Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kusomesha mtoto english medium inaweza isiwe shida ila tatizo ni pale mtu anapong’ang’ania mwanae asome Feza au Tusiime kwa kusumbua ndugu na jamaa ili wamchangie

Nilishakataa huo upuuzi. Kila mtu abebe mkonga wake

Hao wanaosumbua watu wako wengi sana
 
english haina umuhimu wowote kwenye sayansi labda kwenye history huko, lakini sayansi ni Ujiniazi wako tu mkuu. Wewe endelea kubishana na sisi tu.

Upo sahihi.. physics , chemistry na hesabu hata wazungu wengi hawaziwezi.. english sio factor kwenye sayansi
 
Upo sahihi.. physics , chemistry na hesabu hata wazungu wengi hawaziwezi.. english sio factor kwenye sayansi

Acheni kujidanganya wakubwa, Nipo Canada hizi hadith za abuniuasi wazee, Hivi unategemea uajiriwe English speaking countries kisa una A ya Phys, SAHAUU, utazungumza nini kwenye vikao, bora uwe na C ya physics, C ya Kemia na C ya hesabu huku unateme ngeli
 
Mshahara haueleweki, unakuta mtumishi anasomesha watoto watatu shule ya mabasi ya njano, Kivumbi na jasho.

Sehemu nyingine familia haina kipato Cha uhakika mathalani ni wafabiashara ndogondogo nao huingiwa na ulimbukeni kupeleka watoto huko matokeo yake ni madeni na maisha ya aibu.

Wazazi wengine huenda mbali zaidi mpaka kuuza ardhi ya familia Ili wapate ada ya shule.

Kuuza ardhi ya familia kwa ajili ya ada ni ujinga wa hali ya juu sana kwa zama hizi.
 
True.. mtu analipa milioni 3 ama nne kwa mwaka ili mwanae ajue kiingereza tu. Huku sylabus anayofundishwa mwanae wa tusiime ni ile ile ambayo wa elimu bure anafundishwa. Tofauti ni lugha tu.

Tatizo la elimu yetu ni sylabus. Jaribu kuwaza hiyo milion 3 kila mwaka mnunulie kiwanja ndani ya miaka 7 atakuwa na asset kiasi gani huyo mtoto.

Mtoto atakuwa na uhakika wa kupata elimu ya juu ama basic need hata kama mzazi umefariki.
Cha ajabu atakuja kuonba kazi na Hawa wa kayumba na bahasha mtaani wakati primary school amemaliza tandam ya m60...ungejenga hoteli au real estate angemaliza angekuwa na Cha kufanya
 
Back
Top Bottom