Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Ni ukweli ulio bayana kuwa Serikali imeshindwa kufanya biashara na nibusara waukubali ukweli huu ili either waiachie private sector ifanye biashara wao wabaki kukusanya kodi au washirikiane na private sector through PPP.
Historia siku zote ni mwalimu. Tulikuwa na mashirika ya umma lukuki kama - NASACO, TRC, UFI, URAFIKI, TANGANYIKA PECKASE, ALAF, UDA , ATC ,TRC etc yote hayo tuliyazika kaburini kutokana na mapungufu ya namna ambavyo Serikali haiwezi kuendesha biashara.
Na kushindwa kwa mashirika yote hayo ni kwa sababu moja tu kwamba serikali haiwezi kufanya kazi hiyo?
 
Robert kisena achiwe aendeshe kampuni yake aliwekwa ndani kwa hila tu za marehemu, yani marehemu alikuwa na roho mbaya sana.
Mjanja mjanja hana uzoefu na sekta ya usafirishaji zaidi ya kukwapua Uda na wapigaji wengine.

Mradi ulikuwa mzuri, shida kupeana tenda kishkaji
 
Serikali haiwezi kufanya biashara. Hasa hizi za kwetu.

Kama Waziri Mkuu anaona madudu kwenye mradi wa mwendokasi.

Kama Serikali imeshindwa kufanya miradi ya reli ya Kati na TAZARA, vivuko, ndege na sasa Mabasi ya mwendokasi kujiendesha ni wakati wa kubadili mtazamo.

Wajiondoe waruhusu sekta binafsi iviendeshe yenyewe ichukue Kodi na idili na kutoa huduma kwa wananchi.
Mwendokasi ni tusi kubwa kwa serikali, kwani serikali yenyewe ilitengeneza mazingira ya mradi usifanikiwe kwa makusudi.
Hata pale Waziri Mkuu alipotoa ndimi za moto majuzi,tunauliza miaka yote mitano hakuyaona hayo hadi mradi umekufa!
Serikali kwa hilo ilikosea.
 
Masuala ambayo yanagusa wananchi moja kwa moja na usalama wa taifa na ni vigumu kufanywa kwa ufanisi na sekta binafsi peke yake ni Elimu, Maji, Afya, Miondombinu ( barabara, umwagiliaji, airports,bandari, reli) na Ulinzi.

Kwingine kote serikali haipaswi kujiingiza na huwa inajiingiza kwa ushabiki, fahari, kiherehere na kushindwa kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi kufanya kazi.
Mkuu Yoda, hakuna serikali yoyote wakati huu 2021, hata ile ya kijana Kim Jong Un, wala Cuba, wanaofikiria kurudi kwenye enzi za miaka hiyo, sembuse sisi?

Lakini wakati huo huo, hata hawa Wamarekani, Waingereza, au Wajerumani, hakuna serikali inayokataa kata kata kuwa na mchango wowote katika uendeshaji na usimamizi wa baadhi ya maswala yanayogusa maisha ya wananchi wao moja kwa moja.
 
Ungeenda kuleta hao wawekezaji wa kuja kujenga reli kwa hela zao halafu ndio utoe hayo mapendekezo, better still nchi bado inahitaji rail roads za kuunganisha mikoa kadhaa tafuta hao wawekezaji wa kujenga hizo reli kama biashara (siyo mambo ya kujenga huku wakiitaji government guarantees za kutokulipa kodi) halafu tuone kama watazuiwa.

Yaani watu wanapenda vya kuchinja tu, kunyonga na-ah. Wakishaona vipo ndio utasikia serikali aiwezi. Mapungufu yapo kwa sababu unqualified people are given managerial post which are beyond their abilities.

Lakini mnataka serikali ijenge kwanza barabara kwa mabilioni, inunue mabasi na kujenga vituo halafu itoe zawadi ya private kuendesha. Au we ukuona kama kuna shida ya vivuko miaka yote, mbona ukuleta wawekezaji.

Hizi akili sijui huwa mnazitoa wapi.
 
Mada muhimu kweli kweli, lakini wachangiaji wanachungulia tu na kupita zao! Wanatafuta mada za CCM na CHADEMA!

Mimi sikubaliani na wewe juu ya hiyo dhana ya serikali haifanyi biashara.

Usiifanye kuwa 'dogma', au kama kitu ulichokaririshwa.

Hata kama ulisikia ikisemwa hivyo, kwa nini usiweke muda ujaribu kutazama uhalisia na ukweli wake ukoje?

Sasa mimi nakushauri uanze kulitazama hilo kwa jicho la pili; acha kufumba jicho moja, yafungue yote mawili ili upate picha nzuri.

Ni hivi: kuna kizuizi gani kinachofanya serikali isiweze kufanikisha kuendesha miradi hiyo yote uliyoitaja?

Kwani haina watu wenye uwezo wa kuifanya. Kama wapo, ni nini kinazuia wasifanye hiyo kazi kwa ufanisi?

Na kama hawapo, serikali haiwezi ikamwajiri, ndiyo kuajiri kampuni kwa mkataba inayoweza kuendesha shughuli hizo kwa ufanisi? Sijasema serikali ibinafsishe, kama wewe unavyotaka.

Lakini la muhimu hapa ninalolisisitiza, ni hii dhana potofu ya kwamba serikali haiwezi kufanya mambo yake kwa ufanisi.

Kuna sababu zipi...., hizo sababu haziwezi kuondolewa?

Kila mara imekuwa ni kutafuta visingizio tuuu kwa kushindwa tu kutimiza wajibu mliopewa kuutimiza.

Hapa ndipo nilipopenda Magufuli apafanyie udikteta wake haswa haswa...! Hali ingebadilika tu baada ya muda.

Haya mashirika makubwa ya ujenzi na mengine toka China tunayoona yametapakaa duniani kote, mbona haya yalikuwa ni mashirika chini ya serikali?
Wao waliweza vipi?
Kitu kinachopelekea massive failure kwenye mashirika ya serikali ni kutokana na aina ya recruitment ya management inavyofanyika.

Mara nyingi hawatafutwi watu wenye uwezo wa kuendesha shirika: Mtu anapewa kama kulipa fadhila aidha kwasababu alimsaidia mtawala wakati wa kampeni, au ili atulie.

Maana yake kazi inafanyika nje ya shirika, ukishapewa fadhila kifuatacho ni ulaji.

Mfano Mtu kama Musiba ameshatumika sana, sasa siku akipewa nafasi usitegemee ufanisi wowote, kwasababu siyo sehemu ya makubaliano. Kama ni kazi alifanya atakapowekwa ni kutafuna tu kwa wakati wake.

Wangekuwa na nia ni aidha wangeuza hisa wabaki kupokea gawio na kodi au wangeajiri waendeshaji hata kwa mkataba wa miaka 3 mitatu huku wakipima ufanisi.
 
Utasema mengi lakini ukweli ndio huo ..

Serikali haiwezi kufanya biashara! Tokea tupate uhuru mpaka leo hakuna sehemu ilipofanikiwa ni madudu tu kila siku.

Ni bora wajiweke pembeni wajikite kwenye kukusanya kodi tu

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Hata kazi yake ya msingi kukusanya kodi imechemka
 
Ubunifu huwa unachochewa na faida ambayo inaenda kwa mmiliki na wafanyakazi wake moja kwa moja. Shirika la serikali likipata faida au hasara mshahara wa mkuregenzi na wafanyakazi ni ule ule unaopangawa na utumishi au kuongezwa kwa pamoja na watumishi wengine wote mei mosi. Kwa mantiki hiyo kwa nini Mkuregenzi wa shirika la serikali afanye juhudi yoyote kuongeza ubunifu??
Hapana.

Bado unaona muundo mbaya wa uongozi na kufanya ni aina hiyo hiyo tu inayowezekana huko serikalini, jambo ambalo siyo kweli.
Tunapozungumzia biashara binafsi, bila shaka unajua kwamba ni makampuni makubwa yanayofanya biashara hizi na sio lazima kuwa ni mtu mmoja pekee , kama Mo hivi au Bakresa au Marehemu Mengi.
Makampuni haya miundo yao haina tofauti kubwa na muundo wa serikali. Hata huko wapo viongozi wabaya, na kuna bodi mbovu vilevile. Na kuna wanahisa, wanaowawajibisha, kama inavyotakiwa wananchi nao wawawajibishe watendaji wabovu badala ya watendaji ndio wawashambulie wananchi.
 
Masuala ambayo yanagusa wananchi moja kwa moja na usalama wa taifa na ni vigumu kufanywa kwa ufanisi na sekta binafsi peke yake ni Elimu, Maji, Afya, Miondombinu ( barabara, umwagiliaji, airports,bandari, reli) na Ulinzi.

Kwingine kote serikali haipaswi kujiingiza na huwa inajiingiza kwa ushabiki, fahari, kiherehere na kushindwa kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi kufanya kazi.
Kwa leo katika mjadala huu, sitaingia huko kwenye kunyambua ni kipi serikali ifanye na kipi isifanye. Kuna mambo ambayo itakuwa ni aibu kabisa kwa serikali kuyafanya.
 
Amezengumza jambo la ukweli kwa asilimia 90. Kwa kiasai kikubwa China imeendelea si kwa sababu ya ubunifu mkubwa wa watu wake bali ni kukopi teknolojia za Magharibi na kuzitumia vizuri. Ni "inventions" chache sana za teknolojia zilizofanyika China, sehemu kubwa ya meandeleo yake ni kutokana na "innovations"
Aiiseee, wewe unaishi dunia yako kama unaona hivyo ulivyoandika.
Sina lolote la kujibu hapo.
 
Mkuu Yoda, hakuna serikali yoyote wakati huu 2021, hata ile ya kijana Kim Jong Un, wala Cuba, wanaofikiria kurudi kwenye enzi za miaka hiyo, sembuse sisi?

Lakini wakati huo huo, hata hawa Wamarekani, Waingereza, au Wajerumani, hakuna serikali inayokataa kata kata kuwa na mchango wowote katika uendeshaji na usimamizi wa baadhi ya maswala yanayogusa maisha ya wananchi wao moja kwa moja.
Mkuu kwa hayo mataifa uliyotaja ni vitu vichache sana ambavyo Serikali inafanya,ebu jaribu kufikiri Nchi kama U.S.A kuna Makampuni yana miliki vikosi vya kijeshi achana na private companies zinazo tengeneza vifaa vya kijeshi,unadhani kwenye Nchi kama hiyo Serikali wanaweza fanya Biashara ya usafiri wa mabasi??
 
Muone huyu na akili zake za kijima na kijwe.
Sasa kwa nini serikali haina mabasi yake ya biashara kwenda mikoani??
Ungeenda kuleta hao wawekezaji wa kuja kujenga reli kwa hela zao halafu ndio utoe hayo mapendekezo, better still nchi bado inahitaji rail roads za kuunganisha mikoa kadhaa tafuta hao wawekezaji kujenga hizo reli na kuendesha halafu tuone kama watazuiwa.

Yaani watu wanapenda vya kuchinja tu, kunyonga na-ah. Wakishaona vipo ndio utasikia serikali aiwezi.

Serikali ijenge barabara kwa mabilioni, inunue, mabasi na kujenga vituo halafu itoe zawadi. Au we ukuona kama kuna shida ya vivuko miaka yote, mbona ukuleta wawekezaji.

Hizi akili sijui huwa mnazitoa wapi.
 
Mkuu, ahsante kwa mchango wako, lakini dhana hii ni potofu kabisa.

Kwa nini watu wote hao walioko serikalini wote wawe hawana ubunifu, ila hawa wengine ndiko kuwe na wabunifu?

Umetoa mfano huo wa TTCL, ukalinganisha na TIGO, VODA na HALOTEL - hivi kweli unaweza kusema kwamba wafanyakazi walioko TTCL hawana ubunifu kama hao walioko kwenye mashirika hayo? Ushahidi wa hili ni upi?

Serikali wangetaka mashirika yao yafanye vizuri ingewezekana sana!

Basi tu, hatujapata viongozi ambao wana nia ya kuyafanya haya mashirika yawe imara. Ni mambo ya uzembe tu na kukosa usimamizi unaotakiwa kuyawezesha mashirika yafanye kazi vizuri.
Bonge la ufikiri. Mi nichangie tu japo sina majibu yote. Nadhani kuna sababu mbili kwanini mambo yanayoendeshwa na serikali hayaleti tija. Sababu ya kwanza ni kwamba wale wafanyakazi wa hayo mashirika hawaoni sense of ownership kwenye kile wanachokisimamia -- si mali yao binafsi hivyo hawawezi kwenda extra mile katika kuleta ufanisi. Na hasa kama mishahara ya hao wafanyakazi haitegemei uzalishaji wa hiyo biashara mtu anaweza kufanya hovyo, shirika likapata hasara lakini bado uhakika wa mshahara ukawepo maana serikali ina "vyanzo vingine" vya mishahara yao.

Sababu ya pili inaweza kuwa sabotage kutoka sekta binafsi, ili mambo ya serikali yakifa yajustify sekta binafsi ipewe nafasi.

Mapendekezo yangu ni kwamba ukiachilia mashirika ya kimkakati kama ya Ndege, Umeme, n.k ambako maslahi ya nchi ni ya msingi, vishirika vidogo vidogo kama UDART waachiwe sekta binafsi waoperate. Serikali ikishaweka miundo mbinu ya msingi kazi yake iwe kupokea kodi tu.
 
Robert kisena achiwe aendeshe kampuni yake aliwekwa ndani kwa hila tu za marehemu, yani marehemu alikuwa na roho mbaya sana.
ukweli kabisa Kisena anadhulumiwa mali zake kienyeji sana, wamemweka ndani yeye na mke wake, hivi hamna namna ya kuendesha kesi huku mtu akiendelea na biashara zake? ifike sehemu tutambue mchango wa mtu mmoja mmoja katika kujenga uchumi.
 
Amezengumza jambo la ukweli kwa asilimia 90. Kwa kiasai kikubwa China imeendelea si kwa sababu ya ubunifu mkubwa wa watu wake bali ni kukopi teknolojia za Magharibi na kuzitumia vizuri. Ni "inventions" chache sana za teknolojia zilizofanyika China, sehemu kubwa ya meandeleo yake ni kutokana na "innovations"
Ni nani/taifa gani halijakopi/kuiba mkuu Yoda!
 
Mo Dewji au Bakhresa group, Precision sio kama shirika la serikali na nilikupa sababu kubwa mbili mwanzoni tofauti ya biashara ya serikali na binafsi.

ATCL inaweza kuanzisha route kwa sababu mwanasiasa fulani anapenda, hicho kitu hakiwezi kufanyika Precision airways. ATCL inaendelea kupewa pesa na hazina wakati huu ambapo bado inatengeneza hasara na hata haijulikani lini inategemewa kupata faida.Precision wakipata faida zaidi ya miaka miwili mfululizo na wasiweze kufanya predictions lini watapata faida hawatapa mahali pa kukopa tena na watajiunga au kuuza kampuni kwa mwingine mwenye ubavu.

Mo na Bakhersa anawapa mkataba wafanyakazi wake. Kufanikiwa kwa kampuni yao ndio kunawahakikishia hao wafanyakazi kuendelea kuwepo zaidi sana wanaweza kmfukuza mfanyakazi muda wowote hata kama mkataba wake haujaisha.Serikalini sio rahisi hivyo.

Halafu Shirika la Serikali sio la Mtu mmoja au wanahisa ni la wananchi, ni la kila mtu.Hiyo tu ni tofauti moja kubwa sana.
Hapana.

Bado unaona muundo mbaya wa uongozi na kufanya ni aina hiyo hiyo tu inayowezekana huko serikalini, jambo ambalo siyo kweli.
Tunapozungumzia biashara binafsi, bila shaka unajua kwamba ni makampuni makubwa yanayofanya biashara hizi na sio lazima kuwa ni mtu mmoja pekee , kama Mo hivi au Bakresa au Marehemu Mengi.
Makampuni haya miundo yao haina tofauti kubwa na muundo wa serikali. Hata huko wapo viongozi wabaya, na kuna bodi mbovu vilevile. Na kuna wanahisa, wanaowawajibisha, kama inavyotakiwa wananchi nao wawawajibishe watendaji wabovu badala ya watendaji ndio wawashambulie wananchi.
 
Shirika la ndege na Umeme sio hata ya kimkakati. Ni mambo yanayofanywa na sekta binafsi vizuri kwa ufanisi mkubwa tu katika nchi nyingi.
Bonge la ufikiri. Mi nichangie tu japo sina majibu yote. Nadhani kuna sababu mbili kwanini mambo yanayoendeshwa na serikali hayaleti tija. Sababu ya kwanza ni kwamba wale wafanyakazi wa hayo mashirika hawaoni sense of ownership kwenye kile wanachokisimamia -- si mali yao binafsi hivyo hawawezi kwenda extra mile katika kuleta ufanisi. Na hasa kama mishahara ya hao wafanyakazi haitegemei uzalishaji wa hiyo biashara mtu anaweza kufanya hovyo, shirika likapata hasara lakini bado uhakika wa mshahara ukawepo maana serikali ina "vyanzo vingine" vya mishahara yao.

Sababu ya pili inaweza kuwa sabotage kutoka sekta binafsi, ili mambo ya serikali yakifa yajustify sekta binafsi ipewe nafasi.

Mapendekezo yangu ni kwamba ukiachilia mashirika ya kimkakati kama ya Ndege, Umeme, n.k ambako maslahi ya nchi ni ya msingi, vishirika vidogo vidogo kama UDART waachiwe sekta binafsi waoperate. Serikali ikishaweka miundo mbinu ya msingi kazi yake iwe kupokea kodi tu.
 
Marekani kuna hadi magereza za binafsi![emoji3]
Mkuu kwa hayo mataifa uliyotaja ni vitu vichache sana ambavyo Serikali inafanya,ebu jaribu kufikiri Nchi kama U.S.A kuna Makampuni yana miliki vikosi vya kijeshi achana na private companies zinazo tengeneza vifaa vya kijeshi,unadhani kwenye Nchi kama hiyo Serikali wanaweza fanya Biashara ya usafiri wa mabasi??
 
Mkuu kwa hayo mataifa uliyotaja ni vitu vichache sana ambavyo Serikali inafanya,ebu jaribu kufikiri Nchi kama U.S.A kuna Makampuni yana miliki vikosi vya kijeshi achana na private companies zinazo tengeneza vifaa vya kijeshi,unadhani kwenye Nchi kama hiyo Serikali wanaweza fanya Biashara ya usafiri wa mabasi??
Mkuu Econometrician, tusipoteze muda bure juu ya haya majadiliano.

Hakuna popote nilipokataa kwamba mashirika au watu binafsi waweze kuendesha shughuli, kama hizo za UDA kama watazifanya kwa ufanisi. Umeona popote nilipokataa hilo?

Nisichokubaliana nacho ni hii dhana potofu, inayotokana na mifano mibovu ya viongozi serikalini, kudhani kwamba serikali haiwezi ikasimamia huduma/biashara kwa ufanisi.

Tafadhali, jaribu sana kujielimisha na haya mambo unayosikia au kudhani yanafanyika kwenye hizo nchi unazodai makampuni binafsi kuwa na jeshi.
Haya makampuni ya marekani yanayowaajiri majirani zetu hapa kaskazini kwenda Iraq na Afghastan, usidhani yana uwezo wa kufanya hivyo huko huko nchini kwao.
Haya mambo siyo ya kusoma na kunakiri kirahisirahisi hivyo.
 
Shirika la ndege na Umeme sio hata ya kimkakati. Ni mambo yanayofanywa na sekta binafsi vizuri kwa ufanisi mkubwa tu katika nchi nyingi.
Kwetu bado muhimu hayo mashirika kuitwa ya kimkakati.
 
Back
Top Bottom