Kwa nini serikali haiwezi kufanya biashara ambazo kupata faida ni muhimu kwa mafanikio kama sekta binafsi.
1.Serikali zinaongozwa na wanasiasa sio wafanyabiashara.Kawaida ya mwanasiasa ni kuangalia mambo kwa vipindi vifupi vifupi.Mwanasiasa anafanya mambo akiangalia uchaguzi unaofuata kwa mfano miaka mitano ijayo.
Haijalishi kama serikali inao watu wenye ujuzi wa biashara au inaweza kuchukua watu kutoka nje ya mfumo wake.Mara zote katika kuajiri,kuongeza mtaji, kutafuta soko n.k itatanguliza maslahi yake ya kisiasa kwanza na kile inachoamini ni sahihi kwake na lazima kifanyike.
Biashara zenye ufanisi huwa hazifanyiwi kwa mtindo huo wa serikali bali kwa kungalia uhitaji na ya hali ya upatikanaji bidhaa sokoni pamoja na bei.Kwa mtazamo huo kampuni binafsi inaamua objectively wakati huu niongeze au nipunguze wafanyakazi, nisikope tena, niongeze au nisoongeze bidhaa au huduma.Kampuni ya serikali haiwezi kuwa objectively hivi itakuwa subjectively siku zote ikisikiliza upepo wa kisiasa unapovuma.