Kama Simba iilivyoangukia pua mbele ya Mbeya City leo, ndivyo ambavyo siku ya siku, chama dola kitaanguka kutoka madarakani hata wakibebwa na dola

Kama Simba iilivyoangukia pua mbele ya Mbeya City leo, ndivyo ambavyo siku ya siku, chama dola kitaanguka kutoka madarakani hata wakibebwa na dola

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Leo tumeona jinsi Refa alivyojitahidi kuwabeba Simba lakini haikusaidia. Kama ilivyotokea kwa Simba, ndivyo itakuja kutokea kwa chama dola siku ikifika ambapo hata wakibebwa, mwisho wa siku waatanguka tu na kuachia madaraka.

Siku hiyo ikifika, itakuwa hivi:

Nguvu ya umma itakuwa kama wachezaji wa Mbeya City

Tume ya uchaguzi itakuwa kama Refa wa mchezo wa leo

Wasimamizi wa uchaguzi watakuwa kama wachezaji wa Timu ya Simba kwenye mechi ya leo

Watakaokuwa kwenye tallying center, watakuwa kama waliokuwa kwenye benchi la ufundi la Timu ya Simba leo

Dola itakuwa kama mabeki wa Simba kwenye mechi ya leo

Mashabiki wa chama cha kijani watakuwa kama wa Simba ya leo

Mashabiki wa upinzani watakuwa kama wale wa Mbeya city ya leo

Mabomu ya machozi na risasi za moto(kama zitatumika), zitakuwa kama ule mpira wa penati uliogonga mwamba

Maboksi ya kura yatakuwa kama nyavu za simba

Karatasi za kura zitakuwa kama ule mpira/mipira iliotumika kwenye mechi ya leo

Mwenyekiti wa Tume atakuwa kama mpiga penati wa Simba iliyocheza leo

Ukumbi wa kutangaza matokeo utakuwa kama uwanja wa Sokoine Mbeya siku ya leo.

Time will tell.

Kwasababu soka ina mashabiki wengi,naamini hata wale wasiofuatilia siasa ,watachungulia hapa japo kidogo(mashabiki wa Simba mtanisamehe kwani lengo ni ujumbe ufike bila chenga).

Mfungaji wa goli la leo(Paul John Nonga) katika ubora wake:

1642448350619.png



1642448542174.png
 
Leo tumeona jinsi itakuja kutokea kwa chama dola siku ikifika ambapo hata wakibebwa, mwisho wa siku waatanguka tu na kuachia madaraka.
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip, kwanza neheshimu mawazo yako hata kama sikubaliani na wewe!, pili hakuna ubaya wowote kwa mtu kuwa a wishful thinker, ila kama unasusubiri siku CCM ianguke, kiukweli, utasubiri sana!, kama fisi anavyonyemelea nyuma ya binadamu anayetembea kwa jinsi mikono inavyopishana, masikini fisi anaamini imelegea karibu itaanguka!.
P
 
Mkuu Kishina, utasubiri sana !
P
Hata mashabiki wa Simba walikuwa hawaamini kuwa kilichotokea leo kinaweza kutokea.

Hata Lema wakati anatabiri anguko la Job, wengi walimuona kama anaota.

Nakuhakikishia hiyo siku yaja na hamtoamini.

Anguko la chama dola laja, tusichokijua kwa uhakika ni mazingira gani yatapelekea anguko hilo, au kwa maneno mengine, ni mazingira gani yatasababisha anguko hilo.
 
Mkuu Kishina, utasubiri sana !
P
Paschal kwanini umemjibu atasubiri sana?

Kumbe mnajua njia mnazotumia kushinda uchaguzi?

Lakini hakuna kitu kiliwahi kudumu bila kupotea.

Kwa majirani kulikua na KANU hawa walikua ngangari kweli kweli ! ila walikuja kuangukia pua.

Kuna kizazi kinakuja ndio naona kabisa kitakua kizazi cha mageuzi CCM hamtoamini , ujinga wa watanzania mliotumia kama mtaji kuanzia 1970's utakwisha.

Kuna siku watu watambua haki zao vyema na ndio macho yatafunguka.

Sishangai kwanini unawish CCM iendelee kuwepo sababu wewe ni mnufaika tangu ukiwa kijana mdogo.
 
Moja kati ya mfano wa kiboya sana tangu tuuanze mwaka
From my point of view:

People with great minds, take time to ignore things that they see, hear, read, etc; whereas, those with small minds, take no time to ignore what they see, read, hear, etc.
 
From my point of view:

People with great minds, take time to ignore things that they see,hear,read, etc; whereas, those with small minds, take no time to ignore what they see,read ,hear, etc.
Hakuna cha great minds, kama umezingua unachanwa kueleweshwa wapi umefakisha afu tunawekana sawa mchongo unaishia hapo

Hivyo ndo tunavyo ishi
 
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip , hakuna ubaya wowote kwa mtu kuwa a wishful thinker, ila kama unasusubiri siku CCM ianguke, kiukweli, utasubiri sana!, kama fisi anavyonyemelea nyuma ya binadamu anayetembea kwa jinsi mikono inavyopishana, masikini fisi anaamini imelegea karibu itaanguka!.
P
P, ndugu kishina Cha mshahara amepata maono, na maono haya yapo dhahiri sana, Kaa tulia naamini katika kurejesha kwako kwa jamii , utayachambua upya maono ya ndugu Salary slip.
 
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip , hakuna ubaya wowote kwa mtu kuwa a wishful thinker, ila kama unasusubiri siku CCM ianguke, kiukweli, utasubiri sana!, kama fisi anavyonyemelea nyuma ya binadamu anayetembea kwa jinsi mikono inavyopishana, masikini fisi anaamini imelegea karibu itaanguka!.
P
Unakumbuka kampeni za 2015 zilikuaje?
Time will tell
 
Back
Top Bottom