Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Shirika la ndege na Umeme sio hata ya kimkakati. Ni mambo yanayofanywa na sekta binafsi vizuri kwa ufanisi mkubwa tu katika nchi nyingi.
Eeenh Heee, wachana na biashara ya ndege mkuu!

Siyo serikali wala binafsi, hiyo ni biashara ngumu sana popote pale.
Ni mambo yanayofanywa na sekta binafsi vizuri kwa ufanisi mkubwa tu katika nchi nying
Shirika lipi mkuu?
Hata hayo ya Kimarekani, yote ni tia maji, tia maji!
 
Sekta binafsi ndio solution sababu serikali kila kitu ni siasa hivyo biashara hawaziwezi.

Wauze hiyo company.
 
Makampuni binafsi ya Marekani ulinzi yanapata tenda za kufanya kazi za kijeshi kutoka serikali ya Marekani na nchi nyingine nyingi duniani. Iraq na Afghanistan kuna makampuni binafsi ya ulinzi ya Marekani yanafanya kazi za kijeshi.

Silaha na Vifaa vyote muhimu vya ulinzi vinavyotumiwa na US na hata hapa Tanzania ambao ni wanunuzi vimetengenezwa na makampuni binafsi.
 
Wale watu wanapenda kuona ATCL ikiendelea kuwa ya serikali ndio wamepika propoganda hii ya kwamba biashara ya ndege ni ngumu sana na kila shirika linapata hasara kwa muda mrefu.Huo ni uongo mtupu.

Ukiacha huu mwaka mmoja wa COVID mashirika binafsi ya ndege yamekuwa yanafanya biashara ya kawaida na nzuri tu inayowapa faida.

Hujiulizi kama shirika binafsi la ndege linapata hasara kwa miaka mitano mfululizo litaendeleaje kuwa hewani ??!
Eeenh Heee, wachana na biashara ya ndege mkuu!

Siyo serikali wala binafsi, hiyo ni biashara ngumu sana popote pale.

Shirika lipi mkuu?
Hata hayo ya Kimarekani, yote ni tia maji, tia maji!
 
Sababu zote mbili zinahusika.

Na ndio maana tunasema, hasa kwenye hiyo ya kwanza ya kutokuwa na moyo wa kufanikizsha shughuli toka kwa wafanyakazi..., kwani ni lazima iwe hivyo?

Hawa wasiokuwa na moyo wa kujituma wakiwa kazini; sasa wapo kazini kufanya nini?

Hata kama sio kazi ya biashara wanayofanya, si hata hiyo ya ufagizi tu watashindwa?

Msisitizo wangu ni huo huo; kwa nini iwe hivyo serikalini? Serikali haiwezi ikawa na wafanyakazi wanaopenda kazi zao na maendeleo ya nchi yao na wakafaidika na kazi zao wanazofanya? Kwa nini?
 
Sekta binafsi ndio solution sababu serikali kila kitu ni siasa hivyo biashara hawaziwezi.

Wauze hiyo company.


Mbona halmashauri ya jiji la London ndio ☝️linaendesha London under ground, asilimia kubwa ya mabasi London, Trams, trains na njia nyingine nyingi za usafiri.

Na tena njia za mabasi zikiaribika sio serikali inayolipia matengenezo wao, train serikali itajenga reli deni wanalipa wao; hakuna dezo.

Issue Tanzania ni management sio serikali kuendesha; isitoshe kuna huduma zingine serikali inazishikilia ili kuhakikisha unafuu au kuzipeleka mahala ambapo wawekezaji awataki kwenda. Nyie mkishaona serikali imewekeza ndio mnaibuka aiwezi kazi.
 
Nadhani hukuelewa maana yangu ya mfano huo.

Hakuna kampuni yoyote inayoweza kufanya shughuli kama hizo nchini kwao.
 
Serikali wabishi kwa sababu kuna raia wengi watapiga makelele imeuzwa na pia ikiendelea kubaki ya serikali kuna ulaji kwa baadhi ya watendaji pamoja na kuwepo kwa hasara!
Sekta binafsi ndio solution sababu serikali kila kitu ni siasa hivyo biashara hawaziwezi.

Wauze hiyo company.
 
Ndugu William Mshumbusi & Kalamu1;

1. Tutabishana sana lakini ukweli wa mambo ni kuwa, miradi (projects) zinazoendeshwa na kusimamiwa na serikali moja kwa moja huwa mwisho wa siku zinaishia kwenye massive failure kwa sababu ya kuingiza SIASA ZETU MBOVU na ambazo huzaa tatizo jingine la UONGOZI/MANAGEMENT mbovu zisizo na ubunifu lakini zenye nia ovu za kuteketeza (kuiba) mtaji na faida kidogo yote inayopatikana kutokana na shughuli za mradi huo kwa kushirikiana na wanasiasa (watawala) ambapo mwisho wa siku shirika/kampuni/mradi unakufa kifo cha kawaida kabisa...

2. Rejea mifano ya viwanda vyote vilivyojengwa wakati serikali ya awamu ya kwanza ya Nyerere, vyama vya ushirika SHIRECU, NYANZA, TARECU nk nk. Vyote hivi vilikufa kifo cha kawaida tokana na tatizo hili nililolieleza hapo juu...

Mifano mingine iliyo hai kabisa na inavyoendelea hata sasa ni; angalia TANESCO, NHC, MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YOTE ni shida tupu na yote yanajiendesha pasipo ufanisi huku watawala wa kisiasa wakiyaingilia na SIASA ZAO MBOVU na kuyavuruga vuruga kiasi cha kuyafanya yajiendeshe kwa hasara kubwa na kushindwa Ku - deliver kwa wateja wao...

Ndo kusema kuwa, ishu siyo nchi kukosa wataalamu wa nyanja zote i.e management, uchumi, fedha nk bali ni SIASA CHAFU na UONGOZI WA HOVYO WA TAIFA HILI..

3. Sasa ili ku solve tatizo hili sisi kama nchi ni lazima kujengwa kwa taasisi imara na huru zenye kujiendesha zenyewe pasipo kuingiliwa na siasa za watawala...

Ni ngumu sana kwa DG mfano wa TANESCO au hata UDART kujisikia yuko huru na akafanya iwapo hana uhakika wa nafasi yake kwa sababu anakuwa hajui Rais au PM amelalaje Leo na ataamua nini juu ya hatima yake...

Asanteni..
 
Ukitaka kujua ugumu wa biashara ya ndege ilivyo, angalia tu mabadiliko ya makampuni hata huko nje, kama Marekani. Mashirika yaliyokuwepo miaka 20 iliyopita sasa hivi hayapo tena.
 
Sekta ya umma na sekta binafsi ni vitu viwili tofauti, sekta ya umma in mlolongo mrefu katika maamuzi, na unaweza ukatekeleza ukaonekana umefanya matumizi mabaya ya madaraka au fedha za umma.Ndio maana wasiotaka presha,wanapewa nafasi...watafanya kwa muda wao na baadaye wanawaachia wengine maisha yanaendelea
 
Biashara kuwa ngumu haimaanishi makampuni hayapati faida bali inamaanisha yale makampuni yenye ubunifu zaid yatafanya vizuri na mengine kufa au kununuliwa. Makampuni yanayofanya kufa, kuuzwa au kuungana kwa sababu za kibiashara ndio uzuri mmojwapo wa sekta binafsi.Ila likiwa la serikali litalindwa tu kwa ruzuku liwepowepo.

Ningeelewa kama ungeniambia mabadiliko hayo yamesababisha kudodora kwa sekta ya anga Marekani ila matokeo yake ni sekta hiyo imekuwa bora zaidi kiasi cha kuwa usafiri wa kawaida hata kwa raia wa kipato cha chini.
Ukitaka kujua ugumu wa biashara ya ndege ilivyo, angalia tu mabadiliko ya makampuni hata huko nje, kama Marekani. Mashirika yaliyokuwepo miaka 20 iliyopita sasa hivi hayapo tena.
 
Ndo kusema kuwa, ishu siyo nchi kukosa wataalamu wa nyanja zote i.e management, uchumi, fedha nk bali ni SIASA CHAFU na UONGOZI WA HOVYO WA TAIFA HILI..
Ninachokubaliana nawe moja kwa moja katika hoja yako ni hayo hapo juu niliyonakili.

Hii ina maana, hata mengine yasiyo ya biashara huko serikalini yapo hivyo hivyo. Je, na yenyewe tuyabinafsishe?
Hili ni swali halisi ninalouliza, wala sio katika kujibu hoja yako.

Sasa swali ni hili. Tufanyeje?

Tunaweza tukawapata viongozi wenye 'commitment' ya kuliendeleza taifa hili, pamoja na udhaifu wa ubinaadam walionao kila mmoja wao? Tufanyeje?
Hawa makampuni binafsi, tuwakodishe watuendeshee serikali pia?

Maswali ni mengi.
 
Hili la ndege hadi kinatoa ukakasi. Ndege si mali ya ATCL bali Shirika hilo limezikodi toka Mamlaka ya Ndege za Serikali. Hii ni kwa sababu moja muhimu. Kwa kufanya hivyo haziwezi kukamatwa na wale wanalolidai Hilo Shirika. Pesa za kulipia gharama za kukidhi zipo pale pale wakati biashara yenyewe imedoda. Ni wazi ATCL itafanya hasara tu na ndio maana sasa upo Makati wa kutafuta hayo madeni chechefu ili kupata ripoti yenye kuonesha kwamba hakuna hasara.
 
Ukikubali uliyoandika kwenye aya ya kwanza, itakuwa kwamba unakubali pia serikali mashirika yake nayo kufa na serikali hiyo hiyo kuanzisha mengine na uendeshaji mpyakwenye mashirika inapotaka kuhusika.

Mstari mmoja na nusu wa mwisho..., kushiriki kwa raia wengi katika usafiri huo maana yake ni kwamba hali ya uchumi wa wananchi hao inawawezesha wakati huu; lakini bado mashirika yanahangaika na ugumu wa biashara yenyewe.
 
Kama mashirika ya serikali nayo yanakufa sasa kwa nini ATCL na mengine mengi hayajafa mpaka leo na hasara zao zote za miaka yote yakaanzishwa mengine?

Mashirika ya serikali hayafi kibiashara kama ya binafsi, yanakufa pale ambapo wanasiasa wanajisikia yanapaswa kufa kwa sababu hayana maslahi tena kwao.

Marekani sio kwamba kipato cha wananchi kimeongeza tu ndio maana wanaweza kupanda ndege kama daladala ni kwa sababu masihirika ni mengi yanashindana kushusha bei,kuboresha huduma na kuzingatia muda.
 
Shirika la ndege na Umeme sio hata ya kimkakati. Ni mambo yanayofanywa na sekta binafsi vizuri kwa ufanisi mkubwa tu katika nchi nyingi.
Kwetu bado muhimu hayo mashirika kuitwa ya kimkakati. Sekta binafsi wana modus operandi ya namna ya kudeal na wafanyakazi wazembe: fanya uzembe leo, kesho unafukuzwa, kesho kutwa mtu mwingine anachukua nafasi. Sekta ya umma mtu hawezi kufukuzwa namna hiyo, kuna michakato mingi ili mtu afukuzwe rasmi, na hata Magufuli aliyekuwa akitumbua lakini wanaotumbuliwa wanaendelea kupata mishahara yao kama kawa.

Sasa nchi zote duniani huwa zina sekta ya umma, na inawezekana kabisa sekta ya umma ikawa efficient na effective. Lakini ili kufika hapo ni lazima mabadiliko ya msingi yafanyike nayo ni namna wafanyakazi wanavyokuwa incetivised au kuwa rewarded na utendaji wao. Kwa sasa katika nchi yetu tuna mfumo mbovu kabisa wa kureward wafanyakazi sekta ya umma, nao ni kuweka viwango vya mishahara bila kuzingatia viwango vya tija. Yaani embu chukulia sekta kama ualimu: shule binafsi zinareward waalimu wao kulingana na namna mwalimu anavyoiingizia shule faida, wakati shule za umma nyote mtalipwa TGS fulani kama tuna kiwango sawa cha elimu na miaka ya ufundishaji bila kujali mwalimu anaeleweka darasani au la. Hapo ndipo wafanyakazi wa umma hupoteza kujiongeza kwao, maana hata akijiongeza vipi hakuna wa kurecognize na kureward accordingly.
 
Nilitaka kuuliza, kumbe jibu unalo hapa.

Haijalishi, iwe sekta gani, ni utaratibu tu?

Watu hawaajiriwi sekta ya umma kwenda kufanya uzembe. Sijui serikali yoyote inayofanya hivyo.

Lakini, kama serikali yenyewe haina taratibu nzuri za kuwakomesha wazembe, basi, hilo ni tatizo la serikali yenyewe;na tatizo hilo ndilo tunalozungumzia hapa

Kama serikali inafanya kazi vizuri, hakuna sababu ya wafanyakazi wake wasifanye vizuri na kwa hiyo hata shughuli zinazofanyika huko kwenye mashirika yake zitakuwa ni nzuri
 
Mkuu, ATC ilishakufa mara kadhaa. Hii iliyopo hata sijui ni ya mara ngapi!

Huko Marekani? Acha aiseee, mwaka 1989 ukipanda ndege ungeonekana wewe ni mtu wa daraja fulani! Kipato kimeongezeka sana na kusambaa kwa watu wengi.
Siku hizi huko mtu kuwa na gari haistui mtu kama ilivyo hapa kwetu mtu akienda sasa hivi 2021 kununua baiskeli hapa kijijini kwetu Mchanaganue. Hapa mtaani kwetu baiskeli tu naweza kuzihesabu kijiji kizima hata 20 sipati!

Mashirika yanakuwa mengi kwa sababu walaji wapo, vinginevyo mashirika hayo usingeyaona. Lakini pamoja na hali hiyo, bado biashara ya ndege ni ya kuuma meno hasa kuifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…