 
Waafrica tunaweka siasa hata kwenye mambo ya majanga.......wacha tupukutuke ili tutie adabu......

eti makanisa yasifungwe sababu yanaombea Corona.....yale yale ya Kibwetele.
Ukishapukutika utatiaje adabu bwashee?!
 
Back
Top Bottom