Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Lakini si serikali ipo vipindi vyote mkuu Yoda?

Wanasiasa watakuja na kuondoka, lakini serikali haiondoki!

Labda tuseme tu kwamba nchi zetu hizi hazina taratibu nzuri za uendeshaji serikali.

Wanasiasa wanapoondoka, hawaondoki na serikali wanapomaliza ngwe zao au wanapoachishwa kazi.

Kama mwanasiasa kakuta shirika linajiendesha vizuri na linaingiza faida, ataanzia wapi kuliua?
 
Watu ndio wanaendesha serikali. Na ndio wanaamua kipi kinafanyika na kipi hakifanyiki kwa muda upa.
Biashara haiwezi kuongozwa kwa katiba, ni maamuzi yanayotegema hali halisi ya wakati husika.
Huko kwenye nchi zilizoendelea ndio huwezi kukuta kabisa serikali zake zikifanya biashara.
 
Unadhani nakukatalia hayo unayoyasema kuhusu hawa viongozi wetu kutojali? Ninakuelewa na kukubaliana nawe kabisa juu ya hilo.

Lakiniiii, hoja ya msingi hapa ni:je hawa ndio viongozi wa mfano? Ndio viongozi wazuri katika kuendesha serikali?

Hata huko kwa wafanya biashara, wewe huoni watu wakifilisika kutokana na kuwa na tamaa ya kuoa wake (huu ni mfano tu, wa aina ya udhaifu wa binaadam).

Kwenye siasa pia hali ni hiyo hiyo. Tukipata viongozi wenye 'commitment' na dhamira ya kweli ya kuliinua taifa letu, kwa nini mashirika yake yasifanye vizuri?
 
Najua serikali haifanyi biashara hizi za kuuza pipi.

Lakini, hata huko unakosema walikoendelea, kuna vitu ambavyo serikali haiwezi ikajitoa moja kwa moja na kuwaachia watu binafsi ndio waendeshe shughuli hizo.
Hawa wachina hadi juzi juzi walikuwa wamejifungia ndani. Mashirika yao mengi yalikuwa ya kiserikali, yakiendesha shughuli na kutoa huduma kwa wananchi wake.
Leo hii mashirika hayo ndiyo yanayofanya shughuli dunia nzima! Na ndiyo yaliyoijenga China na kuibuka hivi sasa kuwa kama ilivyo.
 
Katika suala la biashara sio viongozi wetu Tanzania tu, serikali zote duniani zinakabiliwa na hali hiyo hiyo.Nchi nyingi zilizopiga hatua kwa haraka ziligundua haya mapema zikaachana na zile biashara zinazoweza kufanywa kwa ufanisi na sekta binafsi.
 
Sasa si hata huko kukusanya kodi uliona wakiwa wanashindwa?

Sikubaliani nawe kamwe juu ya hayo mawazo ya kusema "Tokea uhuru mpaka leo hakuna sehemu linapofanikiwa..., ni madudu tu kila siku."

Unachanganya mambo mengi hapa pengine bila kujua.

Kushindwa kwa mambo mengi yaliyofanyika hapa tokea uhuru sababu zipo nyingi sana, hata zisizohusu maamuzi ya serikali. Kama wewe huwezi kulitambua hilo, basi maana yake ni kwamba mawazo yako umeyagandisha sehemu moja tu, na huna uwezo wa kupambanua hali zinazohusiana katika kufifisha mafanikio.
Ni vigumu sana kujadili jambo na mtu wa aina hiyo.
 
Pia waliona mwelekeo wabdunia wakaona ni vyema sekta binafsi iwe ni mshirika na sii adui kama ilivyokuwa kwetu.
Mkuu, unadhani hilo nalikataa? Silikatai kamwe, hali ndivyo ilivyo sasa duniani kote. Sekta binafsi inao mchango mkubwa sana katika taifa lolote, kama ilivyo kwa serikali kushiriki katika baadhi ya mambo kufuatana na hali ya nchi ilivyo.
 
Sio kwamba serikalini hakuna watu wenye ubunifu, ila hakuna mazingira yanayohamasisha waajiriwa kuwa wabunifu kila kitu mpaka bodi ya wakurugenzi ikae na maazimio ya kikao lazima yapelekwe kwa waziri ili yapatiwe solution
Sasa nikuulize.
Kuna katazo gani huko serikalini kufanya ubunifu?

Huo muundo ndio unaokataza ubunifu?

Mimi naona kinyume kabisa, kwa sababu kama Bodi ni ya watu waelewa na inafanya kazi vizuri, ubunifu huo ndio wangekuwa wanauchochea kabisa?

Wewe unaangalia uongozi mbaya, halafu unahitimisha kwamba hapawezi kuwepo na uongozi unaoweza kuendesha mashirika haya kwa ufanisi.
 
Mabadiliko makubwa yanakuja.. Serikali itabaki na huduma tuu, biashara zitapelekwa sekta binafsi
 
Kuanzia mwaka 1950 hadi 1980 China ilikuwa na uchumi wa kijamaa haswa. Ule ujamaa wa serikali kumiliki kila biashara,rasilimali na kila kitu. Hapo mwanzoni waliua hadi matajiri viwanda vyao na ardhi zao zikachukuliwa na serikali ya Kikomunisti ya Mao.

Kipindi cha mapinduzi ya kiutamaduni kati ya mwaka 1966 hadi 1976 Hadi CocaCola zilipigwa marufuku China, suti za ulaya ilikuwa marufuku, kila kitu ilibidi ununue cha nchini kwako na sio kutoka kwa mabeberu.
Na sisi tukiamua kuua ushindani namna hiyo kwa sekta binafsi ya ndani ili biashara za serikali zifanikiwe tunaweza kufanikiwa ila kwa sekta binafsi ya nje haiwezekani kwa sababu hatuna soko la watu billion moja kama china kuweza kuuza kila kitu chote humu ndani mataifa mengine watakapoanza kutuwekea vikwazo na wao.
 
zikaachana na zile biashara zinazoweza kufanywa kwa ufanisi na sekta binafsi.
Haswaaaa.
Umetumia maneno ninayokubaliana nayo moja kwa moja.
Serikali haiwezi ikajiingiza kwenye kila aina ya biashara.

Lakini hilo sio sawa na kusema kwamba hakuna maeneo, kwa sababu mbalimbali, isipoweza kushiriki katika biashara yoyote.
 
Na ndio maana China haindelei kulinganisha na rasilimali ilizo nazo kutokana na mifumo mibovu kama hii ya Serikali ki hodhi kila kitu na kufanya Biashara.

Kutokana na mambo hayo itachukua Miaka 1000 China kuizidi U.SA huku kimsingi kutoka na Rasilimali zake pamoja na Idadi kubwa ya watu ambao ni Mara 4 ya Idadi ya Watu wa U.S.A alitakiwa awe amisha mpita U.S.A kiuchumi.
 
Ni ukweli ulio bayana kuwa Serikali imeshindwa kufanya biashara na nibusara waukubali ukweli huu ili either waiachie private sector ifanye biashara wao wabaki kukusanya kodi au washirikiane na private sector through PPP.
Historia siku zote ni mwalimu. Tulikuwa na mashirika ya umma lukuki kama - NASACO, TRC, UFI, URAFIKI, TANGANYIKA PECKASE, ALAF, UDA , ATC ,TRC etc yote hayo tuliyazika kaburini kutokana na mapungufu ya namna ambavyo Serikali haiwezi kuendesha biashara.
 
Ubunifu huwa unachochewa na faida ambayo inaenda kwa mmiliki na wafanyakazi wake moja kwa moja. Shirika la serikali likipata faida au hasara mshahara wa mkuregenzi na wafanyakazi ni ule ule unaopangawa na utumishi au kuongezwa kwa pamoja na watumishi wengine wote mei mosi. Kwa mantiki hiyo kwa nini Mkuregenzi wa shirika la serikali afanye juhudi yoyote kuongeza ubunifu??
 
Mkuu Yoda, hakuna serikali yoyote wakati huu 2021, hata ile ya kijana Kim Jong Un, wala Cuba, wanaofikiria kurudi kwenye enzi za miaka hiyo, sembuse sisi?

Lakini wakati huo huo, hata hawa Wamarekani, Waingereza, au Wajerumani, hakuna serikali inayokataa kata kata kuwa na mchango wowote katika uendeshaji na usimamizi wa baadhi ya maswala yanayogusa maisha ya wananchi wao moja kwa moja.
 
Aiiseee, wewe unaishi dunia yako kama unaona hivyo ulivyoandika.
Sina lolote la kujibu hapo.
 
Suala la muhimu zaidi ni siku ya uzinduzi kukata utepe na kujipongeza....huko kwingine ni juu yenu🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…