Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Bado huelewi the spirit of free enterprise na innovativeness of private business.
Serikali kufanya biashara ni sawasawa na paka kukata mawimbi kuogelea pale Feri!

Ni ukweli usiopingika kuwa huwezi kukuta ati “mzalendo” akabidhiwe mabilioni ya wananchi halafu ayachekee bila kuchota kiasi.

Mwisho sisi wenyewe kwa ujinga wetu tunamkabidhi mabilioni halafu tunamwita mhujumu.
Huyo mtu hana uchungu wowote na mtaji au mali ya umma iliyopo pale , wala hajawekeza chochote pale zaidi ya ajira!

Halafu tunategemea afanye wonders!
Hapo ni kutegemea yule paka aogelee toka Feri hadi Kigamboni.

Tatizo mko wengi msiojua principles hizo, na wasiojua kwa kiwango cha lami wanafikiri msomi zaidi hasa mwenye PhD ndio watakuwa enterprising zaidi.

Experience is proving them wrong!
Mwalimu alitengeneza mashirika zaidi ya 400, yalikufa YOOOTE!
Na hilo somo wenye vichwa vigumu hawalielewi.............!
 
Experience is proving them wrong!
Mwalimu alitengeneza mashirika zaidi ya 400, yalikufa YOOOTE!
Na hilo somo wenye vichwa vigumu hawalielewi.............!
Hii mnapenda sana kuiimba kama kasuku, lakini hamuelewi chochote mnachoimba.

Inaelekea unasoma, lakini ubongo wako umeganda palepale ulipogandia toka mwanzo.

Kuna biashara inayoweza kuzifanya serikali kwa mafanikio makubwa kwa manufaa ya wananchi. Kama wewe hutaki kukubali hilo, hiyo ni shida yako, baki nayo hivyo hivyo.
 
Srikali inafanya biashara kama zipi kwako wewe ubongo uliozibuka!
Zitaje!
 
Hujui biashara zinazofanywa na serikali?

Sasa hapa unalalamikia nini juu ya serikali kujiingiza kwenye biashara!
Usikwepe kwepe swali.
Zaidi ya kodi tupe shirika linaloendeshwa kibiashara na kwa faida ya "kizalendo" kama ulivyohamasika!
 
UshU Ushauri NI kuwa serikali idili na vitu vichache tu. Huwezi kung'ang'ania vitu ambavyo sekta binafsi Inaweza kuvifanya vizuri.
 
UshU
Ushauri NI kuwa serikali idili na vitu vichache tu. Huwezi kung'ang'ania vitu ambavyo sekta binafsi Inaweza kuvifanya vizuri.
Hata sasa hivyo inavyovifanya bila ufanisi ni vichache; lakini haina maana kwamba haiwezi kuvifanya kwa ufanisi. Inaweza sana.
 
Hata sasa hivyo inavyovifanya bila ufanisi ni vichache; lakini haina maana kwamba haiwezi kuvifanya kwa ufanisi. Inaweza sana.
Kama inaweza sana kufanya kwa ufanisi, then tatizo ni nini?
 
Mfumo wa uendeshaji mashirika ya umma Una mapungufu,watendaji wangeajiliwa kwa kutuma maombi na pawepo na vipengele vya uwajibikaji kwa watumishi pia,CEO awe na mkataba na si mtumishi wa umma na apewe malengo ya shirika akishindwa anaondolewa kama makocha wa mpira .
 
Kama inaweza sana kufanya kwa ufanisi, then tatizo ni nini?
Tatizo ni serikali, kwani serikali haiwezi kufanya kazi zake kwa ufanisi? Inazuiwa na nani kufanya hivyo.

Hivi serikali zinakuwepo ili zifanye mambo bila ufanisi; hiyo ndiyo kawaida?
 
Biashara ipi na kwa mfano upi dhahili?
 
Mnapenda kukifananisha na China lakini hamtaki hata kidogi kuishi kama wachina. Lakini hata serikali ya China haifanyi biashara japo inatoa huduma ya usafiri mijini kama hiyo ya mwendo kasi.
Tatizo letu ni moja, UBINAFSI.
Magu nae aliteswa na ubinafsi ,, kile kituko cha kuipaisha chato kwa nguvu huku akitumia kodi zetu kilimtoa kabisa sifa za kuweza kusimamia mali zetu vizuri.
Hivyo njia inayobaki ni serikali kutojiingiza kwenye biashara au la iamue kutoa huduma.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Biashara ipi na kwa mfano upi dhahili?
Hutaki kuelewa ninachoeleza, siwezi kukulazimisha uelewe na ukubali.
Wewe hujui mifano ya mashirika inayoyaendesha? Unataka nikupe mifano?
Mashirika yote yanayoendeshwa na selikali kwa 100% uendeshwa kwa hasara, hutegemea ruzuku tu kujiendesha na hayana UBUNIFU na mshindani. Mfano NI Tanesco, Posta, TLA,
Using'ang'anize hoja zisizo na uhalisia
 
Siyo lazima tuishi kama wachina, lakini tunaweza kutumia baadhi ya njia zao zinazofanikisha katika mazingira yetu. Kwa nini tuishi kama wao; kwani sisi hatuna akili za kufikiri na kupanga mambo tunayoona yanafaa?

Una maana unamwona mchina bora kuliko ulivyo wewe, hadi upende kuishi maisha yake?

Serikali zote dunia hutoa huduma, sio China pekee...

Hata hivyo, unaangalia tu huduma za mwendo kasi hapo, kwani huduma zinapotolewa hazipashwi kufanywa ili ziwe huduma bora?

Sikubaliani na wewe juu ya serikali ya china kutofanya biashara. Mashirika yote yaliyotapakaa duniani kote yanayojenga kila aina ya miundo mbinu yanatoa huduma?
TTCL hapa kwetu haiwezi kufanya biashara, kwa nini?
 
Mashirika yote yanayoendeshwa na selikali kwa 100% uendeshwa kwa hasara, hutegemea ruzuku tu kujiendesha na hayana UBUNIFU na mshindani. Mfano NI Tanesco, Posta, TLA,
Using'ang'anize hoja zisizo na uhalisia
Kwa nini kwa mfano, Tanesco iwe biashara ya hasara, hebu nieleze wewe? Na kwa nini hiyo biashara inatakiwa ifanywe na shirika binafsi ndipo liwe na faida, kwa nini?
Hapa ndipo ninapotaka ufafanue kwa nini iwe hivyo.

Usiseme tu kwa kuwa ni serikali haiwezi kufanya biashara, hiyo siyo sababu.

Ndio, kuna aina za biashara/huduma zinazohitaji kupewa ruzuku, lakini si zote.
 
Serikali uajili kwa vyeti. Sio uwezo nA UBUNIFU. Haina uwezo wa kuongeza tija. Unaweza ukaws mbunifu ukaongeza mapato ya kampuni lkn mshahara unabak vile vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…