Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Mkuu, ahsante kwa mchango wako, lakini dhana hii ni potofu kabisa.

Kwa nini watu wote hao walioko serikalini wote wawe hawana ubunifu, ila hawa wengine ndiko kuwe na wabunifu?

Umetoa mfano huo wa TTCL, ukalinganisha na TIGO, VODA na HALOTEL - hivi kweli unaweza kusema kwamba wafanyakazi walioko TTCL hawana ubunifu kama hao walioko kwenye mashirika hayo? Ushahidi wa hili ni upi?

Serikali wangetaka mashirika yao yafanye vizuri ingewezekana sana!

Basi tu, hatujapata viongozi ambao wana nia ya kuyafanya haya mashirika yawe imara. Ni mambo ya uzembe tu na kukosa usimamizi unaotakiwa kuyawezesha mashirika yafanye kazi vizuri.
Kaka unajaribu kubadili fikra kuwa uhalisia. Mfumo wa serikali kufanya biashara ulifeli Dunia nzima miaka ya '80
Na nchi za ulaya zote walianza kuamini na kusapoti sekta binafsi kabla ya Karne ya 10.
Kampuni kubwa duniani NI za watu binafsi. Zio za ndege Wala za vinywaji.
Tanzania tunawatu wehu kweli. Simba inaajili kocha na wachezaji kutoka kila Kona wenye vipaji ndio wa kapata mafanikio.
Nmb manajment yote wazungu wenye vipawa vya usimamizi wa fedha na taaluma ndio maana imesimama.
Sisi wasomi wetu NI wasaka fursa sio talented. Mtu anakipawa Cha kuwa dokta anasoma uinjinia Sasa akija kwenye utendaji Hana Cha kuongezsa zaidi ya aliyoyasoma pindi akiwa chuo.
 
Unadhani nakukatalia hayo unayoyasema kuhusu hawa viongozi wetu kutojali? Ninakuelewa na kukubaliana nawe kabisa juu ya hilo.

Lakiniiii, hoja ya msingi hapa ni:je hawa ndio viongozi wa mfano? Ndio viongozi wazuri katika kuendesha serikali?

Hata huko kwa wafanya biashara, wewe huoni watu wakifilisika kutokana na kuwa na tamaa ya kuoa wake (huu ni mfano tu, wa aina ya udhaifu wa binaadam).
Kwenye siasa pia hali ni hiyo hiyo. Tukipata viongozi wenye 'commitment' na dhamira ya kweli ya kuliinua taifa letu, kwa nini mashirika yake yasifanye vizuri?
Kifupi wanaofanikiwa kwenye biashashara NI watu wenye vipawa vya UBUNIFU na kufanya biashara na sio wasomi. Wao ndio hubuni mbinu mpya za kutafuta masoko, kuvutia wateja na kusimAmia mitaji na kuchungulia fursa. Serikali haiwezi kuajili watu hao. Huajili kwa kuangalia vyeti na vyama vyao vya siasa.
Bodi za wakurugenzi kwa Kampuni kubwa huwa NI watu wenye hisa kubwa kwenye kampuni husika. Ikitokea limefilisika NI wao huwa wa kwanza kuumia.
Ila bodi ya wakurugenzi kwa mashirika ya Uma NI wateule wa Raisi au waziri. Wengi NI wanasiasa wastafu. Hawajui lolote kuhusu biashara na uenda uko kupokea posho tu sio kushauri.

Sio biashara tu vitu vya serikali vyote Hadi shule, hospital huduma NI mbovu kwa kukosa UBUNIFU.
 
Kosa Liliazna alipofanyiwa zengwe max maliopo, alionekana anafaidi sana marehemu dikteta alikua hapendi sekta binafsi

Max maliopo aliuwezea sana mfumo wa kie-lectronic wa mwendokasi
 
Unadhani nakukatalia hayo unayoyasema kuhusu hawa viongozi wetu kutojali? Ninakuelewa na kukubaliana nawe kabisa juu ya hilo.

...

Kwenye siasa pia hali ni hiyo hiyo. Tukipata viongozi wenye 'commitment' na dhamira ya kweli ya kuliinua taifa letu, kwa nini mashirika yake yasifanye vizuri?

Jibu la hoja yako lipo kwenye hiyo aya ya mwisho.

Kwa kifupi kabisa, pitia historia ya uchumi ya Tanzania tangu kupata uhuru kisha toa pendekezo la uhakika jinsi Tanzania itakavyoweza kuwapata hao “viongozi wenye commitment na dhamira ya kweli ...” na kuwapa madaraka stahiki ya uongozi wa mashirika ya serikali.

Ukitoa jibu thabiti kuhusu changamoto hilo basi hakika hoja yako ya serikali kufanya biashara kwa ufanisi/ushindani haitakuwa na ubishi.

Nyerere alishindwa na alieleza kuwa tatizo kubwa lililoua mashirika ya umma ni “kutotilia umuhimu mkubwa kwenye suala la management”. Ukweli ni kwamba isingewezekana kwa jinsi serikali ilivyokuwa ikiendeshwa huku malengo ya kisiasa yakiwa na kipaumbele namba moja ilhali yakikinzana na ya kibiashara/kiuchumi mara kwa mara.
 
Kifupi wanaofanikiwa kwenye biashashara NI watu wenye vipawa vya UBUNIFU na kufanya biashara na sio wasomi. Wao ndio hubuni mbinu mpya za kutafuta masoko, kuvutia wateja na kusimAmia mitaji na kuchungulia fursa. Serikali haiwezi kuajili watu hao. Huajili kwa kuangalia vyeti na vyama vyao vya siasa.
Bodi za wakurugenzi kwa Kampuni kubwa huwa NI watu wenye hisa kubwa kwenye kampuni husika. Ikitokea limefilisika NI wao huwa wa kwanza kuumia.
Ila bodi ya wakurugenzi kwa mashirika ya Uma NI wateule wa Raisi au waziri. Wengi NI wanasiasa wastafu. Hawajui lolote kuhusu biashara na uenda uko kupokea posho tu sio kushauri.

Sio biashara tu vitu vya serikali vyote Hadi shule, hospital huduma NI mbovu kwa kukosa UBUNIFU.

Najua serikali haifanyi biashara hizi za kuuza pipi.

Lakini, hata huko unakosema walikoendelea, kuna vitu ambavyo serikali haiwezi ikajitoa moja kwa moja na kuwaachia watu binafsi ndio waendeshe shughuli hizo.
Hawa wachina hadi juzi juzi walikuwa wamejifungia ndani. Mashirika yao mengi yalikuwa ya kiserikali, yakiendesha shughuli na kutoa huduma kwa wananchi wake.
Leo hii mashirika hayo ndiyo yanayofanya shughuli dunia nzima! Na ndiyo yaliyoijenga China na kuibuka hivi sasa kuwa kama ilivyo.
China wanafanya ubadhirifu kwenye mashirika ya umma wanachukuliwa hatua Kali, huku wapo na wanadunda mtaani

Ni Ujinga kila saa kutolea mfano wa china, Tanzania mtu anaiba na afanywi chochote kwa sababu tu ni kada wa chama na alikua mteule wa rais
 
View attachment 1764397

Umeona hapo ☝️mwaka jana walitengeneza faida ya £671.2 million.

Yes kuwekeza 80% back ni sera yao kwa sababu kampuni ni 100% mali ya serikali hawana interest na dividend bali kutoa merit good zenye ubora na kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Ndio maana wanarudisha kwenye kujiboresha.

View attachment 1764398

Tazama hapo ☝️ juu tena utaona mwaka jana wamelipa £526.6 million ya madeni ya grant. Na bado wanadaiwa zaidi ya £1.5 billion za grants.

Kuwa mali ya serikali aina maana wanaendeshwa kwa subsidies. Grants ni sources of finances za kawaida sana nchi za wenzetu, hata taasisi binafsi zinapata provided serikali inataka kusaidia sector fulani, wanao qualify kwenye hiyo industry can apply.

Acha kumsikiliza huyo jamaa alieni quote anaunga unga tu ubishi wala ajapitia hiyo statement yenyewe aliyoileta.

PS. British Airways sio mali ya UK kwa sasa inamilikiwa na ‘International Airline Group’ (AIG) shirika lilisojaliwa Spain.

Hiyo 526.6 ni kipato siyo malipo. Ndiyo maana imejumlishwa na haikutolewa kwenye mahesabu yao. But that is beside the point. Swali la muhimu ni je unaelewa kwamba hela za serikali ni hela za walipa kodi?
 
... Net Group Solutions waliopewa Tanesco na Mkapa waliifikisha wapi?
Net group walipewa NMB na ndio wameifanya Nmn kujisimamia, kujiendesha kwa faida, kulipa Kodi na kufadhili sekta za afya na ELIMU kwa kuwapa zaidi ya bilion moja kila mwaka kununulia vitanda au dawati
 
China wanafanya ubadhirifu kwenye mashirika ya umma wanachukuliwa hatua Kali, huku wapo na wanadunda mtaani

Ni Ujinga kila saa kutolea mfano wa china, Tanzania mtu anaiba na afanywi chochote kwa sababu tu ni kada wa chama na alikua mteule wa rais
Watu sio waelewa kabisa kuhusu uchumi. China ilikuwa masikini wa kutupwa mpaka miaka ya 1980'. Wakati huo Hong Kong iliyokuwa chini ya mwingereza ikikua kwa Kazi ya ajabu. Mwaka 1980 China ilifanya mabadiliko makubwa ya Sera za kiuchumi sawa na Urusi. Kuruhusu sekta binafsi na uwekezaji wa magharibi kulipelekea China kuwa taifa kubwa ulimwenguni. Watu binafsi wamekuwa matajili wakubwa. NI nchi yenye mabilionea wengi Sasa kuliko nchi yoyote duniani. Huko ndio kimalik kwa sekta binafsi
 
Mfano mzuri mwendokesa mwaka 2016 na 2017 Max malipo a private sector alikua anatoa huduma za kuuza tiketi kielectronic, mwanzon mwa 2018 serekali ikasitisha mkataba wake anapewa ttcl since then haya madudu ndo yakaanza
 
Hiyo 526.6 ni kipato siyo malipo. Ndiyo maana imejumlishwa na haikutolewa kwenye mahesabu yao. But that is beside the point. Swali la muhimu ni je unaelewa kwamba hela za serikali ni hela za walipa kodi?
Ndugu Grant funding ni jambo la kawaida nchi za wenzetu. Mfano kwa Tanzania ukipekuwa utakuta asilimia kubwa ya FDI za wawekezaji wa kati kutoka UK sources za investment funds ni government grants.

Serikali yao inaweza kuwa na sera za kusaidia sector fulani ya supply chain au area of concern za kibiashara Tanzania. Grants za namna hiyo zipo mpaka kesho provided unaishi huko na una permanent residency (hizo ni kwa raia wao tu) na kila mwaka mara mbili wanatoa update kama umejiunga na U.K aid. 👇

Ndio maana unaona wawekezaji wakubwa Tanzania ni UK citizens, lakini ni grants ambazo unalipa kama umekopa bank tofauti riba ni ndogo sana, tatizo watanzania wanaoshi huko na wenye makaratasi hawana business ideas or can’t write convincing business proposals or are just not bothered kwa wale wachache wanaojua.

Hizo grants za TfL na zenyewe zina minajili hiyo hiyo kama ulivyosoma asilimia kubwa ya grants zao ni kupitia cross-rail grant funding 👇

Hiyo fund ni kuchochea uwekezaji wa reli biashara za serikali na private wote wapo entitled to apply but kuna malipo sio bure. Nonetheless not a subsidy by any means.

Ni sawa na kutaka kusaidia wakulima kupitia bank ya kilimo watu wanunue matreka ili kukuza kilimo kwa mikopo nafuu. Kutoa mbolea za ruzuku, mikopo ya vikundi kwa vijana, walemavu na akina mama kupitia mapato ya halmashauri.

Hiyo ndio mifano kwa standard zetu, but not subsidy. More like a fiscal policy tool through a third part.
 
Mada muhimu kweli kweli, lakini wachangiaji wanachungulia tu na kupita zao! Wanatafuta mada za CCM na CHADEMA!

Mimi sikubaliani na wewe juu ya hiyo dhana ya serikali haifanyi biashara.

Usiifanye kuwa 'dogma', au kama kitu ulichokaririshwa.

Hata kama ulisikia ikisemwa hivyo, kwa nini usiweke muda ujaribu kutazama uhalisia na ukweli wake ukoje?

Sasa mimi nakushauri uanze kulitazama hilo kwa jicho la pili; acha kufumba jicho moja, yafungue yote mawili ili upate picha nzuri.

Ni hivi: kuna kizuizi gani kinachofanya serikali isiweze kufanikisha kuendesha miradi hiyo yote uliyoitaja?

Kwani haina watu wenye uwezo wa kuifanya. Kama wapo, ni nini kinazuia wasifanye hiyo kazi kwa ufanisi?

Na kama hawapo, serikali haiwezi ikamwajiri, ndiyo kuajiri kampuni kwa mkataba inayoweza kuendesha shughuli hizo kwa ufanisi? Sijasema serikali ibinafsishe, kama wewe unavyotaka.

Lakini la muhimu hapa ninalolisisitiza, ni hii dhana potofu ya kwamba serikali haiwezi kufanya mambo yake kwa ufanisi.

Kuna sababu zipi...., hizo sababu haziwezi kuondolewa?

Kila mara imekuwa ni kutafuta visingizio tuuu kwa kushindwa tu kutimiza wajibu mliopewa kuutimiza.

Hapa ndipo nilipopenda Magufuli apafanyie udikteta wake haswa haswa...! Hali ingebadilika tu baada ya muda.

Haya mashirika makubwa ya ujenzi na mengine toka China tunayoona yametapakaa duniani kote, mbona haya yalikuwa ni mashirika chini ya serikali?
Wao waliweza vipi?
Mchangiaji hujamtendea haki mtoa mada. Unanamtaka ataje sababu za kwanini serikali inashindwa kuendesha biashara badala ya kujikita kwenye maoni yake yanayotokana na uzoefu anaouona juu ya serikali kuendesha biashara.

Ukweli ni kwamba kutokujua chanzo cha tatizo haimaanishi kutokuwepo kwa tatizo. Ukweli ni kwamba kubainisha sababu za serikali kushindwa kuendesha biashara si kazi rahisi hivyo bali kunahitaji utafiti wa kina na ni wajibu wa serikali yenyewe na si mtoa mada.

Mtoa mada yeye ni shuhuda tu wa matatizo yanayojitokeza katika biashara zinazoendeshwa na serikali. Mara nyingi matizo hujidhihirisha yenyewe na kwahiyo kila mwenye macho na akili anaweza kuyaona kama mtoa mada anavyoyaona kwenye biashara za serikali

Nilidhani ingekuwa vizuri kukubaliana na mtazamo wa mtoa mada kwamba serikali haiwezi kuendesha biashara badala kumtaka ataje sababu jambo ambalo ni nje ya uwezo wake.
 
Ndugu Grant funding ni jambo la kawaida nchi za wenzetu. Mfano kwa Tanzania ukipekuwa utakuta asilimia kubwa ya FDI za wawekezaji wa kati kutoka UK sources za investment funds ni government grants.

Serikali yao inaweza kuwa na sera za kusaidia sector fulani ya supply chain au area of concern za kibiashara Tanzania. Grants za namna hiyo zipo mpaka kesho provided unaishi huko na una permanent residency (hizo ni kwa raia wao tu) na kila mwaka mara mbili wanatoa update kama umejiunga na U.K aid. 👇

Ndio maana unaona wawekezaji wakubwa Tanzania ni UK citizens, lakini ni grants ambazo unalipa kama umekopa bank tofauti riba ni ndogo sana, tatizo watanzania wanaoshi huko na wenye makaratasi hawana business ideas or can’t write convincing business proposals or are just not bothered kwa wale wachache wanaojua.

Hizo grants za TfL na zenyewe zina minajili hiyo hiyo kama ulivyosoma asilimia kubwa ya grants zao ni kupitia cross-rail grant funding 👇

Hiyo fund ni kuchochea uwekezaji wa reli biashara za serikali na private wote wapo entitled to apply but kuna malipo sio bure. Nonetheless not a subsidy by any means.

Ni sawa na kutaka kusaidia wakulima kupitia bank ya kilimo watu wanunue matreka ili kukuza kilimo kwa mikopo nafuu. Kutoa mbolea za ruzuku, mikopo ya vikundi kwa vijana, walemavu na akina mama kupitia mapato ya halmashauri.

Hiyo ndio mifano kwa standard zetu, but not subsidy. More like a fiscal policy tool through a third pa

Mbona hujibu swali nililokuuliza? Je unaelewa kwamba hela za serikali ni hela za walipa kodi?
 
Mbona hujibu swali nililokuuliza? Je unaelewa kwamba hela za serikali ni hela za walipa kodi?
5DCBFFC1-1097-4D47-8010-4A58A0CFE053.jpeg

Nilishakuwekea jibu hapo ☝️hizo grants ni mkopo kutoka serikalini wanalipa sio bure. Umeona mkopo wa £1.3 billion kwa jiji GLA (greater London authority) inayoendesha TfL; na TFL yenyewe imepokea £750 directly na umeambiwa kabisa ni loan from DfT (Department for Transport; wizara ya uchukuzi).

Kama umesoma biashara utakuwa unaelewa sources of investment finance; government grants ikiwa moja wapo na wanufaika includes private organization.

Anyway mada inasema serikali aiwezi endesha biashara na mabeberu hawafanyi ivyo; jambo ambalo si la ukweli.
 
China wanafanya ubadhirifu kwenye mashirika ya umma wanachukuliwa hatua Kali, huku wapo na wanadunda mtaani

Ni Ujinga kila saa kutolea mfano wa china, Tanzania mtu anaiba na afanywi chochote kwa sababu tu ni kada wa chama na alikua mteule wa rais
Hayo mashirika ya china hayaendeshwi kwa malengo ya kisiasa bali kwa mlengo wa biashara
 
Ethiopia Airlines ilikuwa Shirika pekee la ndege la Ethiopia kati ya 1950 hadi 2002. Unahitaji kuwa TANESCO ndio ushindwe kujijenga na uendelee kupata hasara ukiwa mwenyewe sokoni.

Usiongelee IPTL aliyekuwa supplier tu na ambaye ni dili la wanasiasa.Ongelea TANESCO ambayo haijawahi kutoka mikononi mwa serikali, haijwahi kupata faida na huduma zake ni tia maji tia maji tu siku zote. Na vigogo wa serikali hawataki kusikia suala la sekta binafsi kwenye umeme!!!

Kama una mashaka na Huduma kutoka kampuni binafsi nenda Agha Khan, Regency, Kairuki. Nenda Feza, St Mary's, ISM, St Anthony. Angalia wanafunzi wanaotoka shule za kata na hao kutoka st st, Angalia usafiri wa dalaldala za binafsi ulivyo na uhakika kuliko hizo daladala za mwendokasi, Angalia usafiri wa mikoani kwa mabasi ambako serikali haina hata basi moja la abiria.

Serikali iliwaindoa Maxmalipo kwenye mwendokasi,wakati huu tiketi zinachanwa na huduma ya kadi imekufa. Sasa hivi ni miaka miwili hilo dude lao la E-government bado liko linajenga mfumo wa kielectronic.Two damn years!!!.
Mkuu Yoda, tumetoka huko nyuma vizuri sana; lakini nikiri mchango wako huu hapa hukuupa uzito stahiki.

Sikuona la kujibu kwenye mchango huu hapa.

Nadhani 'fatique' uchovu wa mjadala umechukua nafasi yake.

'Anyway', bado naheshimu uungwana wa michango yako.
 
Hayo yalifanywa kwenye TRC ,kuna tija ilipatikana?

Wakati wa JK alijaribu kwa kuleta watanzania waliokuwa nje ya nchi kwenye sekta binafsi kama TIC,NSSF,NHC nk nk walijitahidi lakini mwendazake alivyokuja akadai hawezi lipa salary kubwa na hadi leo hii mashirika yamejifia huko

Tukubali serikali iwe na hisa tuu ila shughuli za uendeshaji zifanywe na sekta binafsi tena kipaombele iwe watu wa ndani ndio wawe investors
Unajua mkuu 'Opportunity', binafsi sina tatizo kabisa na serikali kuwaachia wanaoweza waendeshe mashirika hayo kwa ufanisi, sina tatizo kabisa juu ya hilo, mradi nchi/wananchi wanafaidika na huduma nzuri na nchi inapata haki yake toka kwenye mashirika hayo.

Sasa basi, ukikaa chini na kufikiri, serikali inayoshindwa hata kuendesha kishirika kama UDA tu, itakuwa na uwezo gani wa kuhakikisha nchi inafaidika toka kwa hawa tunaowaachia waendeshe? Viongozi ambao kila ukiangalia wana njaa ya kutisha sana kujinufaisha wao zaidi kuliko manufaa yanayopatikana ili wananchi na wao wafaidike.

Tatizo ndilo hilo, na sijui kama wewe una suluhisho juu ya hali hiyo.
 
Hayo mashirika ya china hayaendeshwi kwa malengo ya kisiasa bali kwa mlengo wa biashara
Basi sawa, kwa nini isiwe hivyo hata hapa kwetu?

Nadhani tunachanganya mambo kidogo hapa wakati tunaposema "malengo ya kisiasa". siasa gani hiyo?
Mimi naiita kwa "malengo ya kifisadi" siyo siasa hasa!
 
Hao(sekta binafsi) hatuwaachii waendeshe tu kama wanavyoendesha TICTS bandarini. Serikali ikiamua kuindoa ATCL na mwendokasi mikononi mwake hayo mashirika yanakuwa kampuni binafsi kabisa za mtu mmoja au wanahisa wenye hisa nyingi waliokidhi vigezo vya kuuziwa.

Serikali inabaki kukusanya kodi au ushuru tu kama inavyokusanya kwenye mabasi ya watu binafsi mikoani, daladala na inavyokusanya fastjet na precision airways na kusimamia sheria.
Nchi kufaidika ni kukusanya kodi yake inavyotakiwa baada ya kuyauza hayo makampuni katika mchakato wa wazi na unaozingatia vigezo na kanuni, kama hata hiyo kazi yake ya msingi haiwezi basi iombe isaidiwe.
Unajua mkuu 'Opportunity', binafsi sina tatizo kabisa na serikali kuwaachia wanaoweza waendeshe mashirika hayo kwa ufanisi, sina tatizo kabisa juu ya hilo, mradi nchi/wananchi wanafaidika na huduma nzuri na nchi inapata haki yake toka kwenye mashirika hayo.

Sasa basi, ukikaa chini na kufikiri, serikali inayoshindwa hata kuendesha kishirika kama UDA tu, itakuwa na uwezo gani wa kuhakikisha nchi inafaidika toka kwa hawa tunaowaachia waendeshe? Viongozi ambao kila ukiangalia wana njaa ya kutisha sana kujinufaisha wao zaidi kuliko manufaa yanayopatikana ili wananchi na wao wafaidike.

Tatizo ndilo hilo, na sijui kama wewe una suluhisho juu ya hali hiyo.
 
Serikali haiwezi kufanya biashara. Hasa hizi za kwetu.

Kama Waziri Mkuu anaona madudu kwenye mradi wa mwendokasi.

Kama Serikali imeshindwa kufanya miradi ya reli ya Kati na TAZARA, vivuko, ndege na sasa Mabasi ya mwendokasi kujiendesha ni wakati wa kubadili mtazamo.

Wajiondoe waruhusu sekta binafsi iviendeshe yenyewe ichukue Kodi na idili na kutoa huduma kwa wananchi.

Serikali haitakiwi kufanya biashara. Inajiongezea mzigo usio na sababu. Ingawa,lazima waamue kufanya biashara na taasisi au makampuni binafsi yenye kuaminika.
Yale mambo ya kubinafsha ATC kwa SA Airline au kuwapa reli ya kati wale wahindi ambao hawakuwa na lolote la kuongeza ni uhujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom