Kama Tanzania ingeshindwa vita ya Kagera: Je, Rwanda na Uganda zingefika hapa zilipofika leo?

Anhaaaaaa. Sawa mkuu
 
Hii kitu ipo mkuu,kuna dada miaka kama 7 nyuma alikua anajitangaza mrwanda,hadi kwenye profile yake ya facebook aliweka from gisenyi,ninavyokuambia hivi sasa ni diwani simiyu huko,na yuko close sana na baadhi ya waheshimiwa wa CCM, kipindi cha bunge umkosi mitaa ya Dodoma
 
Aisee !!!
 
Nakubaliana na wewe kabisa lengo la M7 lilikuwa nikuongoza Uganda na ndio maana sasa hivi kuna kauli kule kuwa "

"wakati tukikuwa tunaoigana msituni mlikuwa wapi?"

Yaani kule kuna watu hawaguswi kabisa ukitaka kuwagusa unakutana na hiyo kauri hapo juu.
 
Huo msemo upo hadi Leo na Mwalimu pamoja na Wazanaki wenzake waliutumia kuwagandamiza wajita kwa kuwanyima huduma muhimu kama shule. Maeneo ya kuzunguka wajita shule zilikuwa chache sana.
Inawezekana Ndio. Wazanaki ni jina walilopewa na Wajita. Ukilitamka kwa sauti ya kikabila za kibantu ina maanisha "Ulikuja na nini". Wajita waliwadharau kwa kuwauliz walikuja na nini zaidi ya mifugo?

Bazazi
 
Sasa hapa niweke wazi na Nyerere alikuwa ni sehem mpango wa Hima empire dominance au alikuwa akichezeshwa ngoma asiyoijua?
 
Huo msemo upo hadi Leo na Mwalimu pamoja na Wazanaki wenzake waliutumia kuwagandamiza wajita kwa kuwanyima huduma muhimu kama shule. Maeneo ya kuzunguka wajita shule zilikuwa chache sana.
These are very serious allegations.
 
Malcom Lumumba,

Watu hawatengenezi historia, ni historia inayoandaa watu wa kuja kuitengeneza. Hivyo kuna kuwepo na future then mchakato wa kuitengeneza future au kuandaa watu wa kuja kuitengeneza hiyo future huanza.
Kama Uganda angeishinda Tanzania basi huenda British na France zingepigana ili yaliyopo hivi sasa yawe.
 
With reference mkuu
lini Tz ilikuwa na influence over other African states ?
Hadi kufika miaka ya themanini mwishoni Tanzania ilikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa mataifa mengi ya Afrika. Hebu tuangalia machache tu kwenye uwanja wa diplomasia.

Mosi, Tanzania ilileta kitu kinachoitwa Nyerere's Doctrine of State Succession ambacho kilielekeza jinsi gani nchi inaweza kushughulika na mikataba yote ambayo ilisainiwa na wakiloni. Mwalimu Nyerere alisema litakuwa ni jambo la kipuuzi kama mikataba ya Kikoloni iliyosainiwa na Serikali za kikoloni itaendelea kuwa na nguvu hata baada ya Uhuru.

Utaratibu wa kanuni hii ni kwamba ni kwamba nchi ikishapata Uhuru inatoa miaka miwili ya neema kwa nchi ambazo zilisaini mikataba ya kikoloni kuamua kama zinataka kuendelezea hiyo mikataba au kutoendeleza kwa kuandika barua (Exchange of Notes). Miaka miwili ikipita na hakuna kilichofanyika mikataba inakufa.

Sasa mpaka kufika mwaka 1973 nchi sita za Afrika ikiwemo Kenya zilifuata hii kanuni ya Nyerere's Doctrine of State Succession katika kishughulikia mikataba ya kikoloni.

Pili, mwaka 1963 Mwalimu Nyerere ndiye aliyeshauri nchi za Afrika zifuate kanuni inayoitwa The Doctrine of Intangibility of Frontiers ambayo iliseme nchi za Afrika zisibadilishe mipaka iliyochorwa na mkoloni ili kudumisha amani barani Afrika. Hii kanuni iliheshimiwa na nchi nyingi huru za Afrika. Kanuni hii waliiga kutoka nchi za Amerika Kusini, na Nyerere ndiyo aliyependekeza itumike hapa Afrika.

Natumai hizi rejea zimekutosha kwa leo !
 
Hata hivyo DRC ingekuwa kama Rwanda unadhani PK asingekuwa anaitawala yaani angekuwa Mkoloni wa DRC. Ukubwa wake umemfanya PK ashindwe kuitawala wala kuiteka yote

Bazazi
Labda nikumbushe tu Kagame amewahi Iteka Congo nzima wakati wa 1st congo war ya kumng'oa mobutu kutokea ziwa kivu mpaka port matadi!!

Sio hivyo tu alipotaka kumng'oa Kabila aliiteka tena congo na alifika mpaka kinshasa kabisa na kama sio msaada wa Angola basi angekua ameiteka Congo nzima ndani ya wiki 2 pekee.

Kwenye vita za kileo ukubwa wa nchi hauna maana yeyote sababu vita inapiganwa kwa teknolojia nyingi mfano matumizi ya ndege na makombora ya masafa marefu kwahiyo unaweza zingirwa kwenye anga na kumalizwa ndani ya wiki tu kabla hata majeshi ya ardhini hayajafika Dodoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…