Mada muhimu kweli kweli, lakini wachangiaji wanachungulia tu na kupita zao! Wanatafuta mada za CCM na CHADEMA!
Mimi sikubaliani na wewe juu ya hiyo dhana ya serikali haifanyi biashara.
Usiifanye kuwa 'dogma', au kama kitu ulichokaririshwa.
Hata kama ulisikia ikisemwa hivyo, kwa nini usiweke muda ujaribu kutazama uhalisia na ukweli wake ukoje?
Sasa mimi nakushauri uanze kulitazama hilo kwa jicho la pili; acha kufumba jicho moja, yafungue yote mawili ili upate picha nzuri.
Ni hivi: kuna kizuizi gani kinachofanya serikali isiweze kufanikisha kuendesha miradi hiyo yote uliyoitaja?
Kwani haina watu wenye uwezo wa kuifanya. Kama wapo, ni nini kinazuia wasifanye hiyo kazi kwa ufanisi?
Na kama hawapo, serikali haiwezi ikamwajiri, ndiyo kuajiri kampuni kwa mkataba inayoweza kuendesha shughuli hizo kwa ufanisi? Sijasema serikali ibinafsishe, kama wewe unavyotaka.
Lakini la muhimu hapa ninalolisisitiza, ni hii dhana potofu ya kwamba serikali haiwezi kufanya mambo yake kwa ufanisi.
Kuna sababu zipi...., hizo sababu haziwezi kuondolewa?
Kila mara imekuwa ni kutafuta visingizio tuuu kwa kushindwa tu kutimiza wajibu mliopewa kuutimiza.
Hapa ndipo nilipopenda Magufuli apafanyie udikteta wake haswa haswa...! Hali ingebadilika tu baada ya muda.
Haya mashirika makubwa ya ujenzi na mengine toka China tunayoona yametapakaa duniani kote, mbona haya yalikuwa ni mashirika chini ya serikali?
Wao waliweza vipi?