Kama siyo mlemavu sikushauri utumie choo cha kukaa nyumbani kwako

Mimi kama Fundi ujenzi na umeme pokea ushauri wangu.

Watu wengi sana wanaamini choo cha kukaa ni bora zaidi. Ukweli ni kwamba choo cha kukaa kilibuniwa kwa mara ya kwanza ili kukidhi mahitaji ya walemavu na wazee wasioweza kuchuchumaa.

Maumbile ya mwanadamu hususani mwafrika yanafunguka vizuri zaidi anapochuchumaa ili kujisaidia kuliko akikaa.

Sehemu za haja zimeumbiwa seal (mfuniko) ambao ili ufunguke ni lazima binadamu achuchumae ndipo swichi iliyopo kwenye ubongo iruhusu kusukuma uchafu (haja).

Hilo kufanyika kinyume chake ni sawa na kuulazimisha kukata kifuniko hicho kwa nguvu (seal)
Ambapo ni hatari sana kiafya.

Miongoni mwa madhara yanayoweza kumpata binadamu kwa kutumia choo cha kukaa;
1. Kukata au kulegeza seal kifuniko cha haja kubwa
2. Inaweza sababisha Bawasiri
3. Haimalizi haja hususani kwa watu wasiyokunywa maji mengi

Faida za kuchuchumaa wakati kujisaidia;
1. Mwili ndivyo ulivyoumbwa ndiyo maana makalio yaligawanywa pande mbili ili uchuchumae
2. Ni sehemu pekee ya kuupa mwili mazoezi
3. Ni kipimo cha kujitathimini afya ya uzito na mifupa (ukiweza kuchuchumaa na kunyanyuka kirahisi)
4. Humaliza haja yote

Kipi kifanyike ili kulinda muonekano mzuri wa choo;
1. Kwa watumiaji wa vyoo vya kuchuchumaa vipo vifuniko vizuri vinavyeleta muonekano mzuri chumbani
2. Kwa watumiaji wa choo cha kukaa, zipo bench au Vikanyagio vya pembeni ambavyo unaweza kuviweka kwenye choo chako pembeni ili kukusaidia kukanyaga na ukajisaidia pasipo kukaa! (Na vikanyagio hivyo unaweza kuvitoa wakati wowote ukihitaji maana ni vya kusogeza kama viti) ili muonekano wa chumba chako ubaki na hadhi ileile

View attachment 2886667
Logic [emoji1434][emoji1434]
 
Kuna mahali nilienda nikalala kumbe kuna choo cha kukaa nilishindwa kabisa nilipanda kwa juu sasa kutoka mahali tiggo ilipo hadi kwenye yale maji pakawa mbali nikiachia furushi kinaenda kudondokea kwenye maji pwaaaaa maji yanaruka naloa hadi miguuni nachafuka ile siku nililaani sana.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kuchuchumaa kunaleta ganzi kwenye miguu damu haizunguki vizuri Kipande hicho ikizingatiwa haja za siku hizi zinachukua mda mrefu.

Ukiona hivyo ujue uzito wa mwili wako ni mkubwa kuliko miguu yako inayoubeba.

“haja za siku hizi zinachukua muda mrefu.” Ningependa kujua zaidi hapa utofauti wa “haja za siku hizi na hizo za zamani.
 
Ukiugua miguu au ukiwa na mgonjwa asiyeweza kuchuchumaa utaenda kuomba ajisaidie kwa jirani? tumia akili japo kidogo na usitafute kupotosha watu humu...
 
Kwani unakoment pasipo kusoma Mada ndugu!?
Mbona nimeeleza wazi kabisa vyoo vya kukaa lengo lake kuu ilikuwa wazee, walemavu na wagonjwa.

Ambacho hujaelewa nini
 
Nilienda nchi moja ya ulaya, vyoo vya kuchuchumaa havitumiki tena......kwa hiyo wao hawana akili, mwenye akili ni wewe unaekuja na hoja zisizo na mashiko za kutaka watu wachuchumae chooni eti kwa sababu siyo wagonjwa, wazee wala walemavu, kwamba ndo njia pekee ya kufanya mazoezi ya mwili!!!​
 
Kwani wanaofanya ushoga wote hawana akili? ..
 
Tatizo hutaki kukubali kwamba umekurupuka, kwamba uweke choo cha kuchuchumaa ndani......siku ukiugua miguu uking'oe uweke cha kukaa, kwa nini usiweke cha kukaa moja kwa moja......punguza ujuaji usio na maana.
 
Tatizo huelew hata unachouliza, mimi nimeshauri kutokana na uhalisia siyo mihemko!
Soma mada inajieleza wazi kabisa kwamba unaweza kuwa na choo cha kukaa ukaweka side bench za kupanda,
Pia kiufundi ukiwa na choo cha kuchuchumaa unaweza funga cha kukaa pasipo kutindua cha kuchuchumaa!!
 
Kwa nini uingie gharama hizo zote wakati kuna short cut ya kutengeneza choo cha kukaa moja kwa moja!

Kwamba haiwezekani kufanya mazoezi ya kuchuchumaa hadi uende chooni?......sababu ulizotoa zote ni dhaifu sana na umeziokota okota tu kwenye vijiwe vya kahawa.​
 
Maumbile ya mwanadamu hususani mwafrika yanafunguka vizuri zaidi anapochuchumaa ili kujisaidia kuliko akikaa.

Mkuu hili ni kwa binadamu wote
Wazungu wanalazimisha tu ingawa nao wanashauriwa hivyo hivyo kuwa vya chini ndio mahali pake
 
Kwa nini uingie gharama hizo zote wakati kuna short cut ya kutengeneza choo cha kukaa moja kwa moja!

Kwamba haiwezekani kufanya mazoezi ya kuchuchumaa hadi uende chooni?......sababu ulizotoa zote ni dhaifu sana na umeziokota okota tu kwenye vijiwe vya kahawa.​
Unafaham gharama kurekebisha haja ya mtu iliyoharibiwa?
Unafaham madhara ya bawasili kisaikolojia? Unafahama madhara ya mwanaume ambaye seal imeachia anapungukiwa na urijali?

Mungu kaumba ile sehemu ibane mtu anapokuwa wima au kukaa! Sasa ukilazimisha kuachia inapolegea lazima madhara yatakukuta tu,

Choo cha kukaa kilibuniwa kwa ajili ya wagonjwa,wazee na walemavu hapo awali kabla ya kuanza kutumiwa na watu wazima
 
Ushauri mzuri sijui watu wasio na mahitaji maalum wanapendea nini hivyo vyoo
 
Unafaham gharama kurekebisha haja ya mtu iliyoharibiwa?
Unafaham madhara ya bawasili kisaikolojia? Unafahama madhara ya mwanaume ambaye seal imeachia anapungukiwa na urijali?

Mungu kaumba ile sehemu ibane mtu anapokuwa wima au kukaa! Sasa ukilazimisha kuachia inapolegea lazima madhara yatakukuta tu,

Choo cha kukaa kilibuniwa kwa ajili ya wagonjwa,wazee na walemavu hapo awali kabla ya kuanza kutumiwa na watu wazima
Hapa unachoongea ni dhana tu, huna backing yoyote ya kisayansi wala tafiti........ndo maana nikakwambia hoja yako ni dhaifu.
 
Unafaham gharama kurekebisha haja ya mtu iliyoharibiwa?
Kuna tatizo la watu kuharibika haja sababu ya vyoo vya kukaa. Hilo Tatizo ni kubwa kiasi gani jamii isilione wenyewe? Maana hata matukio tu kwenye jamii yangejieleza kuwa kuna hii shida.
Unafaham madhara ya bawasili kisaikolojia? Unafahama madhara ya mwanaume ambaye seal imeachia anapungukiwa na urijali?
Choo cha kukaa kilibuniwa kwa ajili ya wagonjwa,wazee na walemavu hapo awali kabla ya kuanza kutumiwa na watu wazima
Kila ubunifu una chanzo. Na chanzo huwa ni kutafuta kutatua tatizo.
 
Punguzeni uchafu majumbani mwenu tumieni vyoo vya kupumzika vya kukaa uchafu wenu unawafanya muone hivyo vyoo sio vizuri ila nimegundua hivyo vyoo vinataka watu wasafi kweli...
 
Back
Top Bottom