Kama Serikali ya Tanzania haina dini, Mungu anayetajwa katika wimbo wa taifa ni yupi?

Kama Serikali ya Tanzania haina dini, Mungu anayetajwa katika wimbo wa taifa ni yupi?

Magufuli tenda haki, usiwe kama firauni aliyewainua watu wake na kuwadhalilisha waisrael, Muogope Mungu ukijua kuna siku ya haki, siku ya hukumu! Waislam sio wajinga kulalamika! Muogope Mungu, wewe ni mwanadamu tu usijione una akili sana kwa kuwa tumekupa urais
 
Magufuri si mdini kabisa. uteuzi wa wakuu wa mikoa 19 wakristu na 7 waislamu. wakati serikali iliyopita wakristu walikuwa 5 tu wakati wa uteuzi wa awali wa jk

hahaha kwa hiyo udini wakiwa waislam wengi tu
 
Hii hoja ya udini inanichanganya kichwa!! hivi hao walioteuliwa watawatumikia wananchi wa dini fulani tu au?? hivi ktk akili ya kawaida tu kuteuliwa kwa mkristo kuwa mkuu wa mkoa kutayafanya maisha yangu yaboreke kwakuwa mimi ni mkristo na ya muislamu yaharibike kweli? au ni yeye mhusika,familia yake na watu wake?

Mimi naunga mkono hoja ya mtu kuchaguliwa/kuteuliwa kwa uwezo wake wa kuongoza wengine na si kwa kigezo cha sura yake, jinsia yake, kabila lake, rangi yake au dini yake. Kwa mtindo huu nchi haiwezi kusonga mbele.

Raisi anateua kwa mujibu wa katiba ambayo inamfanya awe Imperial President na amepewa mamlaka ya kuteua kwa utashi wake.Huwezi kumpangia wala kumlazimisha afanye vile unavyotaka wewe.

Wakati wa bunge la katiba wawakilishi kutoka baadhi ya taasisi za kidini ikiwemo ya kiislamu hamkushiriki kuipindua rasimu ya pili ya Warioba iliyokua mwarobaini wa haya matatizo yote? Mlichukua hatua gani wawakilishi wenu walipoipitisha ile rasimu mpya iliyopata baraka ya watu wa mlengo mmoja wa kisiasa huku wengine waliojiita ukawa wakitoka?

Rasimu ya Warioba ilifuta vyeo vya Ma-RC na Ma-DC, ilipunguza mamlaka ya raisi ktk uteuzi nk. lakini vyote baadae vilirudishwa kama ilivyo kwenye hii katiba ya sasa ya mwaka 1977!! Mvumilie tu maumivu kwa kweli hakuna namna ya kuwasaidia.
 
Ndo tatizo LA viongozi wa Africa kila raisi huvutia kwake akipata uongozi. Hizo ndo favouratism na nepotism haishangazi hata ku complain mana jk naye aliwabeba sana watu wake mfano Chuo cha Udom udini ulivotamalaki

Si unaona sasa unaonyesha double Standard, Wakiteuliwa waislamu mfano hapo UDOM unasema udini huo!
Lakini wakiteuliwa Wachache na wakalalamika unasema hapa ni ishu ya kuzingatia ujuzi tu na elimu na si dini ya mtu n.k
 
Mleta mada ni mtu mufilisi kabisa asie na mbele wala nyuma, ukimuona mtu anaaza kuangalia mambo ya UDINI huyo ni Cancer na anatakiwa apuuzwe, adhauliwe, aogopwe kama njaa!
Wewe ndiye usiye na mbele wala nyuma,wakati wa JK akiteua waislam wanne Kati ya watu kumi ulikuwa unaharisha maneno maachafu sana
 
Ninakumbuka mpaka mzee Mtei alishawahi kumsema JK ni mdini.

"Kwa mwali ikiliwa na kwa kungwi pia"
 
Magufuri si mdini kabisa. uteuzi wa wakuu wa mikoa 19 wakristu na 7 waislamu. wakati serikali iliyopita wakristu walikuwa 5 tu wakati wa uteuzi wa awali wa jk
Ww ndo mdini unaletwa takwimu zako za nin! Kwan dini ni jina au imani? Tunataka maendeleo eboo
 
Bakwata bwana kwenye kampeni mlimsifu leo mnatoka povu la udini, tulieni sindano iwaingie
 
Magufuri si mdini kabisa. uteuzi wa wakuu wa mikoa 19 wakristu na 7 waislamu. wakati serikali iliyopita wakristu walikuwa 5 tu wakati wa uteuzi wa awali wa jk
Ningeshangaa sana kama mada kama hii isingeletwa hapa!
 
Watu wengine udini utawaua. Kila kitu kinaangaliwa kwa ukristu na uislam, kweli??
 
Bakwata bwana kwenye kampeni mlimsifu leo mnatoka povu la udini, tulieni sindano iwaingie
Sio kila muislam ni mfuasi wa taasisi ya Bakwata elewa hilo,rudi katika mada.Miaka kumi yote ya teuzi za JK zilizua mijadala ya udini sasa leo iweje kwa Magufuli tukae kimya? Mwenyewe aliahidi kwamba atakuwa rais wa wote bila kujali dini,vyama au rangi ya mtu.
 
Bakwata bwana kwenye kampeni mlimsifu leo mnatoka povu la udini, tulieni sindano iwaingie
Hata Kikwete mlisema ni chaguo la mungu lakini kwenye teuzi zake mlisema ni mdini.Tulia jipu likamuliwe
 
SIFA UWE john, petro, jacob, paul! yaani uwe mgalatia
 
Back
Top Bottom