KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Eeenh Heeee, mchango wako 'serious', lakini ulivyouwasilisha imenibidi nicheke, hasa huko mwisho kwa 'dokta kuwa injinia"!Kaka unajaribu kubadili fikra kuwa uhalisia. Mfumo wa serikali kufanya biashara ulifeli Dunia nzima miaka ya '80
Na nchi za ulaya zote walianza kuamini na kusapoti sekta binafsi kabla ya Karne ya 10.
Kampuni kubwa duniani NI za watu binafsi. Zio za ndege Wala za vinywaji.
Tanzania tunawatu wehu kweli. Simba inaajili kocha na wachezaji kutoka kila Kona wenye vipaji ndio wa kapata mafanikio.
Nmb manajment yote wazungu wenye vipawa vya usimamizi wa fedha na taaluma ndio maana imesimama.
Sisi wasomi wetu NI wasaka fursa sio talented. Mtu anakipawa Cha kuwa dokta anasoma uinjinia Sasa akija kwenye utendaji Hana Cha kuongezsa zaidi ya aliyoyasoma pindi akiwa chuo.
Mkuu, kama unanielewa vizuri, mimi sikatai ushiriki wa sekta binafsi sehemu yoyote katika biashara. Sikatai kabisa.
Ila naomba unielewe: unavyoliweka hapa wazo lako, ni kama huko kwenye sekta binafsi biashara hazianguki, na kana kwamba watu walioko huko ni kama malaika wenyewe walioshuka toka mbinguni.
Hali haipo hivyo hata kidogo
Na kwa maoni kama uliyotoa hapa, sijui unashindwa kitu gani kuhitimisha kabisa kwamba hata serikali yenyewe inafaa tuiondoe, tuwape sekta binafsi waiendeshe!
Labda nikutahadharishe kidogo unaponogewa na fikra zinapotiririka ukiandika; kwa mfano unaandika: "Na nchi za ulaya zote walianza kuamini na kusapoti ekta binafsi kabla ya karne ya 10". Kweli? Histyoria hii unayo? Na una uhakika nchi zote hizo hakuna kinachofanywa na serikali katika baadhi ya mashirika katika nchi hizo, badala ya kuiachia sekta binafsi ifanye, nchi zote za Ulaya?