Kama siyo mlemavu sikushauri utumie choo cha kukaa nyumbani kwako

nice message
 
Ni ushamba wa waswahili wenzetu hawali vyakula vizito hivyo haja yao kama bata tu sasa sisi waswahili ugali wa uwele kwenye haja bila msaada wa kidole hupati choo na choo Cha kukaa kifuatacho bawasili tu.
 
Ushauri wako ni mzuri na una nia njema japo hukuzingatia baadhi ya hali za watu.
Kwanza watu wazito kuchuchumaa na kujikamua hakuawfai.
Na kwa vile wewe ni fundi ujenzi nakushauri kuanzia sasa anza kujenga fremu mbele ya choo cha kukaa ya mtu kujishikilia wakati akifanya shughuli yake ili uzito usiende chini muda wote anaokuwa hapo.
 
Kiujumla squatting position is the overall best .kuchutama ndio asili ya amumbile.na ukizoea vya kukaa hata kijana siku ukikuta cha kuchuchumaa miguu inavibrate kama simu, ila cha kukaa nacho ukiwa mgonjwa kinasaidia sana,
 
Vitu vizuri kwako anasa..umezoea shida ww...
Choo cha kukaa ni kizuri sana unashusha mzigo comfortably...
Tafuta hela upate mambo mazuri
 
Sio hoja maana vyoo vya kukaa ni asilimia 85 dunia kote vinatumika... muhimu watu wazikatie usafi kwenye vyoo..

Ila nnyaa ikubane isubili sijui uchuchumae weee ulisikia wapi..! Ukishikwa na haja tii sheria bila shuruti utadhalilika..
 
Mkuu choo cha kukaa kipo kitambo, wafalme wa uingereza walikuwa na hadi mtu wakupasha choo joto kabla hajaenda kujisaidia kwa hiyo havikubuniwa kwaajili ya walemavu.

Ila una hoja Mkuu. Bawasiri inawasumbua watu wengi sasa sababu ya hivi vyoo na ulaji wao. Ukitumia hicho choo kula sana matunda na maji. Kifupi kula mlo kamili plus usafi wakutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…