Uchaguzi 2020 Kama TPSF ni wakweli, then, JPM, CCM itashinda ushindi wa kishindo cha ajabu! But for National Unity, TL ateuliwe Ubunge kuwafariji his sympathizers?

Uchaguzi 2020 Kama TPSF ni wakweli, then, JPM, CCM itashinda ushindi wa kishindo cha ajabu! But for National Unity, TL ateuliwe Ubunge kuwafariji his sympathizers?

Paskal acha unafiki sisi ni watu wazima na tunaelewa kila kitu kinachoendelea , hao TPSF ndiyo waathirika wakubwa wa utawala huu wa Magufuri. Kumbuka Magufuri aliwahii kuwaambia wataishi kama mashetani na baadhi yao walienda jela na walifanikiwa kutoka baada ya kutoa pesa...
Wewe ndio mnafiki! Mayalla ameshiriki kikao cha jana lakini pia mkutano ulikuwa live waliwasha luninga zao wameona. Sasa unafiki uko wapi hapo. Acha kumjengea chuki JPM na sekta binafsi. Kwa taarifa yako wale ni viongozi ni wawakilishi wetu tumewatuma wakamshukuru JPM. Mitano 5 kazi inaendelea.
 
Jinsi sekta binafsi ilivyoyumba ....mhh unafiki tuu unaendelea.
Nadhani wewe unaongea kwa mihemko. Jana tumesikia takwim zikitajwa za mafanikio ya sekta binafsi katika kipindi Cha miaka mitano ya JPM. Ama kweli CHADEMA kazi yenu kupinga tu, maana unambiwa tulikuwa na moja sasa tumeongeza zimekuwa tano bado pia unaita unafiki! Ama hakika fikra zenu huwaga zinaongozwa na mahabaniue.
 
Kwenye JPM weka TL. Halafu soma tena uzi wako.

40 ni namba ya kiimani pia. 40 years ilikuwa imeisha 2017, kwa sababu ya utaratibu wa katiba yetu juu ya mambo ya uchaguzi, tukacarry forward kwa 2020.

Kama ambavyo Sauli haikuwa rahisi kuachia kijiti kwa Daudi, ndivyo itavyokuwa. This time si KURA tu zitaamua, lakini NYAKATI zitaamua pia.
 
Nadhani wewe unaongea kwa mihemko. Jana tumesikia takwim zikitajwa za mafanikio ya sekta binafsi katika kipindi Cha miaka mitano ya JPM. Ama kweli CDM kazi yenu kupinga tu, maana unambiwa tulikuwa na moja sasa tumeongeza zimekuwa tano bado pia unaita unafiki! Amahakika fikra zenu uwaga zinaongozwa na mahabaniue.
Unazungumzia sekta binafsi gani? Hii hii hali mbaya kwa wafanyabiashara wakubwa mpaka wadogo?
 
Kwenye JPM weka TL. Halafu soma tena uzi wako.

40 ni namba ya kiimani pia. 40 years ilikuwa imeisha 2017, kwa sababu ya utaratibu wa katiba yetu juu ya mambo ya uchaguzi, tukacarry forward kwa 2020.

Kama ambavyo Sauli haikuwa rahisi kuachia kijiti kwa Daudi, ndivyo itavyokuwa. This time si KURA tu zitaamua, lakini NYAKATI zitaamua pia.
Unaota asubuhi wewe! JPM mitano tena. 28/10/20202 kura zote kwa JPM
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, ikitokea Tundu Lissu ameshindwa uchaguzi huu kihalali katika Uchaguzi Mkuu huru na wa haki, jee tumchagize JPM, for the the sake of national unity, and to heal the nation, amteue Tundu Lissu kuwa Mbunge wa kuteuliwa katika zile nafasi zake kumi za uteuzi as a consolation prize na kuwapooza sympathisers wake watakao mpigia Tundu Lissu, compassionate and sympathetic votes?...
Naamini hakuna sehemu ambayo imeathiriwa vibaya kama Sector binafsi, hivyo TPSF waongo.

This time imekula kwenu asee.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Naamini hakuna sehemu ambayo imeathiriwa vibaya kama Sector binafsi, hivyo TPSF waongo.

This time imekula kwenu asee.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Kama huna data huna haki ya kujibu hoja ambayo imewasilishwa na data. Gala wewe ninani wakati waliowasilisha data na kutoa pongezi viongozi wa mashirika binafsi. Mfano ulianza kule Mbeya wakati CEO wa WCB alipotoa ushuhuda wa mafanikio aliyopata ikiwa yeye pia ni sekta binafsi. Sasa wewe lete takwimu zako ili tusikuone mpayukaji, mnafiki, uliojawa na mahabaniue kwa Mbeligiji wenu.
 
Nadhani sasa umeanza kurudi rudi,bila shaka unaweza kuwa na bifu na hao TPSF,yule mwenyekiti wao aliyekamatwa kwa uhujumu uchumi lazime awe kibra na hiki chama chake.
 
Nadhani wewe unaongea kwa mihemko. Jana tumesikia takwim zikitajwa za mafanikio ya sekta binafsi katika kipindi Cha miaka mitano ya JPM. Ama kweli CDM kazi yenu kupinga tu, maana unambiwa tulikuwa na moja sasa tumeongeza zimekuwa tano bado pia unaita unafiki! Amahakika fikra zenu uwaga zinaongozwa na mahabaniue.
Wewe upo sekta binafsi? Naongelea uhalisia sio maneno ya wanasi - hasa!
 
Wewe upo sekta binafsi? Naongelea uhalisia sio maneno ya wanasi - hasa!
Ndiyo nipo sekta binafsi nimeajili vijana kadhaa tunalima matikiti na viazi vitam hapa. Nashukuru mzigo wangu ambao hauzidi tano moja naufikisha sokoni bila ushuru wowote njiani, pia nimelipia elfu ishirini ya kitambulisho cha ujasuliamali hapa sokoni kwetu sipati usumbufu wowote. JPM mitano tena kazi iendelee
 
hIVI AKILI ZAKO ZINAKUAMBIA LISSU ATALETA AJIRA, KIJANA FUNGUA MACHO NA MSIMPACHIKE MGOMBEA WENU ZIGO ASILOWEZA KULIBEBA. KIJANA NI KAWAIDA KWENYE KAMPENI WANASIASA KUTOA AHADI 100 NA KUTIMIZA 10. KUPUNGUZA AJIRA TANZANIA KWA ASILIMIA 60, ITATUCHUKUA MIAKA KAMA 20 YA UCHUMI USIOPUNGUA 5-7% KILA MWAKA, NA LAZIMA KUWE NA MCHANGANYIKO WA UCHUMI WA BIASHARA, KILIMO, VIWANDA NA MADINI. TUKITEGEMEA BIASHARA ZA KUAGIZA VITU NA KUVIUZA TUU , TUTAZIDI KWENDA CHINI NA KUTEGEMEA NCHI KAMA CHINA KWA BIDHA
Nani amemuongelea Lissu hapa?

Mimi nimeongelea pongezi za TPSF wanaosema miaka 5 imekuwa ya neema kwa sekta binafsi; miaka ambayo Magufuli amekuwa rais. Aliyetoa ahadi na akapewa nafasi ya kutekeleza ni yeye, jama hajaweza Lissu asilaumiwe.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, ikitokea Tundu Lissu ameshindwa uchaguzi huu kihalali katika Uchaguzi Mkuu huru na wa haki, jee tumchagize JPM, for the the sake of national unity, and to heal the nation, amteue Tundu Lissu kuwa Mbunge wa kuteuliwa katika zile nafasi zake kumi za uteuzi as a consolation prize na kuwapooza sympathisers wake watakao mpigia Tundu Lissu, compassionate and sympathetic votes?.

Hoja hii imeanzaje?
Saa hizi ni usiku wa manane, usingizi umekata ghafla nikaanza kuwaza uchaguzi na haswa kitu cha ajabu sana nilichokisikia leo kwenye mkutano wa Taasisi ya Sekta Binafsi, TPSF, pale katika ukumbi Kimataifa wa mikutano, JNICC, hivyo nikaamua kuendelea kuandika zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa".

Declaration of Interest
Naomba kuanza na declaration of Interest
Mimi Pascal Mayalla, japo ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, mimi sio kada fagilia, kada shangilia au kada piga makofi, mimi ni kada Mzalendo ambaye ninatanguliza mbele maslahi ya taifa. Hivyo ukiamua usinisome au usizingatie hoja zangu kwa vile sasa na mimi ni kada wa CCM, rukhsa kuishia hapa, nisije kukukerehesha nikakuharibia bure siku yako ya leo, na kwavile leo ni Jumatatu, ukiianza vibaya, utakuwa umeharibu wiki yako yote.

Kwa vile mimi ni muumini wa ukweli, na uwazi na ninaamini ukweli na uwazi ndio utaliponya taifa, sitaacha kuusema ukweli bayana ili kulisaidia kuliponya taifa langu, Pasco Mayalla licha ya sasa kuwa ni kada wa CCM, lakini Pasco bado ni yule yule juzi jana na leo, na hoja zake ni zile zile za kwa Maslahi mapana ya taifa.

Mkutano wa TPSF
Jana nimehudhuria mkutano wa Taasisi ya Sekta Binafsi, TPSF ambayo ni Taasisi Apex, yaani Taasisi Mwamvuli, an Umbrella Organisation, chini ya mwamvuli huo wa TPSF, kuna taasisi nyingine nyingi zinazo deal na sekta binafsi. Taasisi nyingine zote zilizo chini yake, jana zimemshukuru rais Magufuli kwa mambo makubwa, mazuri na ya kuonekanika aliyo yapanga, akayasema na kuyatenda kwa kuyafanya na kuyatekeleza, hivyo, wakuu wa taasisi zilizo chini ya mwamvuli wa TPSF, mmoja baada ya mwingine, jana walipanda jukaani na kunadi mazuri ya Magufuli kwenye tasisi zao, na kuahidi kuwa wametumwa na wanachama wao, kumpigia kura zote rais Magufuli wamemuhakikishia kura zote wanachama wote walio chini ya mwamvuli wa TPSF zitakwenda kwa JPM na wagombea wa CCM pekee, kwasababu aliahidi kwa kusema na sasa ametenda.

Hivyo kama ni kweli, hao wanachama wa Taasisi zote zilizo chini ya TPSF wameamua unanimously kumpigia kura JPM na CCM, then, kiukweli kabisa, rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, JPM, katika uchaguzi huu, yeye na CCM Itashinda kwa ushindi wa kishindo kikubwa cha ajabu kabisa kuwahi kutokea Tanzania, tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ile 1992!.

Kwasababu nimeshuhudia chaguzi zote 5 za vyama vingi toka ule wa 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na sasa uchaguzi huu wa 2020 ni wa 6!, huko nyuma haijapata kutokea, hii ndio kwa mara ya kwanza, sekta binafsi nayo inatoa msimamo wa kisasa, na kuzungumza kwa kauli moja unanimously kuunga mkono mgombea mmoja wa chama kimoja tuu cha siasa!,
kwasababu hizo taasisi, sio taasisi za kisiasa na zinategemewa wanachama wake wako huru kujinga na vyama vyovyote vya siasa na wako huru kuchagua viongozi wao wowote wanaowapenda kutoka vyama vyovyote, hivyo kama sasa wameamua kwa kauli moj, kutangaza hadharani kumchagua mgombea mmoja, JPM na kuichagua CCM, huu sasa ni uamuzi wa kisiasa, then there is no way Tundu Lissu anaweza kupata kura zozote za maana!.

Hii ya TPSF, ni ukiondoa watumishi wa serikali ambao tunajua watamchagua nani, then TPSF encompasses
1. Wafanyakazi wengine wote wako chini sekta binafsi nchini chini ya TPSF, wakiwemo
2. Wafanyabiashara wote nchini wa biashara zote, wako chini ya TCCIA wameahidi kura kwa JPM na CCM.
3. Wafanyabiashara wote wanawake chini ya TWCC wameahidi kura kwa CCM
4 Wenye viwanda wote chini ya CTI, wameahidi kura kwa CCM
5. Wakulima wote Tanzania chini ya TFA, wameahidi kura kwa CCM
6. Wenye mabenki wote chini ya TBA nao wameahidi kuwashawishi accounts holders wao wote wampigie JPM na CCM
7. Makampuni yote ya simu kuwashawishi subscribers wao wote kumpigia JPM na CCM.
8. Wafanyabiashara ndogondogo wote, wasiosajiliwa, wamachinga, mama lishe, wenye bodaboda wote, madereva, makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu wote wameahidi kura kwa JPM na CCM, hivyo kama hii ni kweli, then its as if rais Magufuli na CCM anakwenda kukomba kura zote za Watanzania wote toka makundi yote ya jamii, swali la kujiuliza ni kama ndio hivyo, nani atachagua upinzani?.

Kwa vile kabla sijajiunga siasa, nilistaafu kwanza uandishi wa habari, hivyo sikuweza kufuatilia ni lini hizi taasisi zote chini ya TPSF zilifanya AGM zake na kupitisha hizo resolutions kumsupport JPM na CCM, na kwa vile AGM zote ni open conferences zinatakiwa kutangazwa, kama kuna yoyote aliyesikia matangazo ya AGM, za taaisi hizo zikiitishwa, atujuze, unless AGM ziliitishwa na media zilialikwa ila kutokana na media kuwa too busy na politics, resolutions za AGM hizi hazikutangaza hivyo hizo resolutions zote halali na ziko valid ila mimi ndio nikazisikia hiyo jana, lakini ikitokea, hakuna vikao vyovyote rasmi vilivyoitishwa na taasisi hizo, kupitisha hizo political resolution kwenye taasisi zao, na badala yake ni vingozi wa Taasisi hizo, wamefikia maamuzi ya kuwaamulia wanachama wao wamchague nani na chama gani na kuyatangaza maamuzi hayo hadharani kuwa wote wameamua kwa kauli moja, bila AGM, bila, bila kushirikishwa, then this leaves much to be desired!, na kwavile kura ni siri, then lets wait for JPM na CCM landslide victory, or surprises iwapo hawakushirikishwa!.

Sasa kwa vile kura zote zimeahidiwa kwa JPM na CCM only, lakini kwenye mikutano ya Tundu Lissu pia inajaza watu wenye too great expectations kuwa Tundu Lissu atashinda, bila kuonyesha atashinda kwa sera zipi, hoja zipi na kura zipi toka makundi gani ya kijamii, lakini kwavile na kiukweli kabisa kwa kilichomtokea Tundu Lissu kushambuliwa na risasi 16 za moto na akapona na sasa ni mgombea, huu ni muujiza mkubwa wa Mwenyezi Mungu na usikute ule umati wa watu katika mikutano ya Tundu Lissu ni umati wa kushuhudia tuu muujiza wa kupona kwa Tundu Lissu na sio umati wa wapiga kura, na akitokea kupata kura, then Tundu Lissu atapata kura chache za sympathetic na compassionate votes kwa maswahibu yaliyomfika.

Hivyo nashauri for the sake of national unity, kwasababu rais Magufuli anakwenda kukomba kura zote za Watanzania wote, haku kuna watu wana too great expectations na Tundu Lissu, mimi kama Mtanzania Mzalendo, katika wiki hii ya mwisho ya kampeni za uchaguzi, namuomba mgombea wetu na Mwenyekiti wa chama changu CCM, JPM, atangaze na ku ahidi wafuasi wa Tundu Lissu kuwa baada ya uchaguzi, atamteua Tundu Lissu kuwa Mbunge wa Bunge la JMT katika zile nafasi zake kumi ya uteuzi, ili Tundu Lissu angalau aweze kurejea Bungeni kuendelea kulichangamsha Bunge letu lijalo and at the same time, kuwafariji wale minority wote waliopanga kumpigia kura za sympathetic votes na compassionate votes, na hivyo to heal wafuasi na washabiki wake?.

Jee wenzangu mnalionaje hili?. si ni jambo jema?. Tena kama hoja za TPSF ni kweli, hii maana yake, Bunge lijalo litakuwa ni Bunge la CCM dominated house, hivyo sio tuu namuombea uteuzi Tundu Lissu pekee, bali namumba JPM pia amteue, hata Zitto Kabwe, na Freeman Mbowe kuwa wabunge, amteue Benard Membe kuwa balozi, Maalim Seif yeye hana wasiwasi ni atakuwa Makamo kule Zanzibar hivyo wafuasi wake watatulia!.

Upendo, Amani, Utulivu na National Unity ni components muhimu sana kumsaidia Magufuli kwenye mitano tena yake.

Nawatakia Jumatatu njema.

Paskali
wanafanya hayo kinafiki magu hapendwi Lisu ni chaguo la watanzania kwa sasa,watanzania wamechoka kunyanyaswa,kuonewa kila kona na huu utawala wa jiwe
 
Pamoja na kutambua ushindi wa JPM upo wazi kabisa kutokana na ugeugeu na unafikir wa upinzani Ila bandiko lako limeegemea ktk kujipa promo na kujipendekeza zaidi.

Paskal tambua JPM anasifika kwa makubwa alofanya ndan ya muda mgupi lakini asifiwi kwa masifa ya mapambio ili mpate vyeo wengine.

Hebu safisha kalamu yako,Kuna mengi JPM kafanya unaweza kuyachambua kwa uweledi na kulinganisha awamu zilopita,Mnashindwa na Masanja mkandamizaji anayeonesha kinaga ubaga nchi ilivyojengwa!

Nataka=njaa isikuharibu kabisa akili, JPM haitaji sifa za kujipendekeza kwa maslahi ya mtu,yule Ni mzalendo na muumini wa uzalendo asili kabisaaa,na Sisi huku mtaani tunamkubali kinomaaaaaaaaaaaaa
Nchi inajengwa katikati ya mauaji, utesaji na utekaji? Kumbuka haki ya msingi kabisa ni ile ya kuishi.
Huwezi kuua ndugu zetu halafu ujenge barabara tukusifu. Hiyo midege sio mbadala wa uhai wa ndugu zetu. R.IP Kamanda Mawazo na watz wengine.
 
wanafanya hayo kinafiki magu hapendwi Lisu ni chaguo la watanzania kwa sasa,watanzania wamechoka kunyanyaswa,kuonewa kila kona na huu utawala wa jiwe
Ndugu yangu wewe unaishi nchi gani? Tanzania kweli au nje ya nchi? Maana unazungumzia JPM ambaye siyo Tanzania bali mpaka nchi jirani wanatamani wapate huduma yake japo kwa siku moja tu.
 
Back
Top Bottom