komasalonde
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 1,783
- 2,479
Huyo Elon Musk, hataki siasa ila anataka kujilinda na mali yake. Siasa seriously ilikuwa wakati wa Nyerere, unaingia kwenye siasa hata baiskeli huna, ila kuwatumikia wananchi. Sasa hivi huna some millions usijaribu kugusa siasa. Wingi wa pesa ndiyo wingi wa kura.Elon Musk tajiri namba moja dunia hakuna alichokosa dunia hii lakini amempambania Trump kwa nguvu moja na Trump amemteua kwenye position fulani baada ya kushinda.
Sasa tajiri namba moja dunia anakubali teuzi na anapambana siasa na hakatai teuzi.
Wewe hujui hata kesho utakula nini ila unasema eti siasa haikuhusu. Au tatizo ni elimu tu ya watanzania ya kuhudhuria vyuo tu bila maarifa yoyote. Vyuo kama SAUT hakuna mwenye GPA chini ya 4 lakini kichwani empty.