Hii hoja ya udini inanichanganya kichwa!! hivi hao walioteuliwa watawatumikia wananchi wa dini fulani tu au?? hivi ktk akili ya kawaida tu kuteuliwa kwa mkristo kuwa mkuu wa mkoa kutayafanya maisha yangu yaboreke kwakuwa mimi ni mkristo na ya muislamu yaharibike kweli? au ni yeye mhusika,familia yake na watu wake?
Mimi naunga mkono hoja ya mtu kuchaguliwa/kuteuliwa kwa uwezo wake wa kuongoza wengine na si kwa kigezo cha sura yake, jinsia yake, kabila lake, rangi yake au dini yake. Kwa mtindo huu nchi haiwezi kusonga mbele.
Raisi anateua kwa mujibu wa katiba ambayo inamfanya awe Imperial President na amepewa mamlaka ya kuteua kwa utashi wake.Huwezi kumpangia wala kumlazimisha afanye vile unavyotaka wewe.
Wakati wa bunge la katiba wawakilishi kutoka baadhi ya taasisi za kidini ikiwemo ya kiislamu hamkushiriki kuipindua rasimu ya pili ya Warioba iliyokua mwarobaini wa haya matatizo yote? Mlichukua hatua gani wawakilishi wenu walipoipitisha ile rasimu mpya iliyopata baraka ya watu wa mlengo mmoja wa kisiasa huku wengine waliojiita ukawa wakitoka?
Rasimu ya Warioba ilifuta vyeo vya Ma-RC na Ma-DC, ilipunguza mamlaka ya raisi ktk uteuzi nk. lakini vyote baadae vilirudishwa kama ilivyo kwenye hii katiba ya sasa ya mwaka 1977!! Mvumilie tu maumivu kwa kweli hakuna namna ya kuwasaidia.