Kama Tulivyochangishana Michango ya Sherehe, Sasa Tuanze Kuchangishana Michango ya Maendeleo

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Katika maeneo ambayo Watanzania wameonesha ushirikiano wa hali ya juu mno, ni kwenye masuala ya sherehe. Wengi wanaoshirikishwa wamekuwa wakitoa ushirikiano murua kuanzia kwenye uuandaji kamati, kuchangisha michango na hata kula na kunywa.

Miongoni mwa shughuli za sherehe ambazo zimekuwa zikifanyika kwa mtindo huo ni pamoja na harusi na birthday.
Kwa baadhi ya mikoa, hasa yenye Wakristo wengi, kumekuwepo mpaka na sherehe za ubatizo na ubarikio, na mara zote ushirikiano wa wanajamii umekuwa ukihusika.

Kwa nini tusiurekebishe huo utaratibu, badala ya kuchangishana fedha za sherehe, tukafanya hivyo kwa ajili ya maendeleo?

Sidhani kama kuna ulazima wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kula na kunywa, ila kuna faida kubwa sana endapo hilo litafanyjka kwa jambo la kimaendeleo ama kwa ajili ya kutatua tatizo ambalo mhusika ameshindwa, kama matibabu n.k.

Naamini, ni jambo jema endapo tutajijengea utaratibu wa kuwa na harambee kwa ajili ya kuchangishana fedha za kimaendeleo kama vile:

1. Mtaji wa biashara

2. Kugharamia masomo

3. Kuukamilisha ujenzi wa nyumba

4. Kununua gari

5. Kununua shamba au kiwanja

6. Kuvuta umeme na maji, n.k.

Simaanishi sherehe zisiwe zinafanyika, badala yake, zikifanyika, zigharamiwe na wahusika pekee kulingana na uwezo wao. Kama mtu hana uwezo, aachane na masherehe. Hata kama ni anaoa si lazima afanye sherehe, na hata akihitaji sherehe, anaweza akaifanya ambayo ni very simple. Asipike mapilau na makuku, badala yake, aandae chai na karanga, kila mhudhuriaji apate kikombe cha chai na vijiko vitatu vya karanga zilizokaangwa.

Kuna maana gani mtu anayeishi kwenye chumba cha kupanga kutumia zaidi ya milioni moja kwa harusi?

Kwa mtazamo wangu, huoni ufujaji.

Tubadilikeni! Tufurahie kusaidiana katika mambo yatakayokuwa na matokeo ya kudumu kuliko sherehe.
 
Nko pale nasubiria wanakamati wenzangu tuchangiane nataka kununua kagari aisee
 
Nasema toka sakafu ya moyo wangu, ningefurahi sana kama mtu angenipa kadi ya mchango wa kununua gari kuliko ya sherehe.

Ya sherehe nitaichangia, labda tu kulinda uhusiano. Lakini ya kununua gari, nitajitahidi nichangie hata kama hatuna uhusiano wa karibu saaana!
 
Nimependa hiki kilichofanywa na Wakenya kwa Mkenya mwenzao.

Mwanamke mmoja jijini Nairobi amefanikisha kupatikana Ksh 38,800, sawa na laki saba za Kitanzania kwa ajili ya kulipia ada ya kijana aliyekuwa amekwama kuendelea na masomo kwa kukosa ada.

Mwanamke huyo, Kabongo wa Kamau, alibaini kuwa mmoja wa walinzi wanaolinda nyumba yake alikuwa na uelewa mkubwa kuliko mwonekano wake.

Alipomdadisi, aligundua kuwa Ben Oparasi mwenye miaka 27 alikuwa mwanafunzi wa udaktari mwaka wa pili katika cha KENYA MEDICAL TRAINING COLLEGE, lakini alilazimika kusitisha masomo kwa mud ili kutafuta ada. Hiyo ndiyo sababu iliyompelekea kuomba kazi kwenye kampuni ya ulinzi ambayo ilikubali kumlipa mshahara wa Ksh 9,000 kwa mwezi, sawa na Tzs 150,000/=.

Kwa kuguswa na hilo, Kabugo aliamua kuwashirikisha Wakenya wenzake, na ndani ya masaa 24, hizo fedha Ksh 38,800/= zikapatikana kwa michango ya hiari.

Michango bado inaendelea kwa ajili ya kumsaidia Ben mahitaji mengine ya kimasomo, ikiwa ni pamoja na ada ya mwaka wa tatu.

Nimeipenda hiyo! Michango ya aina hiyo ndiyo inayopaswa kupewa kipaumbele.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Tuko.co.ke, na ilichapishwa na Hillary Lisimba tarehe 03/06/2023.
 
Katika maeneo ambayo Watanzania wameonesha ushirikiano wa hali ya juu mno, ni kwenye masuala ya sherehe. Wengi wanaoshirikishwa wamekuwa wakitoa ushirikiano murua kuanzia kwenye uuandaji kamati, kuchangisha michango na hata kula na kunywa.

Miongoni mwa shughuli za sherehe ambazo zimekuwa zikifanyika kwa mtindo huo ni pamoja na harusi na birthday.
Kwa baadhi ya mikoa, hasa yenye Wakristo wengi, kumekuwepo mpaka na sherehe za ubatizo na ubarikio, na mara zote ushirikiano wa wanajamii umekuwa ukihusika.

Kwa nini tusiurekebishe huo utaratibu, badala ya kuchangishana fedha za sherehe, tukafanya hivyo kwa ajili ya maendeleo?

Sidhani kama kuna ulazima wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kula na kunywa, ila kuna faida kubwa sana endapo hilo litafanyjka kwa jambo la kimaendeleo ama kwa ajili ya kutatua tatizo ambalo mhusika ameshindwa, kama matibabu n.k.

Naamini, ni jambo jema endapo tutajijengea utaratibu wa kuwa na harambee kwa ajili ya kuchangishana fedha za kimaendeleo kama vile:

1. Mtaji wa biashara

2. Kugharamia masomo

3. Kuukamilisha ujenzi wa nyumba

4. Kununua gari

5. Kununua shamba au kiwanja

6. Kuvuta umeme na maji, n.k.

Simaanishi sherehe zisiwe zinafanyika, badala yake, zikifanyika, zigharamiwe na wahusika pekee kulingana na uwezo wao. Kama mtu hana uwezo, aachane na masherehe. Hata kama ni anaoa si lazima afanye sherehe, na hata akihitaji sherehe, anaweza akaifanya ambayo ni very simple. Asipike mapilau na makuku, badala yake, aandae chai na karanga, kila mhudhuriaji apate kikombe cha chai na vijiko vitatu vya karanga zilizokaangwa.

Kuna maana gani mtu anayeishi kwenye chumba cha kupanga kutumia zaidi ya milioni moja kwa harusi?

Kwa mtazamo wangu, huoni ufujaji.

Tubadilikeni! Tufurahie kusaidiana katika mambo yatakayokuwa na matokeo ya kudumu kuliko sherehe.
Tatizo tukichangia hizo shughuli zingine mnakula tu na maendeleo hatuyaoni
 
Mkuu, ulishawahi kumchangia mtu na akaishia kuzitafuna?

Vipi wewe, kwa mfano, lakini ni mfano tu, mwanao au wewe mwenyewe ukapungukiwa ada na ukaamua kupitisha mchango, ungezitumia tofauti na malengo?

Au tuchukulie unaishi kwenye nyumba ya kupanga, na, kwa kukerwa na kodi, ukaamua kupandisha kamjengo kako, lakini kabla ya kuukamilisha ujenzi, chanzo cha kipato chako kikapata msukosuko hivyo kushindwa kuukamilisha ujenzi. Ikitokea umeitisha harambee kwa lengo la kushikwa mkono, utazitafuna fedha utakazochangiwa?

Watu hatufanani. Inawezekana kuna watakaofanya kinyume na walivyoahidi, lakini pia kuna watakaotenda kama walivyosema.

Endapo samaki mmoja ameoza, usilitupe kapu lote. Watakuwemo walio wazima.
 
Tunachanga sana kuanzia kwenye ngazi ya familia, jamii inayotuzunguka hadi serikalini
Mambo ni yale yale

Hata humu jf mtu anakuja na mchongo anaomba umpe support unaona huyu anaweza kufanya kitu lakini mwisho wa siku ni aibu tuu

Tunakosa utu na nidhamu ya fedha na kiu ya kufanya maendeleo

Acha tufanye au tuchangie na vitu vyenye kutupa furaha chief maana maisha yanahitaji furaha pia
 
Mkuu, hufahamu?

Kati ya watu wenye furaha sana ni wale wanaofurahia kuwasaidia wengine kufanikiwa.

Anayesaidia wengine kufanikiwa, Kisaikolojia, ananufaika zaidi kuzidi anayesaidiwa.
 
Tunachanga sana kuanzia kwenye ngazi ya familia, jamii inayotuzunguka hadi serikalini
Mambo ni yale yale

Hata humu jf mtu anakuja na mchongo anaomba umpe support unaona huyu anaweza kufanya kitu lakini mwisho wa siku ni aibu tuu

Tunakosa utu na nidhamu ya fedha na kiu ya kufanya maendeleo

Acha tufanye au tuchangie na vitu vyenye kutupa furaha chief maana maisha yanahitaji furaha pia
Aisee
 
Back
Top Bottom