Kama takwimu za miradi ya maendeleo inayotekelezwa zingewafikia Watanzania wote, Wanaokosoa jitihada za Serikali hii wangezomewa sana na Watanzania.

Kama takwimu za miradi ya maendeleo inayotekelezwa zingewafikia Watanzania wote, Wanaokosoa jitihada za Serikali hii wangezomewa sana na Watanzania.

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Toka Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kuna awamu 5 za utawala zimepita, kwa namna yake kila awamu imefanya mambo makubwa kwa wakati wake, kuanzia kwa Baba wa Taifa Hayati J.K.Nyerere, Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa (Mungu ampe pumziko la milele), Mzee wetu Profesa Jakaya Mrisho Kikwete, na Dr John Pombe Magufuli( Endelea kupumzika kwa amani)

Awamu zote zimefanya mambo makubwa yaliyotufikisha leo hapa tulipo. Awamu ya sita iliyo chini ya Dr Samia Suluhu Hassan iliyopo madarakani kwa takriban miaka miwili imefanya mambo makubwa saana ya maendeleo kwa Watanzania.

Ni kweli kuna changamoto ambazo Tanzania kama sehemu ya dunia imepitia kama ugonjwa wa Covid, kuyumba kwa uchumi wa dunia etc lakini bado Serikali ya awamu ya sita imetekeleza miradi mikubwa ya maendeleo bila kutetereka, kama Watanzania kwa umoja wetu tungekuwa tunapata takwimu zote za miradi ya maendeleo inayotekelezwa na awamu hii, wakosoaji wote, wanaharakati wa kupinga bila sababu na wale wapinzani wakutoona nzuri linalotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita Wangefurushwa na kubezwa na Watanzania, wasingepata agenda kwa Watanzania.

Yawezekana Watanzania hawapati taarifa zote sahihi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile
1. Ujenzi wa madarasa yaliyojengwa kwa kipindi cha miaka miwili- Hakuna shule yenye upungufu wa madarasa kwa sasa.
2. Ujenzi wa Zahanati, Vituo vya Afya na Hospital - Kila kijiji kina kina zahanati, kila Kata ina kituo cha Afya na Kila Wilaya ina Hospital yenye vifaa na dawa
3.Ujenzi wa Shule mpya za Serikali kila kata.
4.Ujenzi wa shule maalum mchepuo wa Sayansi kwa Wasichana kwa kila mkoa
5.Ujenzi na ukamilishaji wa maabara za Sayansi kweye shule za Sekondari
6. Ujenzi na uboreshaji wa nyumba za Walimu kwa Shule za Msingi na Sekondari- ujenzi unaendelea.
7. Ujenzi wa barabara na madaraja, kama daraja jpya la wami, ukamilishaji wa mradi wa mwendokasi barabara za DSM ikiwa ni pamoja na njia ya mbagara -posta.
8. Ujenzi wa SGR
9.Ujenzi wa JNHPP
10. Ujenzi mpya wa barabara kiwango cha lami.
11. Uboreshaji huduma za kilimo ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku - mbolea
12. Uboreshaji wa huduma za maji ikiwa ni ujenzi wa miradi mipya ya maji kama uchimbaji wa visima vipya na mradi mkubwa utakaoleta maji DSM toka mto Rufiji
13. Elimu msingi bure.
14. etc

Ifike muda Watu waache kukosoa tu bila sababu, kazi kubwa inafanyika ya kuwaletea Watanzania maendeleo tena katikati ya changamoto kama vile ukame na kuyumba kwa uchumi wa dunia.

Muhimu kwa sasa ni vitengo vya habari viimalishwe ili kuweza kutoa taarifa sahihi kwa wakati, Miradi mingi ya maendeleo inatekelezwa na ni muhimu Watanzania wapate taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu mbariki Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
 
Back
Top Bottom