Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Eeenh Heeee, mchango wako 'serious', lakini ulivyouwasilisha imenibidi nicheke, hasa huko mwisho kwa 'dokta kuwa injinia"!

Mkuu, kama unanielewa vizuri, mimi sikatai ushiriki wa sekta binafsi sehemu yoyote katika biashara. Sikatai kabisa.

Ila naomba unielewe: unavyoliweka hapa wazo lako, ni kama huko kwenye sekta binafsi biashara hazianguki, na kana kwamba watu walioko huko ni kama malaika wenyewe walioshuka toka mbinguni.
Hali haipo hivyo hata kidogo

Na kwa maoni kama uliyotoa hapa, sijui unashindwa kitu gani kuhitimisha kabisa kwamba hata serikali yenyewe inafaa tuiondoe, tuwape sekta binafsi waiendeshe!
Labda nikutahadharishe kidogo unaponogewa na fikra zinapotiririka ukiandika; kwa mfano unaandika: "Na nchi za ulaya zote walianza kuamini na kusapoti ekta binafsi kabla ya karne ya 10". Kweli? Histyoria hii unayo? Na una uhakika nchi zote hizo hakuna kinachofanywa na serikali katika baadhi ya mashirika katika nchi hizo, badala ya kuiachia sekta binafsi ifanye, nchi zote za Ulaya?
 
Wengi hawana elimu ya ujasiriamali
 
Serikali haitakiwi kufanya biashara, full stop. Serikali kazi yake ni kutunga sera na kuweka mazingira rafiki kwa watu ili wavutiwe kufanya biashara.
Huwezi kuwa na serikali inayoshindana na raia wake, lazima raia atashindwa tuu na mwisho wa siku serikali nayo itaboronga.
 
Mchango wako huu umenifikirisha kweli kweli!

Natamani niukalie kidogo na kuutafakari ili nitoe mawazo ya kina juu yake; lakini najua nikiondoka sasa bila kujibu kitu, ninaweza nisipate nafasi tena ya kurudi.
Ngoja nijaribu kuujibu kwa kuukata vipande vipande:

1. Vipawa vya Ubunifu wa wafanya biashara ambao wasomi hawana ubunifu huo - sijui ukweli wa hili jambo. Kwani maana ya kuwa msomi ni nini hasa? Si inahitaji kujua vizuri eneo unalosomea na mbinu mbalimbali zinazotumika katika eneo hilo? Sasa kama umesoma vizuri na kujua mbinu za eneo hilo, kwa nini usiweze kujua mbinu na ubunifu katika eneo hilo?
Kwangu mimi, naamini, sio ukosefu wa kuwa mbunifumbinu, bali ni mchango wa mambo mbalimbali yanayokwamisha mashirika, ikiwemo na hizo siasa na ufisadi na mambo chungu nzima yanayoyakabili mashirika ya umma. Kama vikwazo hivi vingeondolewa, ufanisi kwenye mashirika ungepatikana.

2. "Bodi za wakurugenzi kwa kampuni kubwa huwa ni watu wenye hisa kubwa kwenye kampuni husika"
Na kama ulivyosema, bodi za mashirika ni watu walioteuliwa na wanasiasa, ambao hutumia vigezo ambavyo hata havina manufaa yoyote kwa shirika.
Swali ninalojiuliza hapa, ikiwa ni pamoja na kukuuliza wewe, kwa nini iwe hivi; na kwa nini wenye shirika (wananchi) na waoo wakubali hali hiyo? Hawa wanasiasa tunawachagua sisi wananchi; lakini tunashindwa kuwawajibisha?
Kwa hiyo jibu lipo hapa. Kushindwa kwa mashirika yetu kunatokana na sisi wenyewe wananchi kutowawajibisha wahusika ili watambue kuwa kazi wanazofanya hazikidhi matakwa yetu.

3. "Sio biashara tu, vitu vyote vya serikali, hadi shule, hospitali huduma ni mbovu kwa kukosa UBUNIFU."(?)

Huu mstari wako wa mwisho ndio uliotoa mhitasari mzuri sana wa mengine yote yaliyoandikwa hapo juu.
Siamini kwamba sababu ya ubovu wa shule, hospitali, n.k., ni ukosefu wa UBUNIFU.
Ni kutotimiza wajibu ipasavyo kwa wahusika, ikiwa ni pamoja na waajiriwa wa sehemu hizo na wasimamizi wao wote tokea ngazi za juu serikalini.
Kama serikali inawanyima watumishi wake nyenzo za kufanikisha kazi zao, huko sio kukosa 'UBUNIFU'.
 
Mchango mzito huu.
Sitoweza kuutendea haki kujibu harakaharaka hapa.
Lakini niseme tena hapa. Mimi, Kalamu1, sisemi kwamba serikali ijihusishe na kila aina ya biashara yoyote iwayo; lakini nasema bila kumung'unya maneno, serikali inawajibu, na ni lazima, haiwezi kujitoa moja kwa moja katika baadhi ya maeneo, kama elimu, kama afya, kama mashirika muhimu yanayotoa huduma kwa wananchi, kama umeme, na hata maji.

Na hasa hasa kwa wakati huu wa maendeleo ya nchi yetu.

Ila, naisihi serikali yetu, ifanye kazi zake kwa ufanisi ili mashirika haya yatoe huduma stahiki kwa wananchi.
 
Ni Ujinga kila saa kutolea mfano wa china, Tanzania mtu anaiba na afanywi chochote kwa sababu tu ni kada wa chama na alikua mteule wa rais
Mkuu 'Science Priest', mimi nimekwishatoa mfano wa China kuwa na mashirika yaliyofanikiwa, lakini sikugusia hayo uliyoyaweka hapo ya kuwaondoa uhai wabadhirifu, sio kwamba sikujua. Hilo nililiacha maksudi, na kwa kweli sioni tatizo ikifanyika hivyo hata hapa, mradi haki inatendeka.

Magufuli angeelekeza ukali wake huko, na kutoonea wapinzani wake, hata mimi ningekuwa shabiki wake mkubwa.

Hatuwezi kuendelea kuwachekeachekea hawa washenzi wanaoturudisha nyuma, halafu hao hao wanarudi hata humu JF na kutucheka na kusema serikali haiwezi kufanya biashara!
Inaudhi sana!

Nakushukuru kwa kuwa muwazi, na ningependa sasa tuwaambie hawa watu ukweli bila kuficha kitu kwamba tunataka viongozi serikalini wenye uchungu na mali za nchi hii. Ukihujumu, kama wewe ni mfanya kazi, au mfanya biashara, kukwamisha maslahi ya wananchi, haki yako ni adhabu kali, ikiwa ni pamoja na kuondoa uhai wako.

Utakubaliana nami tuipigie kelele kampeni hii humu JF?
 

Kumbe huelewi kwamba hela ya serikali ni hela ya walipa kodi. London Underground ambayo asilimia 41% ya hela za kuindesha zinatoka kwa walipa kodi tuseme ni government program siyo biashara.
 
Watendaji na wezi kwenye hayo mashirika si ni sisi hawa hawa; inakuwaje tunailaumu serikali inayotuwezesha?
Sioni logic ya kuilaumu serikali wakati tunaoua hayo mashirika ni sisi wenyewe!
 
Miradi ya serikali wanaiendesha bila ya kuwa na uchungu wao hawajali kuhusu pesa
Anglia mradi akiuwendesha mtu binafsi lazima awe na uchungu,mfano tu mtu kama baresa etc ona wanavyoendesha biashara zao
Ila serikali wao wanajua hata mradi ukifa itatafutwa pesa nyingine tu

Ova
 

Nimeeleza nini cha kufanya ktk post yangu uliyoikwoti...

Taasisi na mashirika ya umma yaachwe yajiendeshe yenyewe kwa kuzingatia professionalism huku serikali ikisimama kama mlezi mkuu ili wakikosea tuwe na nguvu kuwauliza na kuwahoji...

Kwa sasa sina hakika kama serikali (viongozi hawa PM, Rais, wabunge nk ) wana audacity ya kukemea hasara na failures ktk uendeshaji wa mashirika na taasisi hizi za umma huku wenyewe wakiwa ni sehemu ya tatizo/failures hizo...

Tuwazuie wanasiasa kisheria kuingiza nepotism na siasa zao kwenye uendeshaji wa taasisi na mashirika haya. Tuziache management ziwe free kuendesha taasisi hizi...
 
Lakini serikali yenyewe pia inaweza ikayaendesha mashirika hayo kwa ufanisi ikitaka kufanya hivyo. Hakuna kizuizi chochote kinachoifanya sewrikali isiweze kuyaendesha vizuri bila ya kutegemea sekta binafsi.
 
Taasisi na mashirika ya umma yaachwe yajiendeshe yenyewe kwa kuzingatia professionalism huku serikali ikisimama kama mlezi mkuu ili wakikosea tuwe na nguvu kuwauliza na kuwahoji...
Hakuna chochote ninachokataa hapa.
Kwa sasa sina hakika kama serikali (viongozi hawa PM, Rais, wabunge nk ) wana audacity ya kukemea hasara na failures ktk uendeshaji wa mashirika na taasisi hizi za umma huku wenyewe wakiwa ni sehemu ya tatizo/failures hizo...
Nadhani kinachotakiwa hapa ni kuwapata viongozi hao wa ngazi za juu wasiokubali uozo popote ndani ya serikali na mashirika yake.

Kutokubali huko ni pamoja na kujitambulisha wazi kabisa kwamba kila atakayevuruga popote hatoachwa hivi hivi. Sheria itamkumba na hata ikibidi adhabu mbaya zaidi ziwekwe kuwadhibiti hawa wakorofi.
Tuwazuie wanasiasa kisheria kuingiza nepotism na siasa zao kwenye uendeshaji wa taasisi na mashirika haya. Tuziache management ziwe free kuendesha taasisi hizi...
Nipo nawe sawia kabisa.

Unajua, hata huko kwenye sekta binafsi wanaohimiza serikali kujiondoa kwenye sehemu kadhaa za kimkakati, ni hawa hawa wanaochochea uozo huko serikalini, halafu wanageuka na kuanza kuhimiza wapewe wao.

Akina Roastam na wengine wamehimiza hapa kugawiwa karibu bure kabisa mali za serikali, halafu wanageuka na kuzifanya mtaji wa kukopa pesa za kufanya shughuli zao nyingine; halafu wanageuka na kuicheka serikali na kuwacheka wananchi.
 
Una akili ya mbuni kuinua mikia ya nyuma angani na kufukia kichwa shimoni.

Umeshawahi kuisikia UDA , DMT na hata KAMATA?

Ziliendeshwa na serikali kwa miongo zaidi ya mitatu, na serikali ikanyoosha mikono.

Sasa leo nini kimebadilika?
Wameendesha mradi kimagumashi na tunaona matokeo yake.
Amka ndugu!
 
1. Ishu si "kuwapata wapi viongozi wa kuwakabidhi taasisi/mashirika haya" ili wayaendeshe. Viongozi ni hawahawa waliopo wanatosha na wana sifa zote..

2. Kinachokosekana kwa viongozi hawa ni Job security zao. Hatima yao iko controlled na wanasiasa. Hawana uhakika wa kesho yao. Wanachofanya ni kutafuta mwanya wa kuchukua chao mapema tena mara nyingi wakishirikiana na wanasiasa - watawala hao hao kuyafilisi na kuyala mashirika haya. Katika mazingira haya, huwezi kuwa na management bunifu kuendeleza taasisi/shirika...

3. Unawalaumu bure kina Rostam na wengine waliopewa viwanda na kushindwa kuviendeleza...

Sababu ni zilezile, SIASA CHAFU ambazo zinazalisha viongozi waovu na mafisadi..

Hawa daima ni walaji na hawana uchungu wala hawaangalii maslahi ya nchi bali matumbo yao na familia zao...

Kupewa viwanda hivyo na kisha kushindwa kuendelezwa, ni deal kati ya wafanya biashara hao na baadhi ya wanasiasa - watawala kujipatia fedha kwenye mabenki kwa dhamana ya serikali kisha kutumika kufanyia mambo mengine...

Na ikitokea hivi hakuna hatua zinazochukuliwa kwa wafanyabiashara hawa kwa kuwa viongozi wenyewe are part of the deal...
 
'Masopya...' vuta pumzi, kwa sababu hapa ni serious discussion, na tambua unanijibu mimi, huwa sitaki upuuzi..., mbona hukumbuki?
Hayo mashirika nayajua sana na nimeyapanda sana, na huwezi kuniambia chochote juu yake.

Soma vizuri unielewe: kama ni nyinyi, sijui kama nawe uko kwenye biashara hizo za kutafuta kila mara kuangusha juhudi za serikali, bado hamjampata kiongozi anayeweza kuwakomesha.

Magufuli kama angeacha upuuzi wa kuonea watu wasiostahiri kuonewa, na akashughulika na wahujumu waliopo humo humo serikalini na huko kwenu kwenye sekta binafsi, angeacha heshima kubwa sana katika jamii ya kumkumbuka kwayo.

Sasa hapa nimemzungumzia Magufuli moja kwa moja kukuchokoza kama wewe ni mtu mwenye kumbukumbu, kwa sababu tulishawashiana moto juu yake wewe na mimi na pacha wako 'Jidu' humu humu JF.

Kwa hiyo wewe kuniita mimi kuwa na "...akili za mbuni" inakufanya wewe uwe kama kichaa fulani.

Katika nchi zetu hizi, na hasa kwa Tanzania, baada ya kuona Magufuli aliyofanya, dawa ya kuyafanya hayo mashirika kufanya kazi ipaswavyo ni kuacha kucheka cheka na wapuuzi wanayoyaendesha.
Ikilazimu, baadhi yao ni kufungwa jela maisha na hao wanaohujumu hata kifo ni haki yao.

Ndiyo, nyinyi watu mnatia hasira sana na hivi vimambo vyenu.

Mnashiriki kuyaua mashirika ya wananchi, halafu mnarudi hapo pembeni na kuchekelea..., kuna usaliti zaidi ya huo?

Huu ndio usaliti unaotakiwa kunyongwa na kufilia mbali, kwa maslahi mazima ya taifa, sio kwenda kuhangaika na akina Lissu!

Nimejaribu kila njia ya kujieleza nieleweke, naona sieleweki na wengi hapa. Maslahi ya waTanzania ni kila kitu, hayawezi kuchezewa na mtu yeyote, iwe serikalini au huko kwenye sekta binafsi.

Naomba sana utulie unisome vyema, usinirukie tu kujibu bila kuelewa ninakotokea.

Mnachosha sana.
 
3. Unawalaumu bure kina Rostam na wengine waliopewa viwanda na kushindwa kuviendeleza...

Sababu ni zilezile, SIASA CHAFU ambazo zinazalisha viongozi waovu na mafisadi..
Huwezi kuwaondoa hao wafanya biashara katika muungano wao na siasa chafu. Kwani historia zao hapa Tanzania hazipo wazi? Walijazana bungeni kufanya nini?

Wanaowachochea hao wenye siasa chafu ni akina nani kama siyo hawa hawa!

Wote wapo kwenye chungu kimoja.
 
Sasa mkuu, 'The Palm Tree', mbona uliwaondoa kwenye lawama kwenye mchango wako huko juu?

Huwezi kurekebisha chochote kwenye siasa bila kuwagusa hawa wafanya biashara wahujumu wakubwa wa nchi zetu hizi.
 
Again!!

Acha porojo nitajie shirika moja tu la serikali linaloendeshwa kwa faida

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Sasa nikisema hakuna, utachukua huo kama ushahidi kuonyesha kwamba serikali haiwezi kuendesha mashirika yake kwa ufanisi?

Mimi sikubaliani na hiyo dhana ya kwamba serikali haiwezi kuendesha mashirika yake, SIKUBALI.

Sitaki kurudiarudia mambo niliyokwishaandika hapa.

Ubovu wa watendaji, wanaoua mashirika, sio sababu ya kuhitimisha kwamba serikali haiwezi kufanya kazi hizo.

Inaweza sana, kwa kuwashughulikia wahujumu wake wote, waliopo kwenye mashirika hayo, na walio nje, hasa kwenye hizo sekta binafsi.

Bado tu hajapatikana mtu sahihi wa kuwanyoosha wote.

Ukitaka kunielewa, utaelewa ninachoandika hapa, ukitaka kuona kuwa ni porojo, sawa, jifurahishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…