Kama Tanzania ingeshindwa vita ya Kagera: Je, Rwanda na Uganda zingefika hapa zilipofika leo?

Mimi huwa nasemaga kila siku kwamba utakapotangaza nia ya Uraisi wa JMT mimi ntajitolea kupiga kampeni kuanzia Masasi hadi Muleba hata kwa mguu!

Braza umetisha sana na umechambua vizuri mno na hili ndilo jibu nililokuwa nalitafuta hapa. Ambacho mimi huwa kinanifanya nifikirie ni kuhusu Mzee Nyerere, hivi hadi wakina Museveni na Kagame wanaanza kufanya vurugu kule Uganda ina maana Tanzania hatukufikiri hata kidogo?

Maana ukiangalia matukio ya Afrika Mashariki hadi kufika mwaka 1998 Tanzania ilikuwa inayafuatilia kwa umakini sana. Kama unakumbuka wakati mauaji yanatokea Rwanda kulitokea mvutano mkubwa sana baina ya Mzee Nyerere na Mwinyi ambapo alitaka Tanzania ifanye kitu na kuita hadi waandishi wa habari lakini Mzee Mwinyi akafunga vioo vyote na kuweka mziki mkubwa. Sijui kwanini ilikuwa iko vile lakini inaleta sana maswali.

Upande mwingine, wakina Kabila, Museveni na Kagame walivyomtoa Mobuthu kule Zaire mwaka 1997 Mzee Nyerere alionekana kufurahishwa sana na kile kitendo na baada ya lile tukio akaenda kabisa kutoa muhadhara kwa uongozi mpya kwamba "Zaire haina wajomba watakaoiletea maendeleo".

Ina maana Nyerere alikuwa hana ufahamu wowote juu ya tabia za hawa jamaa wawili ambao amekaa nao tokea vita za Msumbiji, Uganda na Rwanda kwa wakati wote huo? Mara nyingi alikuwa akienda kwenye mikutano mikubwa alikuwa akijisifia sana kumtoa Mobuthu na unaona kabisa alikuwa anawafahamu Museveni na Kagame vizuri.

Kaka Chige kuna baadhi ya mambo huwa yanaacha maswali mengi sana yenye ukakasi kuliko majibu yenye kueleweka!
 
This is deep!
Narudia kusoma mara mbilimbili hili bandiko. Braza wewe una akili nyingi sana.
 
Sikuwahi kuwaza kama ushindi wa Tanzania kwenye vita vya Kagera ulikuwa na faida kubwa sana ya kisiasa kwa Rwanda na hasa mpaka kumpata huyu raisi wao wa sasa.

Ngoja niendelee kufyonza matarials hapa....
 

Hapo kuna kuangalia kwanini mpaka miaka hii Rais wa nchi ya Africa anapendelea zaidi watu wake kushika nyadhifa nyingi (zote?) muhimu serikalini na impact yake ni nini kwa nchi husika kwa muda huo au baadae.

Ni mambo mengi hapa ya kuongelea. Labda ingeanzishwa Uzi wake.

Lakin kuna hii historia, ambayo hata baada ya miaka 50 au 60 bado haijatuacha salama. Mbelgiji mmoja akiielezea Kongo miaka ile alisema ile si nchi Ila a bunch of tribes. Mkusanyiko Fulani wa makabila. Na yasiyo na umoja wa aina yoyote.

Wazungu walipotutawala walijaribu kututenganisha kwa dhati. Wakiona dini haiko effective walitumia ukabila/ ukanda. Hilo lisipofanya kazi walihamia kwenye kimo, umbo LA pua na nk kama kwa ndugu zetu Rwanda, Burundi. Tofauti zetu ziliimarishwa zaidi ya ufanano wetu. Hili linatutesa mpaka leo. Na kwa baadhi ya nchi hili ndio chanzo cha mitafaruku isiyoisha
 
Mtikila alianza kutuhumu kwama Mzee alikuwa ni mtu wa Bahima. Ila kwa ujumla ile vita ndio mstabali wa kinachoendelea hivi sasa katika nchi za maziwa makuu. Mambo mengi sana yametukia baada ya ile vita. Iwapo Amini angeshinda naona maisha nayo yangekuwa tofauti kabisa.
 
Vita ya Kagera ilizaa mambo mengi sana kwenye ukanda huu ambayo yanatokea leo hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…